Serikali kuvifungulia vyombo vyote vya habari

Naipendatz

JF-Expert Member
Jul 27, 2011
5,080
8,218
Serikali imesema ipo mbioni kuvifungulia vyombo vya habari ambavyo bado vimefungiwa mara baada ya kumaliza mazungumzo yanayoendelea hivi sasa baina ya mamlaka na wahusika.

Kauli hiyo imetolewa leo Jumanne, Desemba 7, 2021 na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Amon Mpanju wakati akizindua kikao kazi cha Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) kinachofanya marejeo na kuchambua mapendekezo 252 ya haki za binadamu.

Mpanju amesema lengo la Rais Samia ni kuhakikisha anarejesha uhuru wa vyombo vya habari nchini.

“Hili ni miongoni mwa mapendekezo mliyoyatoa, itakapofika Februari 14 tutasimama na kutaja mapendekezo ambayo Serikali itakuwa imeyakubali na mpaka sasa tayari mengi yameshafanyiwa kazi likiwamo la wasichana wanaopata ujauzito wakiwa shuleni.

“Uhuru wa vyombo vya habari ni jambo ambalo Rais Samia Suluhu Hassan amelisimamia na anahitaji matokeo ya haraka. Tumeshakutana na wadau na jana tumekutana na mamlaka husika kupitia vifungu vyote kuhakikisha kwamba tunavifungulia vyombo vyote vya habari ambavyo vilifungiwa. Rais ameagiza lazima tumalize hili jambo,” amesema Mpanju.

Mwananchi
 
Hayo mazungumzo kati ya serikali na vyombo vya habari yalihusu nini?

Isijekuwa wanavitaka vifanye kazi kwa kufuata mapenzi ya serikali na sio sheria, then vyombo vitakavyoandika jambo la kuiudhi serikali wavifungie.

Simply sheria ya vyombo vya habari inatakiwa kuangaliwa upya, kama serikali ina nia ya dhati kuviondolea uonevu na hujuma zake wabadilishe au wafanyie marekebisho sheria zote zinazovikandamiza.
 
Serikali imesema ipo mbioni kuvifungulia vyombo vya habari ambavyo bado vimefungiwa mara baada ya kumaliza mazungumzo yanayoendelea hivi sasa baina ya mamlaka na wahusika.
Siamini tena media za ndani, kama JF nayo imesalim amri basi
 
Kama hicho kikao ni kwa maslahi ya Taifa na Demokrasia inachukua mkondo, usiri ni wa nini?
Sasa Mkuu Serikali ikisema kila vikao wanavyofanya kila siku, idara zote, viwe vinaripotiwa kwa wananchi, wataweza kufanya kazi nyingine?
 
Anatengana na majambazi taratibu, kwa Stages! Ujambazi wote uliofanyika awamu ya 5 utafutwa mmoja baada ya mmoja! Nchi haiwezi kuishi kama tupo "Stone Ages".
Wewe ni chawa mjinga sana,ukajifunua mbele ya wageni.
 
Kwa hiyo akija Rais mwingine; let's say Madeluu (God forbid) inaweza kuwa utashi wake kufungia vile visivyompendeza au sio?

Suala la uhuru wa habari sio utashi wa nani yuko madarakani; linapaswa kulindwa na Katiba na viongozi kuanzia Rais waheshimu Katiba. Bila Katiba Mpya hatuchomoki kwenye huu mkwamo!
 
Wewe ni chawa mjinga sana,ukajifunua mbele ya wageni.
Kwani ni uongo hawakuwa majambazi? Mengine si yamefungwa tayari miaka 30? Na ishirini mingine inakuja? Kuna siri yeyote? Or kuna lolote watu hawajui kuhusu awamu hiyo? Mengine si yaliiba Bandarini, na Rais mwenyewe akasema?
 
Tunataka katiba ibadilishwe kabla hatujabadili chama tawala maana bila hivyo watapoingia na wao wataweka ngumu ya kutoka huku wakitugalagaza zaidi ya CCM. Mfano halisi ni mwenyekiti wao ambaye hataki kung’atuka kwenye nafasi hio miaka nenda rudi.

I would suggest under new constitution:
-Raisi asiwe mwenyekiti wa chama kuepusha kujikita na interest za chama kuliko taifa na kuvua watu uanachama kwa kukomoa.

- Budget ya bunge isitegemee serikali.

- baraza la mawaziri litoke kwa wananchi.

- wabunge kwa wananchi.

- Tume ya uchaguzi isiwe appointed na rais.

- Watoto wa wastaafu wawe banned kushika nafasi influential za serikalini kama urais, uwaziri atleast waishie kwenye ubalozi labda na hii si kwa ubaya bali kwa manufaa ya umma. Kwa kampuni binafsi wako free kuwa hata wakurugenzi.

- Ajira za serikalini ziwe za mkataba wa 3-5 years huku maslahi yakiboreshwa ili watu wakipata uzoefu warudi kujiajiri. Mikataba iwe extended kulingana na utendaji kama mtu ana perform aongezewe muda.

-Raisi aweze kufunguliwa mashtaka na wananchi direct bila approval ya DPP.
 
Serikali imesema ipo mbioni kuvifungulia vyombo vya habari ambavyo bado vimefungiwa mara baada ya kumaliza mazungumzo yanayoendelea hivi sasa baina ya mamlaka na wahusika...
Sasa warudishe ITV, Channel 10, StarTV, Clouds Tv kwenye ving'amuzi vya DSTV na vinginevyo, mambo yarudi kama tulivyo kuwa 2016 huu ulikua uduwanzi sana.
 
Sasa warudishe ITV, Channel 10, StarTV, Clouds Tv kwenye ving'amuzi vya DSTV na vinginevyo, mambo yarudi kama tulivyo kuwa 2016 huu ulikua uduwanzi sana.
Hahaaaa!!huko hakuna mkuu, sana sana tunazungumzia magazeti, huko kweny tv ni utaratibu tu wa kidunia(ki digital) ndio umelazimisha tufikie huko.kwani kuna wazarishaji wa vipindi(itv, startv, tbc, etc)na wasambazaji kina azam media, startimes, tin)ni jambo la kisheria zaidi.
 
Back
Top Bottom