Serikali kujaribu kutumia Helikopta ili kuzima Moto unaoendelea kuwaka Mlima Kilimanjaro

Salaam wakuu,naomba mlioko Kilimanjaro mtupe taarifa ya uhakika,nini chanzo cha moto unaowaka hapo mlimani!?

Je, harakati za uzimaji zimefikia wapi? Nasikia bado unawaka na ni mkubwa. Je, ni kweli?
Pale ni volcano si kingine.

Tyr ushazima
 
Hakika we ni mtu pori
[Q UOTE="KENZY, post: 37009966, member: 345804"]
Kwanini wasitumie mbinu ya kuwasha moto mwengine kwa mbele Kisha wanauzima ili ule unaowaka ukifika ukose pa kuendeleza kuwaka..
[/QUOTE]
 
Kwanini wasitumie mbinu ya kuwasha moto mwengine kwa mbele Kisha wanauzima ili ule unaowaka ukifika ukose pa kuendeleza kuwaka..
Hii mbinu nilishuhudia kijijin wangechelewa nyumba zingeungua, walidai moto unaspeed nguvu ya kuudhibiti ni ndogo ikabidi wawashe mdogo wake vikakutana hali ikatengamaa
 
Kwanini wasitumie mbinu ya kuwasha moto mwengine kwa mbele Kisha wanauzima ili ule unaowaka ukifika ukose pa kuendeleza kuwaka..
Asante sana mkuu, bila shaka utakuwa umekulia kijijini kama mimi....kila siku huwa najiuliza kwanini watu hawakumbuki mbinu hii?
 
HII NDO THE BEST STRATEGY KUKABILIANA NA MOTO UNAOSAMBAA,SWALI NI JE WAMEJIPANGA VIZURI KUITUMIA HII NJIA
Kwa hali ya kawaida unapaswa kuwa na mipango ya kukabiliana na janga ambalo linaweza kujitokeza. Tatizo letu tunangoja hadi hapo janga linapotokea ndio tunaanza kupanga mipango ya kulitatua. Hapakuwepo na ndege za kuzima moto, sasa tunahangaika kuzitafuta baada ya kuona kwamba huu moto si wa kuzima kwa kutumia majani ya miti. Mtindo huu ni kwa mioto midogo tu na kamwe haufai kwenye moto huo wa milimani unaochochewa na upepo uendao kasi. Matokeo yake wazimamoto huchoka na kuamua kupumzika na hivyo kuupa nafasi moto uendelee kuwaka kwa nguvu mpya na kasi mpya. Kwa kutokuwa na mipango mizuri sasa tutavuna majivu na jangwa katika misitu yetu.
 
Kwanini wasitumie mbinu ya kuwasha moto mwengine kwa mbele Kisha wanauzima ili ule unaowaka ukifika ukose pa kuendeleza kuwaka..
Hi njia inawezekana Kama kukiwa hakuna upepo, ila upepo ukiwepo ni sawa na kumshauri magu tu, maana haiwezekani.
 
Back
Top Bottom