Serikali kuwasaka wafanyabiashara wanaoficha mafuta au kuuza mafuta juu ya bei elekezi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,501
9,280
WAZIRI wa Nishati, Dk Medard Kalemani ametoa siku saba kuanzia jana kwa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura) na Wakala wa Kuagiza Mafuta kwa Pamoja kuwasaka wafanyabiashara wanaofi cha mafuta au kuuza mafuta juu ya bei elekezi na kuwachukulia hatua za kisheria.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Dk Kalemani alisema kumekuwapo na dalili ya baadhi ya wafanyabiashara hususani wafanyabiashara wakubwa kuficha mafuta kwa kutowauzia wafanyabiashara wadogo.

“Tunazo taarifa za baadhi ya wauzaji mafuta wakubwa kutotaka kuuza mafuta kwa sasa kwa sababu bei ziko chini wakitaka kusubiri bei zipande ili wapandishe bei na Watanzania waumie, jambo ambalo serikali hatualikubali,” alisema.

“Natoa maelekezo kwa Ewura na wakala wa uagizaji mafuta kwa pamoja kuanza operesheni ya kuwasaka wale wanaoficha mafuta kwa lengo la baadaye kupandisha bei ili wapate faida na wananchi aumie.

“Wafuatilieni na muwasake watu wa namna hiyo mkiwakamata chukue hatua za kisheria chini ya Sheria za Ewura ambayo iko wazi kwanza kuna faini si chini ya shilingi milioni 100 na kusitisha shughuli zao,” alisema.

“Wafanyabiashara wa mafuta wanatakiwa kujua kuwa wanatoa huduma kwa wananchi kwa hiyo lazima wazingatie masharti ya leseni zao na kufanya biashara bila kuathiri mapato ya serikali na upatikanaji wa mafuta kwa walaji na mfanye kazi hiyo ndani ya siku saba kuanzia leo (jana) ili tuwabaini wanaofanya hivyo na yoyote atakayepatikana achukuliwe hatua,” alieleza.

Alisema hali ya ufichaji mafuta na upandishaji wa bei zaidi ya bei elekezi ya serikali inatokea sana katika majiji, kama jiji la Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Dodoma na Mbeya na kuwataka kutilia mkazo kwenye ukaguzi huo pamoja na maeneo mengine.

Aidha, Dk Kalemani ameutaka Wakala wa Kuagiza Mafuta kwa Pamoja kuhakikisha wanaendelea kuagiza mafuta hasa ikizingatiwa kuwa uwezo wa nchi katika kuhifadhi mafuta ni lita bilioni 1.2 kwa miezi mitatu huku mahitaji ya nchi kwa kipindi hicho ni lita milioni 750.

Alisema kwa sasa kuna akiba ya mafuta lita milioni 389.6 za mafuta ya deseli, petrol, mafuta ya taa na ndege ndege ambayo yanaweza kutoshereza nchi katika kipindi cha miezi mitatu bila wasiwasi.

Alisema pamoja na uwepo wa mafuta, Serikali inaendelea na uagizaji wa mafuta ambapo jana lita zimepakuliwa lita milioni 90 za mafuta ya diseli na leo zinapakuliwa lita milioni 40 za mafuta ya petrol na lita milioni 2.6 za mafuta ya taa na ndege ambayo yatapakuliwa ndani ya siku mbili zijazo.

“Kwa hiyo hali ya upatikanaji mafuta nchini ni nzuri na inazidi kuimarika,” alieleza. Dk Kalemani alisema bandari za Dar es Salaam, Tanga na Mtwara zinatakiwa kufanya kazi kwa usawa kwani lengo la kuanzisha bandari hizo ilikuwa ni kupanua huduma kwa wananchi ili kusongeza huduma kwa wananchi na zipatikane kwa urahisi.

“Niwatake wafanyabiashara wengine wa mafuta kuendelea kuchukua mafuta kwenye bandari hizo kwani tulifanya hivyo ili kuondoa msongamano wa malori kuchukua mafuta bandari ya Dar es Salaam pekee, na kuepuka uharibifu wa barabara, wito wangu watumie bei linganifu ili wa bei,” alieleza.

“Wito wangu wafanyabiashara wote wahakikishe bei ya mafuta kwa watumiaji zinaendelea kushuka kwa sababu bei katika soko la dunia bado inashuka. Akipatikana mmiliki wa kituo cha mafuta anauza mafuta zaidi ya bei elekezi ya serikali huyo akamatwe mara moja, lazima kushuka kwa bei kunawanufaisha Watanzania,” alisema.

Kuhusu upelekaji wa nishati ya mafuta vijijini, Dk Kalemani alitaka Ewura ukamilisho mapitia ya uanzishwaji wa vituo vya mafuta ili kuwa na vituo vya mafuta vilivyorahisi. Alisema miezi sita ijayo wataanza mradi wa kielelezo wa kupeleka vituo nafuu na kuwa mafanikio ya mradi huo utafanya kuenea maeneo mengine
 
Hakuna anaeficha mafuta sio kila kitu cha kuficha mzunguko wa biashara tu ni mdogo.
 
NINAAMINI KILA MTU AKISIMAMIA KITENGO ALICHOKABIDHIWA KWA UADILIFU, BASI TIIZII ITAFIKA MBALI.
TUNATAKA VIONGOZI KAMA HAWA, NI KWELI LAZIMA KUWE NA UDHIBTI KWANI WASIPODHIBITIWA HAWA WAFANYA BIZNES, BASI LENGO LA MKUU LA KUTETEA WANYONGE HALITATEKELEZEKA.
 
Back
Top Bottom