Moto uliowaka Mlima Kilimanjaro kwa wiki nzima wadhibitiwa

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,118
Moto uliozuka katika Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro nchini Tanzania karibu na eneo la Karanga Camp umedhibitiwa huku eneo lenye ukubwa wa kilometa za mraba 2 hadi 4 zimeteketea.

Akizungumza na waandishi wa habari, Ijumaa Oktoba 28, 2022 katika lango la Mweka, Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Pindi Chana amesema chanzo cha moto huo bado hakijafahamika.

Moto huo ulianza kuwaka Oktoba 21, 2022 katika eneo la Karanga lililopo urefu wa meta 3,963 kutoka usawa wa bahari kupitia njia ya Mweka, hadi sasa hakuna madhara yoyote ya kibinadamu yaliyojitokeza na shughuli za utalii zinaendelea.

"Hivi sasa naomba niseme moto katika Mlima Kilimanjaro umedhibitiwa na hivi sasa nimetoka kuzunguka juu na Helkopta nimeshuhudia moto umedhibitiwa maeneo mengi ukiacha maeneo machache ambayo yalikuwa yana moshi.

"Niseme kwa sasa hali ni shwari lakini wakati umefika sasa tukumbushane ndugu zangu watanzania, Moto ni changamoto, tujitahidi sana kuepuka matumizi mabaya ya moto, kwani moto ukiwaka katika misitu, hifadhi na mashamba, unaleta hasara kubwa sana" amesema.

Akizungumza Kamishina wa Uhifadhi Kanda ya Kaskazini, Betrita James amesema eneo la hifadhi ya Kilimanjaro lililoathirika na moto huo ni Kilometa za mraba 2 hadi 4.

"Moto umedhibitiwa, hadi kufikia jioni ya leo, tumeona matumaini, tulikuwa na moto mmoja ambao ulikuwa korongo la karanga lakini kutokana na juhudi zilizofanywa pamoja na vikosi vilivyokuwa mlimani, tumeona mafanikio makubwa na tuna imani moto kwa sasa umedhibitiwa na shughuli ya kuuzima moto inakwenda kufika ukingoni".

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Moshi, Abbas Kayanda amewashukuru wadau wote ambao wameonyesha ushirikiano wao katika kuhakikisha moto unadhibitiwa katika Mlima Kilimanjaro.

mwananchi
 
Bado ninavyoandika hapa moto bado umepamba mlima Kilimanjaro . Waziri aache kusema uongo
 
Aaah tusishangae kesho tena umewaka

Tupo baranco hapa Moto umetuzuia kwenda karanga(meseji ya asubuhi ya leo toka kwa kijana wangu aliyopo mlimani)
 
Back
Top Bottom