Serikali: Kutokana na uelewa mdogo, watu wanakunywa bia badala ya maziwa

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,552
Hayo yamesemwa na msajili wa bodi ya maziwa Tanzania, Dk George Msalya wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelekea maadhimisho ya wiki ya maziwa Juni Mosi, 2021 ambapo kitaifa yatafanyika jijini Tanga.

Dk Msalya amewataka Watanzania kuwa na uzalendo wa kutumia bidhaa za ndani za maziwa ili kuwainua wafugaji, wasindikaji na wachakataji wa bidhaa hiyo kwani zipo bidhaa nzuri za maziwa zinazotengenezwa Tanzania.

Amesema Tanzania ina uzalishaji mdogo wa maziwa ambao ni lita bilioni 3.4 ambayo ukigawanya kwa idadi ya Watanzania, kila mtu atakunywa wastani wa lita 50 tu kwa mwaka.

Amesema kwa mujibu wa wataalamu wa afya mtu anatakiwa kunywa maziwa lita 200 kwa mwaka, kwamba bado kuna uhitaji mkubwa wa uzalishaji zaidi wa maziwa ambayo ni muhimu kwa afya ya binadamu.

"Bado uelewa ni mdogo, mtu badala ya kunywa maziwa anakwenda baa kunywa pombe wakati maziwa ni muhimu kuliko hiyo pombe," amesema.

Amebainisha kuwa tangu kuanzishwa kwa bodi hiyo mwaka 2005 Tanzania imepiga hatua katika uzalishaji wa maziwa kwani mwaka 2015 kushuka chini wastani kila mtu alikuwa anakunywa lita 40 hadi 45.

"Kufikia mwaka 2015 hadi 2021 kila mtu anakunywa maziwa lita 50 kwa mwaka ambapo katika pato la Taifa maziwa yanachangia kwa asilimia 30 huku katika sekta ya mifugo ikichangia kwa asilimia saba, " amesema.

Ameeleza kuwa katika maadhimisho hayo yatalenga kufanya tafiti kuhusu tasnia ya maziwa, kujifunza namna ya kufuga ng'ombe bora wa maziwa na kugawa maziwa katika makundi mahitaji kama wagonjwa katika hospitali mbalimbali.
 
Kwa hiyo nikitaka kuludi nyumbani napitia baa kupata mbili tatu ilinipate starter ya kuingilia nyumbani ili kupishana na kelele za mama watoto huyu jamaa ndio ananishauri ninywe maziwa.

Wtf
 
Hayo yamesemwa na msajili wa bodi ya maziwa Tanzania, Dk George Msalya wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelekea maadhimisho ya wiki ya maziwa Juni Mosi, 2021 ambapo kitaifa yatafanyika jijini Tanga...
Huyu atakuwa na kiwanda cha maziwa.
 
Hayo yamesemwa na msajili wa bodi ya maziwa Tanzania, Dk George Msalya wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelekea maadhimisho ya wiki ya maziwa Juni Mosi, 2021 ambapo kitaifa yatafanyika jijini Tanga.

Dk Msalya amewataka Watanzania kuwa na uzalendo wa kutumia bidhaa za ndani za maziwa ili kuwainua wafugaji, wasindikaji na wachakataji wa bidhaa hiyo kwani zipo bidhaa nzuri za maziwa zinazotengenezwa Tanzania.

Amesema Tanzania ina uzalishaji mdogo wa maziwa ambao ni lita bilioni 3.4 ambayo ukigawanya kwa idadi ya Watanzania, kila mtu atakunywa wastani wa lita 50 tu kwa mwaka.
Waanze na wakuu wa mikoa ya Dar na Mwanza ndiyo wenye akili hizo
 
Back
Top Bottom