Rufiji,
Nimekupata.
Nilivyoelewa mimi, na hata habari nilizowahi kuzisikia kabla hata JK hajawa rais (mwaka 2000), ni baadhi ya wataalam ndiyo waliopendekeza kuhusu kuhamishia bandari nje ya jiji la Dar.
Nilivyoelewa mimi pia, ni kuwa bandari inayokusudiwa ni pale Mbegani, kwenye chuo cha uvuvi, ambacho sijui kama sasa kinafanya kazi (nilitembelea pale mwaka 2000 kikiwa hoi bin taaban), na si Bagamoyo penyewe kwenye bandari ya enzi za biashara ya utumwa (Boma House, Liku etc). Ni kweli Mbegani iko karibu na Bagamoyo "proper" lakini si sahihi kusema Mbegani ni sawa na Bagamoyo.
Hoja za kujenga au kupanua bandari ya Mtwara nilizizungumzia hapo juu kuonyesha changamoto zake. Kuhusu kina cha bandari ya Mbegani (si Bagamoyo) sina takwimu zake kama ambavyo sina za Mtwara licha ya kusikia tu kuwa Mtwara kuna kina kirefu.
Nionavyo mimi, bandari inaweza kujengwa popote, ili mradi vigezo vya kiufundi na kiuchumi vinazingatiwa (technical and economic considerations). Na uamuzi huo uzingatie mipango ya muda mrefu au uwe sehemu ya mkakati kabambe (strategic plan) kwa mfano ya sekta ya usafirishaji, viwanda, biashara au masoko. Kwa mfano, itakuwa haina maana kama serikali itaamua tu kujenga au kupanua bandari (iwe Dar, Tanga au Mtwara) bila kwanza kuwa na mipango ya usafirishaji wa mizigo hiyo kwenda na kutoka bandarini hapo, masoko na huduma nyingine muhimu za kibiashara.
Kwa muda mrefu Dar itabaki kuwa "katikati" ya Tanzania na si Dodoma kutokana na upatikanaji wa huduma muhimu za mawasiliano na uchumi kwa ujumla: Dar inaunganisha kirahisi njia za reli ya kati na TAZARA, barabara kuu mbalimbali ikiwemo Cape to Cairo, na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Nyerere (kumbuka kuwa wateja hasa wa nchi jirani wanaweza kulazimika kufuatilia mizigo yao "physically" hivyo umuhimu wa usafiri wa uhakika). Hiyo inafanya bandari iliyo "karibu na Dar" kuwa na "advantage". Viwanda vingi ambavyo hatimaye vitasafirisha bidhaa kwenda nje au kupokea mahitaji yake kutoka nje (malighafi nk) viko Dar! Mbegani iko karibu na Dar na hivyo inapata "advantage" hiyo.
Nitapinga uamuzi wa kujenga bandari popote pale ikiwa utakuwa umefanywa kwa sababu za kibinafsi, kisiasa, kikabila au kimajimbo.
Ni kweli tunahitaji maendeleo ya haraka kwani tushachelewa mno. Tunahitaji viwanja vya ndege vingi na bandari nyingi zaidi tena kwa ubora wa juu. Inawezekana waziri wa mawasiliano wa wakati huo alipendelea kwao, lakini binafsi naunga mkono kuwa na uwanja wa ndege mzuri na mkubwa si Mbeya tu (sijui wajenzi wa huo uwanja wa Songwe nao wamefikia wapi) bali katika miji mingine ikiwemo Mwanza, Kigoma, Mtwara, Dodoma na Tabora. Watunga sera na mipango wetu waangalie mbele. Nijuavyo, uwanja wa Songwe unachukuliwa kuwa umo katika Mtwara Development Corridor Project ambayo pia nadhani imesinzia kama si kulala usingizi wa pono!