Serikali kuwatimua wapiga debe Ubungo tutegemee nini?

jerryempire

JF-Expert Member
Jan 4, 2017
5,128
8,648
Habari,
Ni kawaida kuwakuta wapiga debe ndani ya kituo cha mabasi ya mikoani ubungo,ambao huanzia kituo cha river side mpka ndani ya kituo cha ubungo.

Kazi yao kubwa ilikuwa ni kuwapeleka abiria kwenye mabasi husika na hata kuwasaidia kubeba mizigo ili kupata riski ya chochote kutoka kwa abiria hao

Lakini kwa sasa hali ni tofauti kwani uongozi wa kituo pamoja na askari wametumika kuwatimua kutokufanya shughuli hiyo

Je, Serikali imewawekea njia mbadala ya kujiingizia kipato au kipi tukitarajie kutoka kwa hawa watu zaidi ya 800 baada ya kukoseshwa kazi yao ambayo ilikuwa inawasaidia kuingiza chochote kitu?
 
Wewe ulikuwa unaona sawa wale watu wawepo? Unahisi ni sawa kabisa kuwa na watu 800 kituo kimoja tu cha ubungo kupiga debe tu?

Wewe mkuu ulikuwa ni mpiga debe pale? Najua jibu ni hapana, sasa tuambie serekali ilikupa njia mbadala ya kutafuta ridhiki au ulitafuta mwenyewe?

Tuacheni mambo mengine kuishi kwa mazoea mkuu. Infact serekali imechelewa sana kuwatoa hadi leo. Na inabidi iwatoe wote na hata kwenye vituo vingine hata vya daladala na hata wamachinga mabarabarani
 
Nani anawapa njia mbadala ya kujitafutia ridhiki kule Vijijini? Hao vibaka wakatafute kazi halali.
 
Kazi yao kubwa ilikuwa ni kuwapeleka abiria kwenye mabasi husika na hata kuwasaidia kubeba mizigo ili kupata riski ya chochote kutoka kwa abiria hao

Huwa nashangaa sana mtu ametoka Mbagala, mwingine Gongolamboto, au Mbezi au Kigamboni na amebadili magari kadhaa hapo katikati kwa lengo la kufika UBT, cha kushangaza akishuka tu eneo hilo anasumbuliwa na wapiga debe na wakati mwingine hata kufikia kupoteza baadhi ya vitu vyake vya thamani, je ina maana mamlaka husika zimeridhika na adha hiyo? Je ni kweli mtu anatoka kote huko hajui gari analokwenda kusafiri nalo!!

Ifike wakati watu wapumue wawe na uhuru badala ya kusumbuliwa kiasi kile, mbona hatuoni wapiga debe airport na kwenye mwendokasi ambako mazingira yanafanana kabisa na hapo?
 
Kiukweli wanakera sana, wanatukosesha amani. Mimi ndo maana kwa mabasi yenye ofisi zao nje ya ubungo kama kilimanjaro huwaga my first option hata kama bei zao zipo juu
 
Hao jamaa wanakaa Hadi barabara mpaka barabara imekua finyu hasa pale ofisi za TBS. Inawapasa wakatafute real jobs waachane na ujanja ujanja. Kwanza nashauri mabasi yote yaingie kwenye mfumo wa kukata ticket online
 
LAIS wa wanyonge

Habari,
Ni kawaida kuwakuta wapiga debe ndani ya kituo cha mabasi ya mikoani ubungo,ambao huanzia kituo cha river side mpka ndani ya kituo cha ubungo.

Kazi yao kubwa ilikuwa ni kuwapeleka abiria kwenye mabasi husika na hata kuwasaidia kubeba mizigo ili kupata riski ya chochote kutoka kwa abiria hao

Lakini kwa sasa hali ni tofauti kwani uongozi wa kituo pamoja na askari wametumika kuwatimua kutokufanya shughuli hiyo

Je, Serikali imewawekea njia mbadala ya kujiingizia kipato au kipi tukitarajie kutoka kwa hawa watu zaidi ya 800 baada ya kukoseshwa kazi yao ambayo ilikuwa inawasaidia kuingiza chochote kitu?
 
kwakweli walizidi, japo walikua wanajitaftia chochote, serikali ingewapa 'guide lines' za namna ya kuifanya ile kazi ili kuwapunguzia kero wananchi lakini bila kuwapotezea ajira wale vijana.
kinyume na hapo familia kadhaa zinaenda kuathirika na hili katazo, pengine hata muda huu kuna watoto wa baadhi ya wale vijana hawana uhakika wa kula.
 
Wale jamaa walipelekea abiria kupoteza mizigo yao, ukifika pale watakugombea na mpk vitu vinapotea, walitakiwa kuwaondoa mda mrefu sana!
 
Mazoe mabaya tukubali tu mabadiliko japo yanaumiza ila tujitaid tu kam ulay vile mnk week kadha nilitembeleaa maeneo ugaibuni hakuna wapiga debe rodini
 
Wewe umejengewa mazingira gani ya ajira?
Kazi sio kupiga debe peke yake
Habari,
Ni kawaida kuwakuta wapiga debe ndani ya kituo cha mabasi ya mikoani ubungo,ambao huanzia kituo cha river side mpka ndani ya kituo cha ubungo.

Kazi yao kubwa ilikuwa ni kuwapeleka abiria kwenye mabasi husika na hata kuwasaidia kubeba mizigo ili kupata riski ya chochote kutoka kwa abiria hao

Lakini kwa sasa hali ni tofauti kwani uongozi wa kituo pamoja na askari wametumika kuwatimua kutokufanya shughuli hiyo

Je, Serikali imewawekea njia mbadala ya kujiingizia kipato au kipi tukitarajie kutoka kwa hawa watu zaidi ya 800 baada ya kukoseshwa kazi yao ambayo ilikuwa inawasaidia kuingiza chochote kitu?
 
Wewe ulikuwa unaona sawa wale watu wawepo? Unahisi ni sawa kabisa kuwa na watu 800 kituo kimoja tu cha ubungo kupiga debe tu?

Wewe mkuu ulikuwa ni mpiga debe pale? Najua jibu ni hapana, sasa tuambie serekali ilikupa njia mbadala ya kutafuta ridhiki au ulitafuta mwenyewe?

Tuacheni mambo mengine kuishi kwa mazoea mkuu. Infact serekali imechelewa sana kuwatoa hadi leo. Na inabidi iwatoe wote na hata kwenye vituo vingine hata vya daladala na hata wamachinga mabarabarani
YOU HAVE SPOKEN MY MIND.....SAFI SANA
 
Back
Top Bottom