The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 1,091
- 1,792
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, amesema serikali itaendelea kusimamia na kutekeleza maagizo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhusu ujenzi wa vituo vya polisi ili kuimarisha ulinzi na usalama wa raia na mali zao.
Mpogolo amepongeza hatua za Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Elihuruma Mabelya, kwa kuanza utekelezaji wa maagizo hayo kwa kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa vituo hivyo katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo.
Akizungumza mwishoni mwa wiki katika kikao na viongozi na wenyeviti wa serikali za mitaa katika Kata ya Bonyokwa, Mpogolo ameeleza kuwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imepeleka shilingi milioni 40 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa Kituo cha Polisi Bonyokwa, huku shilingi milioni 70 zikiwa zimetengwa kwa ajili ya uendelezaji wa mradi huo.
Aidha, miradi mingine ya ujenzi wa vituo vya polisi inaendelea katika kata mbalimbali za jiji hilo. Katika Kata ya Kivule, Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imeidhinisha shilingi milioni 120 kwa ajili ya ukamilishaji wa kituo cha polisi cha kata hiyo. Vilevile, katika Kata ya Majohe, halmashauri hiyo imepeleka shilingi milioni 110.4 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa kituo cha polisi cha eneo hilo.
Kwa upande wa Kata ya Chanika, halmashauri hiyo imetenga shilingi milioni 178.6 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha polisi, huku shilingi milioni 40 zikielekezwa kwenye ujenzi wa Kituo cha Polisi Bonyokwa, ambacho kilianza kujengwa kwa mchango wa Mbunge wa Jimbo la Segerea, Bonnah Kamori, kwa kushirikiana na wananchi wa kata hiyo.
Mpogolo amesisitiza kuwa hatua hiyo inalenga kuimarisha huduma za usalama kwa wakazi wa kata hizo na kuhakikisha Jeshi la Polisi linakuwa na mazingira bora ya kufanyia kazi.
Rais Dkt. Samia, katika maelekezo yake ya hivi karibuni, alielekeza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kushirikiana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, ili halmashauri zisaidie kujenga vituo vya polisi katika ngazi mbalimbali, badala ya jukumu hilo kubaki chini ya Wizara ya Mambo ya Ndani pekee.
Chanzo: Jambo TV