Serikali kutafuta njia mbadala kushindwa kwa shule za kata

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,174
Serikali kutafuta njia mbadala kushindwa kwa shule za kata


na Victor Masangu, Bagamoyo


amka2.gif
SERIKALI imesema kwamba haijaridhishwa na matokeo ya shule za sekondari za kata ambazo zimefanya vibaya katika mtihani wa kidato cha nne uliofanyika mwaka 2010 huku shule binafsi zikiongoza.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Elimu Mafunzo na Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa, wakati wa sherehe za mahafali ya tisa ya kidato cha sita yaliyofanyika mwishoni mwa wiki katika Shule ya Sekondari Bagamoyo.
Dk. Kawambwa alisema serikali inatakiwa kuangalia kwa makini njia mbadala zinazotumika kufundishia wanafunzi wanaosoma katika shule za seminari.
Aliwataka wanafunzi wanaomaliza kuacha kujiingiza kwenye makundi ya uvutaji wa dawa za kulevya na badala yake watafute njia ya kuendelea na elimu ya juu.
Kawambwa alisema vijana ndiyo nguvukazi ya taifa, hivyo wazazi na walezi wanatakiwa kuhakikisha wanaangalia maendeleo ya watoto wao kila mara.
 
Kama kawaida ya viongozi wetu;majibu mepesi katika maswali magumu!

Suluhisho linaeleweka kabisa. Serikali itimize wajibu wake,baada ya wananchi kutoa nguvukazi na michango ya hali na mali katika ujenzi wa shule hizo,serikali sasa ipeleke waalimu wenye sifa stahili na vifaa vya maabara na wataalamu wake.

Sio huyu Kawambwa anatoa maelezo mepesimepesi!
 
Back
Top Bottom