Serikali kujaribu kutumia Helikopta ili kuzima Moto unaoendelea kuwaka Mlima Kilimanjaro

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
Serikali ya Tanzania inatazamiwa kutuma helikopta na ndege katika mlima Kilimanjaro nchini Tanzania kujaribu kuuzima moto unaendelea kuwaka kwa siku ya saba sasa.

Hayo ameyasema Waziri wa utalii nchini humo Dkt Hamis Kigwangala baada ya moto kuendelea kuwaka katika mlima huo.

Jana Waziri Kigwangala alitangaza kuwa wameweza kuudhibiti moto huo, lakini baadaye moto huo ulisaambazwa zaidi na upepo uliovuma katika mlima huo.

Katika ujumbe wake wa Twitter Waziri Kigwangala amethibitisha kuwa moto unaendela kuwaka tatika mlimo huo mrefu zaidi barani Afrika.
1602747275914.png

#MzeeWaField kazini Mlimani Kilimanjaro jana. Bado tunahangaika na kuzima moto. Kazi ni ngumu na kubwa kuliko inavyodhaniwa. Changamoto ni upepo mkali na kukauka kwa nyasi na vichaka. Taratibu zikikamilika leo tutaweza kuanza kutumia Helicopters na ndege kuzima moto. #HK

Mkuu hili wazo lako bila mpango mkakati mzuri wanawezakujikuta wameuchoma mlima wote :D
Unatengeneza Moto unaoweza kuumudu kikubwa upaunguze pale ambapo ule Moto ulioushindwa usiweze kuendelea yani unapawasha panaungua then unazima kabla haujakolea vilivyo.. Kama hawawezi basi wapeleke matrekta Kama Kuna nyasi izilaze kuwe udongo Moto ukifika uishie hapo Kama ni changanyikeni ya miti Basi na wapambane..😅
 
Mkuu shida ni hapo kwenye kuweza kuumudu, wanaweza kutengeneza tatizo kubwa kuliko hata hili lililopo sasa hivi, ngoja tuone hizo helikopta huenda zikasaidia
 
Mlima hauungui hata kidogo upo kama ulivyo Siku zote.. Na wala mlima hauna kitu chochote kinachoweza kushika moto... Kwa maana ni miamba na mawe tu
Kinachoungua ni misitu mifupi na nyasi za nyika inayozunguka mlima

Hata moto ukiendelea. Kuwaka kwa Mwezi mzima bado sana kuufikia mlima ulipo na sehemu iliyoungua mpaka sasa ni asilimia 1.6℅ tu ya uoto unaozunguka mlima.
Mkuu hili wazo lako bila mpango mkakati mzuri wanawezakujikuta wameuchoma mlima wote :D
 
Serikali ya Tanzania inatazamiwa kutuma helikopta na ndege katika mlima Kilimanjaro nchini Tanzania kujaribu kuuzima moto unaendelea kuwaka kwa siku ya saba sasa.

Hayo ameyasema Waziri wa utalii nchini humo Dkt Hamis Kigwangala baada ya moto kuendelea kuwaka katika mlima huo.

Jana Waziri Kigwangala alitangaza kuwa wameweza kuudhibiti moto huo, lakini baadaye moto huo ulisaambazwa zaidi na upepo uliovuma katika mlima huo.

Katika ujumbe wake wa Twitter Waziri Kigwangala amethibitisha kuwa moto unaendela kuwaka tatika mlimo huo mrefu zaidi barani Afrika.
View attachment 1600836
#MzeeWaField kazini Mlimani Kilimanjaro jana. Bado tunahangaika na kuzima moto. Kazi ni ngumu na kubwa kuliko inavyodhaniwa. Changamoto ni upepo mkali na kukauka kwa nyasi na vichaka. Taratibu zikikamilika leo tutaweza kuanza kutumia Helicopters na ndege kuzima moto. #HK

Magufuli ameshatoa tamko

Nileteeeni Gwajimaaaaaa
Nileteeeni Gwajimaaàaaaaaaaaaa
Nileteeeni Gwajimaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
Nileteeeeni gwajimaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
Nileteeeeni gwajimaaaaaàaaaaaaaaaàaaaaàaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Salaam wakuu,naomba mlioko Kilimanjaro mtupe taarifa ya uhakika,nini chanzo cha moto unaowaka hapo mlimani!?

Je, harakati za uzimaji zimefikia wapi? Nasikia bado unawaka na ni mkubwa. Je, ni kweli?
 
sasa mvua inanyesha
 
Tayari umezimika
Jana mvua ilinyesha
 
Back
Top Bottom