Serikali Kujenga bandari Bagamoyo !

Rufiji

Platinum Member
Jun 18, 2006
1,871
901
Nimesoma hii habari ambayo waziri mkuu alikuwa akimjibu Lipumba madai kwamba Rais apunguze safari za nje.

Mheshimiwa alianza kwa kusema kuwa ,safari za nje zimemwezesha JK kujitangaza nje na pia kutana na wahisani . Mheshimiwa akuishia hapo akatoa mafanikio yaliyoapatikana ni pamoja na kupata mikopo ya kujenga chuo cha DODOMA na kujenga Bandari Bagamoyo, Mbegani .

Swali langu ni kuwa kuna umuhimu wa kujenga bandari Bagamoyo? Vipi mbona tuna bandari mtwara ambayo ina kina kirefu sana na hatuitumiii kabisa (Underutilized). Je, hawa viongozi wanajua ya kuwa hiyo mkopo at the end of the day inatakiwa kulipwa? Na kwa nini hiyo bandari ijengwe bagamoyo , ambayo hiko karibu sana na Dar?

Kwa nini hiyo mikopo isitumiwe kwenye mambo muhimu badala ya kunufaisha sehemu ambayo Rais wetu ametoka.

Chanzo: Nipashe
 
Kwa sasa naweza kujisadikisha kuwa pendekezo au uamuzi wa kujenga bandari Mbegani haukufanywa kwa nia ya "kupendelea" kwao JK...
Kunaweza kuwa na hoja zifuatazo kutetea uamuzi huo. Mathalani:
1. Kumekuwa na mpango wa siku nyingi wa kupunguza msongamano katika barabara kuu ya Morogoro sehemu ya Dar--Chalinze. Wazo lililokuwepo ni kujenga barabara kutokea Bagamoyo kupitia Saadani, kuibukia maeneo ya Chalinze/Msata/Lugoba, na hivyo kuendelea mpaka Moshi-Arusha-Nairobi. Mpaka sasa kuna barabara fulani pale ya vumbi kutokea maeneo hayo (nadhani Mkata ya Pwani - si ile ya Tanga) kwenda Bagamoyo.

2. Inasemekana kuwa kina cha bandari ya Dar es Salaam kwa sasa ni kifupi/kimepungua na kuna meli zimewahi kukwama, na kuna madai kuwa kuna meli kubwa zinashindwa kutia nanga Dar es Salaam kutokana na tatizo hilo. Hakika hivi sasa kuna mpango wa kuongeza kina na kupanua bandari na tathmini imefanywa ya watu watakaohamishwa maeneo ya Shimo la Udongo, kwa mfano.
Hoja hii ya kiufundi, hata hivyo, wakati inathibitisha kuwepo haja ya kuongeza kina, inakinzana na mpango wa kujenga bandari Mbegani. Kwa nini kupanua bandari ya Dar wakati kuna mpango wa kujenga hiyo ya Mbegani?

3. Kujenga bandari Mbegani kutapunguza magari makubwa ya mizigo yanayoingia mjini Dar, hivyo kupunguza msongamano katika barabara za Mandela na Morogoro. Hii itasaidia watumiaji wa barabara hizo jijini. Tufahamu kuwa hivi sasa msongamano barabarani umekuwa kero kubwa jijini.

4. Ujenzi wa bandari Mbegani utakuwa wa maana pia kama utahusishwa au umezingatia ongezeko la mizigo katika bandari ya Dar-kama lipo au limepangwa kuwepo, kwa kuhamasishwa na kuboresha huduma ili jamaa zetu wa Burundi, DRC, Malawi, Rwanda, Uganda na Zambia, watumie zaidi bandari za Tanzania.

5. Ni kweli Bagamoyo ni karibu na Dar, na kweli Mtwara haijatumiwa vizuri. Sababu za Mtwara kutotumiwa ni nyingi ikiwemo miundombinu hasa barabara na majengo mengine kwa ajili ya watoa huduma (hoteli, ofisi nk). Ukweli kwamba Bagamoyo ni karibu na Dar (70km) huenda kukafanya baadhi ya watoa huduma kuendelea kutumia ofisi zao na makazi Dar huku waiendelea na shughuli, tofauti na kama ingekuwa Mtwara ndiyo chagua. Huenda pia bandari ya Mtwara iko kwenye mpango wa Mtwara Development Corridor ambao ni mradi unaohusisha nchi za SADC lakini utekelezaji wake umekuwa unasuasua.

6. Ujenzi wa bandari Mbegani pia utasaidia kuchochea maendeleo katika wilaya ya Bagamoyo ambayo ni moja ya wilaya zilizo nyuma kimaendeleo.

7. Kuweka bandari Mbegani pia kutaongeza udhibiti wa eneo hilo la bahari ya Hindi, ambalo kwa sasa, inadaiwa kuwa linakabiliwa na vitendo vingi vya haramu ikiwemo kuingiza bidhaa za magendo/kukwepa ushuru, dawa za kulevya, na uvuvi haramu wa kimataifa. Kwa sasa eneo hilo halidhibitiwi vema na serikali.

Kwa sasa nichangie hivyo.
 
Mwanagenzi ,

Akhsante sana kwa michango yako madhubuti , ila nataka nikuulize swali moja tuu unajua ya kuwa tuna bandari kubwa na yenye kina kirefu inayoitwa bandari ya mtwara , kwa nini tutumie mamilioni ya shilingi katika kujenga bandari nyingine wakati tuna bandari yenye kirefu sana hapo mtwara .

Kwa hiyo kama sehemu kuna uhalifu , solution ni kujenga bandari na sio kuongeza doria katika eneo husika ! kama kweli lengo ni kupunguza msongamano wa magari makubwa then mtwara ndio solution na kwa nini tutegemee nchi za SADC katika kufanya maamuzi yetu ?


Vipi kuhusu kina cha maji hapo bagamoyo ?
 
Mwanagenzi ,

Naomba usome hii article nadhani utajua sababu iliyofanya bandari ya bagamoyo iache kutumika kwenye karne ya kumi na nane ,

''The decline of the town was initiated when the harbour was too shallow to accommodate modern ships. The German government in 1891 decided to move the new capital of their new crown colony from bagamoyo to the new city.''

Source ;

http://www.webspawner.com/users/bobapache/
 
Ukisikia matumizi mabaya ya pato la taifa ndiyo haya!

Hiyo bandari siyo priority kwa sasa. Ukiona mtua nasema ni muhimu kwa sasa kujengwa hiyo ujue huyo ana lake la ukanda au ..

Kila rais/kiongozi akija akaacha priority na kujiamulia kufurahisha watu wa eneo lake kweli tanzania itajengwa na kufika?!

Mfano kuna wakati fiulani mwaka jana kabla ya Uchaguzi niliwahi kusikia kuwa kiwanja cha ndege kitajengwa Mbeya!! N ahii yoye ni kwa kuwa waziri muhusika alikuwa anatoka huko.


Hivi sasa kama kuna mtu anafuatilia ziara za waziri mkuu toka achaguliwe utagundua amefanya ziara nyingi sana ARUSHA hata kumi zinaweza kufika!

Hatumkatazi mtu kwenda kwao, asizifanye ziara za kitaifa!

hayao ni matumizi mabaya ya fedha za taifa. Je ameisha wahi kufika rukwa kwa mfano???

Ndugu Lowassa tunakuona PUNGUZA ZIARA ZA ARUSHA PLEASE!

IKITOKEA UKAWA RAIS WA TANZANIA UTAHAMISHIA MAKAO MAKUU ARUSHA BELIEVE ME!!
 
Ndugu JK rais wa Tanzania .Najua umesha fanya uamuzi na umesha tangazia Taifa juu ya ujenzi wa Bandari nyumbani kwako ila naomba oia uangalie namna ya kuifufua na kuipa nguvu bandari ya Mtwara iwe msaada kwa watu wa Mtwara kwa ajira , usafiri na pia kuipa Tanzania nafasi ya kuwa na bandari kubwa ikiwepo Mbegani na Mtwara pia Dar .Fanya hili ndugu Rais kwa manufaa ya Tanzania na vizazi vijavyo na zaidi ya hapo .
 
Rufiji,
Nimekupata.
Nilivyoelewa mimi, na hata habari nilizowahi kuzisikia kabla hata JK hajawa rais (mwaka 2000), ni baadhi ya wataalam ndiyo waliopendekeza kuhusu kuhamishia bandari nje ya jiji la Dar.

Nilivyoelewa mimi pia, ni kuwa bandari inayokusudiwa ni pale Mbegani, kwenye chuo cha uvuvi, ambacho sijui kama sasa kinafanya kazi (nilitembelea pale mwaka 2000 kikiwa hoi bin taaban), na si Bagamoyo penyewe kwenye bandari ya enzi za biashara ya utumwa (Boma House, Liku etc). Ni kweli Mbegani iko karibu na Bagamoyo "proper" lakini si sahihi kusema Mbegani ni sawa na Bagamoyo.

Hoja za kujenga au kupanua bandari ya Mtwara nilizizungumzia hapo juu kuonyesha changamoto zake. Kuhusu kina cha bandari ya Mbegani (si Bagamoyo) sina takwimu zake kama ambavyo sina za Mtwara licha ya kusikia tu kuwa Mtwara kuna kina kirefu.

Nionavyo mimi, bandari inaweza kujengwa popote, ili mradi vigezo vya kiufundi na kiuchumi vinazingatiwa (technical and economic considerations). Na uamuzi huo uzingatie mipango ya muda mrefu au uwe sehemu ya mkakati kabambe (strategic plan) kwa mfano ya sekta ya usafirishaji, viwanda, biashara au masoko. Kwa mfano, itakuwa haina maana kama serikali itaamua tu kujenga au kupanua bandari (iwe Dar, Tanga au Mtwara) bila kwanza kuwa na mipango ya usafirishaji wa mizigo hiyo kwenda na kutoka bandarini hapo, masoko na huduma nyingine muhimu za kibiashara.

Kwa muda mrefu Dar itabaki kuwa "katikati" ya Tanzania na si Dodoma kutokana na upatikanaji wa huduma muhimu za mawasiliano na uchumi kwa ujumla: Dar inaunganisha kirahisi njia za reli ya kati na TAZARA, barabara kuu mbalimbali ikiwemo Cape to Cairo, na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Nyerere (kumbuka kuwa wateja hasa wa nchi jirani wanaweza kulazimika kufuatilia mizigo yao "physically" hivyo umuhimu wa usafiri wa uhakika). Hiyo inafanya bandari iliyo "karibu na Dar" kuwa na "advantage". Viwanda vingi ambavyo hatimaye vitasafirisha bidhaa kwenda nje au kupokea mahitaji yake kutoka nje (malighafi nk) viko Dar! Mbegani iko karibu na Dar na hivyo inapata "advantage" hiyo.

Nitapinga uamuzi wa kujenga bandari popote pale ikiwa utakuwa umefanywa kwa sababu za kibinafsi, kisiasa, kikabila au kimajimbo.

Ni kweli tunahitaji maendeleo ya haraka kwani tushachelewa mno. Tunahitaji viwanja vya ndege vingi na bandari nyingi zaidi tena kwa ubora wa juu. Inawezekana waziri wa mawasiliano wa wakati huo alipendelea kwao, lakini binafsi naunga mkono kuwa na uwanja wa ndege mzuri na mkubwa si Mbeya tu (sijui wajenzi wa huo uwanja wa Songwe nao wamefikia wapi) bali katika miji mingine ikiwemo Mwanza, Kigoma, Mtwara, Dodoma na Tabora. Watunga sera na mipango wetu waangalie mbele. Nijuavyo, uwanja wa Songwe unachukuliwa kuwa umo katika Mtwara Development Corridor Project ambayo pia nadhani imesinzia kama si kulala usingizi wa pono!
 
wanagenzi,

Kuhusu bandari ya mtwara , mimi nilipata bahati ya kufika pale na kuongea na manahodha wa meli moja kubwa kabisa iliyokuwa inapakia korosho , na yule captain aliniambia ya kuwa aikuwa ngumu kabisa kuingiza meli pale kwani kima chake ni kikubwa sana ! Unajua ya kuwa kama kungekuwa na barabara nzuri kutoka Mtwara ----Tunduru ----songea meli nyingi zinazoleta mizigo ya zingeenda mtwara . Mimi ninachojiuliza ni kuwa kwa vile nchi yetu ni maskini ni lazima tuwe makini sana katika kutumia scarce resources tulizokuwa nazo , aingii akilini kabisa kitendo cha kujenga bandari nyingine wakati unayo bandari nzuri kubwa " natural " pale mtwara !

Mwanagenzi unapozungumzia umbali hakuna umbali wowote kati ya Dar na mtwara kama barabara ingekuwa nzuri ni mwendo wa masaa sita mpaka saba , na hili suala la kupanua bandari ya mtwara umelipata wapi ? bandari ya mtwara aihitaji hilo ni natural na ina kina cha kutosha tofauti na Bagamoyo ,Dar . Ni kweli tunahitaji maendeleo lakini tuangalie priority , kwa nini tujenge bandari nyingine wakati tungeweza kutumia hizo hela kwenye sekta nyingine kama afya , umeme na elimu. Uamuzi huu ni wa kisiasa sana na sio kiuchumi , Kikwete anajaribu kupeleka maendeleo kwao kwa gharama ya watanzania .

Lakini simalumu JK na CCM , NAWALAUMU WATANZANIA WALIOLALA NA WASIOJUA NCHI YAO INAELEKEA WAPI.
 
Kama yote hayo yako kwenye ilani yao ya uchaguzi ya mwaka jana, basi sina gogoro.

Maana hiyo ndiyo iliyowaweka madarakani!


ILa Mnasemaje kuhusu ziara za LOWASSA huko arusha? au si kweli kwamba zimezidi? fanyeni utafiti bandugu. Niwekeni sawa!
 
Jamani mtu kwao .Anataka kukumbukwa si kama Mwalimu alivyo waacha watu wa Musoma watupu . Hizi ni zama za mtu kwao hata ukisema ni Mbegani basi bado ni Bagamoyo hiyo sijaona tofauti lakini kuiendeleza bandari ya Mtwara ingalikuwa big plus naamini na watu wa Mtwara wapate kusikikana kupata ajira .Kuna mengi yanaandaliwa kwa ajili ya Bwagamoyo na haya sasa yataleta malalamiko . Yangu macho .
 
Nafikiri Tanga ingekuwa chaguo langu.
Mtwara pia kuharakisha maendeleo ya mikoa huko kusini.
 
Siyo Tz tena jamani , Tumeambiwa ni Wachina ! Kwa mkataba wa kujilipa wa 50 years , Shortly , ni mpaka pale jf members wote mtakapokuwa mmekufa , maana inasemekana ' eti ' hamna Dogo !
 
...Na walipa deni hili watakuwa ni walipa kodi na vizazi vyao hasa kutoka tanga,lindi na mtwara ambapo simple economics zipo wazi kwamba upgrading bandari zile na pia investing katika viwanda kule kutakuwa na manufaa zaidi kwa walipa kodi tanzania kuliko kufanya haya bagamoyo as a greenfield investment;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Nimesoma hii habari ambayo waziri mkuu alikuwa akimjibu Lipumba madai kwamba Rais apunguze safari za nje.

Mheshimiwa alianza kwa kusema kuwa ,safari za nje zimemwezesha JK kujitangaza nje na pia kutana na wahisani . Mheshimiwa akuishia hapo akatoa mafanikio yaliyoapatikana ni pamoja na kupata mikopo ya kujenga chuo cha DODOMA na kujenga Bandari Bagamoyo, Mbegani .

Swali langu ni kuwa kuna umuhimu wa kujenga bandari Bagamoyo? Vipi mbona tuna bandari mtwara ambayo ina kina kirefu sana na hatuitumiii kabisa (Underutilized). Je, hawa viongozi wanajua ya kuwa hiyo mkopo at the end of the day inatakiwa kulipwa? Na kwa nini hiyo bandari ijengwe bagamoyo , ambayo hiko karibu sana na Dar?

Kwa nini hiyo mikopo isitumiwe kwenye mambo muhimu badala ya kunufaisha sehemu ambayo Rais wetu ametoka.

Chanzo: Nipashe


8575_156443791185493_610613214_n.jpgMajina ni kati ya HAYO MATANO kati ya WATU MASHUHURI waliosimama katika PICHA... PRINCE yuko katika kila kitu hivi 2015 atagota hapo IKULU? sababu labda watabadilisha PRESIDENTIAL TERMS from 10 to LIFE; like what MUSEVENI
 
Kama raisi anadhani kujenga bandari Bagamoyo kutawanufaisha wazawa wa eneo hilo atakuwa amekosea sana... maana wa moja havai mbili...
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom