Serikali kutumia mashahidi 26, vielelezo 86 kesi ya Kisena Wakurugenzi wa UDART

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Upamde wa mashtaka unatarajia kuita mashahidi 26 na vielelezo 82 katika kesi inayowakabili wakurugenzi watatu wa Kampuni ya Huduma za Usafirishaji wa Mabasi yaendayo Haraka (UDART) akiwemo Robert Kisena.

Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka 25 yakiwemo ya wizi, kutakatisha fedha na kuisababishia serikali hasara ya Sh4.4 bilioni.

Mbali na Kisena ambaye pia ni Mkurugenzi wa Simon Group Ltd, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 40/2022 ni Mtendaji Mkuu wa Kampuni Simon Group Ltd, Charles Newe na mfanyabiashara Kulwa Kisena (34).

Hatua hiyo imekuja baada ya upelelezi dhidi ya kesi hiyo kukamilika na upande wa mashtaka kuwasilisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu maelezo ya mashahidi na vielelezo vitakavyotumika wakati wa usikilizwaji wa kesi hiyo katika Mahakama Kuu Kitengo cha Mafisadi.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Achiles Mulisa kuwa katika kesi namba 40 ya mwaka 2022 iliyokuwa inayosikilizwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi, upande wa mashtaka unatarajia kuwaita mashahidi 26 na kuwasilisha vielelezo 82.

MWANANCHI
 
Back
Top Bottom