PreGE2025 Serikali kukamilisha ujenzi wa vituo vya afya ili kutoa huduma stahiki kwa wananchi

PreGE2025 Serikali kukamilisha ujenzi wa vituo vya afya ili kutoa huduma stahiki kwa wananchi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Nipe Maji

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2025
Posts
335
Reaction score
190
Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Festo Dugange amesema Serikali itaendelea kutenga na kupeleka fedha kwenye halmashauri zote nchini kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa miundombinu ya vituo vya afya ili viweze kutoa huduma stahiki kwa wananchi.

Dkt. Duagange ameyasema hayo Bungeni Jijini Dodoma, wakati akijibu swali la Mbunge wa Jimbo la Maswa Magharibi Mashimba Mashauri Ndaki aliyetaka kujua

lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Kituo cha Afya Mwasayi ambacho kimepelekewa vifaa tiba lakini hakina majengo ya kutosha.”

“Mheshimiwa Spika, Kituo cha afya Mwasayi kilianza kutoa huduma katika ngazi ya zahanati mwaka 1962 na kupandishwa hadhi mwaka 1977 na kuanza kutoa huduma ngazi ya kituo cha afya.

Aidha, majengo ya kituo hiki ni machache na chakavu.”

Amesema, katika mwaka wa fedha 2024/25, Serikali imetenga shilingi milioni 250 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la wazazi na jengo la upasuaji katika Kituo cha Afya Mwasayi.
1747740241082.png
 
Back
Top Bottom