Serikali kuifutia leseni kampuni ya simu ya Manji

Serikali kuifutia leseni kampuni ya simu ya Manji

Awaombe radhi waislamu waliomuombea dua mbaya kama vile watu Wa Kibaha na Mvomero walivyomuombea dua mbaya Sumaye. Mrema yeye ilibidi awaombe radhi, angalau rasha rasha imemfikia.

Kumbe Mungu wenu ni wa visasi ?
 
Kina Bill Gates wangefanyiwa hivi na serikali zao hii misaada wanayotupa tungeipata wapi?

Watakaopoteza ajira wakale wapi?

Anyway,madaraka yana mwisho.
Manji unaweza kumlinganisha na Bill Gate?? Huyu mkwepa kodi wa kutupwa?? Angekuwa Marekani angekuwa amefungwa na kufilisiwa zamani sana mkuu!!
 
nimesoma weee lakini hayo masharti yaliyokiukwa sijayaona


TCRA semeni ni maagizo kutoka juu
 
Jamani waliokuwepo karibu na wafanya maamuzi ya nchi plz tunaomba msikurupuke tena kwenye hili tukaja kulipishwa mabilioni mengine kwa kuifungia kampuni pasipo kufuata njia sahihi..

Kumbukeni nchi inapolazimishwa kulipa mafidia ya kijinga ambayo yangewezwa kukwepwa mapema tunaoumia ni sie akina pangu pakavu kwa makodi kupandishwa ghafla kufidia hilo deni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unamlinganisha Manji na Bill gates?
unatakiwa uelewe logic ya comment

unapomfungia kampuni humkomoi manji peke yake unawakomoa wale maskini wanaotegemea kaz mule

serikali yenye kujali raia zake ingemlamba faini kubwa then aendelee kufanya shughuli zake sasa
kuliko kuifungia kwamba tukose wote alaf then wat??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Walimuombea dua mbaya kisa nini.? Na kumbe ndivyo mafundisho yao yalivyo? Naomba kueleweshwa.
Kama mtu akikukosea na huna uwezo wa kumfanya unamfikishia nung'uniko lako kwa Mwenyezi Mungu tu.. actually sio Dua baya bali ni shitaka unaliwasilisha kwa Mola aamue.. ila u make sure na wewe u msafi ndipo shitaka lako litafanyiwa kazi... hautakiwi kuchukua maamuzi mabaya kama kumpiga au kumuua aliyekukosea Dua tu yatosha dini zote nadhani zinaelekeza hivyo kama ukishindwa samehe..
 
Serikali inaamini kua
Kumchukia TAJIRI NA MFANYABIASHARA NDIO CHACHU YA MAENDELEO NA UCHUMI KUKUA ZAIDI

Sent from Calculator Phone vesion007
 

Dar es Salaam. Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetangaza kusudio la kufuta leseni ya Kampuni ya Mycell inayomilikiwa na Quality Group Limited (QGL) ambayo imekuwa ikiongozwa na mfanyabiashara maarufu nchini, Yussuf Manji.

Kwa mujibu wa sheria, TCRA iliyoanzishwa mwaka 2003 ina jukumu la kusimamia, kutoa na kufuta leseni za mawasiliano kwa kampuni yoyote ambayo imeshindwa kutekeleza majukumu iliyoyabainisha.

“Kampuni ya Mycell imeshindwa kurekebisha ukiukwaji wa masharti ya leseni,” inasomeka taarifa iliyotolewa na kuwekwa kwenye tovuti ya mamlaka hiyo.

Kutokana na upungufu huo, “TCRA inauarifu umma kuhusu kusudio la kufuta leseni za Mycell za kujenga miundombinu kitaifa, kutoa huduma kupitia miundombinu hiyo, kutoa huduma kupitia mtandao na kutumia masafa ya mawasiliano.”

Kuonyesha juhudi ilizochukua kabla ya uamuzi huo, TCRA imesema Januari 27, 2016 ilitoa amri ya utekelezaji kwa kampuni hiyo kwa kukiuka masharti ya leseni walizopewa na kushindwa kutoa huduma kinyume cha Kifungu 21 (a) na (b) cha Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (Epoca) ya mwaka 2010.

Hata hivyo, Mycell haimo kwenye orodha ya kampuni zilizopewa leseni na TCRA ambazo zimo kwenye tovuti ya mamlaka hiyo.

Mamlaka hiyo imeeleza kwenye taarifa yake ya kusudio la kuifuta Mycell kuwa iliipa kampuni hiyo leseni nne tofauti Novemba 21, 2008.

Inafafanua kuwa leseni hizo ni ya kujenga miundombinu kitaifa, kutoa huduma kupitia miundombinu hiyo, kutoa huduma kupitia mtandao wa mawasiliano na kutumia masafa ya mawasiliano.

Kwenye ujumbe wake alioutoa Oktoba, 2011 wakati Quality Group ikitimiza miaka 35 tangu ianzishwe nchini, mwenyekiti wake wakati huo, Yusuf Manji alitabainisha vipaumbele vya utekelezaji walivyonavyo.

“Mycell inatekeleza mpango biashara unaoiruhusu kukodisha masafa iliyopewa na TCRA kwa kampuni ya nje yenye uwezo na uzoefu mkubwa. Inatarajia kujenga miundombinu imara itakayofanikisha miradi mbalimbali,” alisema Manji.

Alisema mpango huo unatokana na fursa kemkem zilizopo kwenye sekta ya mawasiliano nchini hasa kwa kuzingatia njia za kawaida za kufikishiana ujumbe ambazo zimekuwa hazikidhi mahitaji yaliyopo kutokana na kukua kwa kasi kwa teknolojia hasa ya habari na mawasiliano (Tehama).

“Sekta hii ina fursa nyingi kwa kampuni zenye teknolojia ya kisasa kuwekeza na kukua. QGL inaona kwamba kuna haja ya kuwekeza kwenye miundombinu na kuziruhusu kampuni za mawasiliano kuongeza ufanisi. Gharama za kupiga simu na data zipo juu nchini ikilinganishwa na ilivyo kwa nchi za Asia zinazonufaika na Tehama kwa kiasi kikubwa,” alisema Manji kwenye ujumbe wake wa mwaka 2011.

Mwaka 1997, Manji alianza kuiongoza QGL akihudumu kama ofisa mtendaji mkuu kabla ya baadaye kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa kundi hilo, nafasi aliyojiuzulu lakini baadaye akarejea tena na kuendelea kuiongoza

Chanzo: Mwananchi

Sent using Jamii Forums mobile app
Serikali haipaswi kuwabughuuzi wawekezaji badala yake iwaonyeshe nini cha kufanya. Tanzania ilikuwa na ungozi halali hivyo mambo yote yalifanyika kwa mujibu wa serikali ilizopita
 
Hawa matajiri wanayataka wenyewe, kukimbilia kwenye siasa badala ya kukaa wajifanyie biashara zao, yote hii ni tamaa tu.
 
Hawa matajiri wanayataka wenyewe, kukimbilia kwenye siasa badala ya kukaa wajifanyie biashara zao, yote hii ni tamaa tu.
Na pia wanatakiwa wachunge midomo yao wanapojibizana na politicians.... kujifanya " Hujibizani na mbwa unaongea na mfuga mbwa " ....mbwa kumbe baadae nae anakuwa mfuga mbwa kazi kweli kweli [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Kina Bill Gates wangefanyiwa hivi na serikali zao hii misaada wanayotupa tungeipata wapi?

Watakaopoteza ajira wakale wapi?

Anyway,madaraka yana mwisho.
Cha kujiuliza, hivi Bill Gates angekuwa alifanya ufisadi anaofanya huyu mwenzetu angekuwa wapi!!
 
Selective Justice is not justice. It can be an instrument of oppression.

Manji deeds may be illegal. But how many are in the same boat? Why only pick on Manji alone?

The same applies to Sumaye's farms. There are bigger farms compared to those of Sumaye yet nothing is happening.
 
Back
Top Bottom