Ferruccio Lamborghini

JF-Expert Member
Apr 15, 2020
1,664
2,517

UWANJA PIC

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mwada wilayani Babati. Picha Mussa Juma


Babati. Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali itajenga uwanja wa ndege wa Mkoa wa Manyara ambao utasaidia kukuza sekta ya utalii.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara katika kijiji cha Mafuta wilayani Babati leo Jumanne Januari 25, 2022 Majaliwa amesema uwanja huo pia utasaidia kuboresha usafiri kwa wakazi wa mkoa huo ambao hauna uwanja wa ndege.

"tutajenga huu uwanja na watu wa Babati, Mbulu, Hanang’ hadi Kondoa ambao watataka huduma ya usafiri wa ndege watapa" amesema

Amesema uwanja huo ni muhimu kwa utalii kwani utapakana na Hifadhi ya Taifa ya Tarangire na ya Manyara.

Awali Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paulina Gekul ambaye ni mbunge wa Babati mjini oliomba Wizara ya Ujenzi kuanza ujenzi wa uwanja huo.

GekuL amesema uwanja huo umepangwa kujengwa katika kata ya Mwada na ukikamilika utaongeza ajira kwa vijana.

Amesema wanaomba Serikali kukamilisha ahadi ya ujenzi huo kwani utaibua fursa nyingi za kiuchumi mkoani Manyara.
 
Huu uwanja ungejengwa Karatu tuu kwani kuna traffic kubwa ya tourists

Karatu kuna airstrip moja inaitwa manyara. Kuna siku nimeona ndege za utalii zaidi ya 40 zikiruka na kutua kwa siku moja na nilikuwa eneo hilo kwa masaa kama 4 hivi.
 
Huu uwanja ungejengwa Karatu tuu kwani kuna traffic kubwa ya tourists

Karatu kuna airstrip moja inaitwa manyara. Kuna siku nimeona ndege za utalii zaidi ya 40 zikiruka na kutua kwa siku moja na nilikuwa eneo hilo kwa masaa kama 4 hivi.

Ushauri mzee, natumaini wataufanyia kazi.
 
Hakuna Umbali kutoka Mbuyuni hadi karatu nafikiri saa1 na nusu au 2 pia watalii hao hao wanaoshuka Manyara airport wanaenda Tarangira na lake Manyara
 
Back
Top Bottom