Serikali kuhamia Dodoma:Sioni uwezekano wa matawi machace ya mabenki kumudu ongezeke la wateja

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,028
144,382
Moja ya changamoto ambayo kwa mtazamo wangu naona itageuka kero kubwa kwa watumiaji wa mabenki hapa mjini Dodoma endapo wizara nyingi kama sio zote zitahamia hapa Dodoma kabla ya hiyo September,ni kuzidiwa kwa matawi machache sana ya mabenki yaliyopo katika mjii huu wa Dodoma katika kuhudumia wateja ambao wanaweza kuongezeka kwa wingi ndani ya muda mfupi huku mabenki haya yakiwa hayajajiandaa.

Kwa mfano,benki za NMB na CRDB ambazo ndio hutumiwa na watumishi wengi wa umma kila moja ina matawi mawili tu hapa katikati ya mji huku mashine za ATM nazo zikiwa ni za kuhesabu kwa kila benki ukiacha zile chache zilizoko ndani ya viwanja vya Bunge.

NMB hapa Dodoma mjini wana matawi 2 tu moja likiwa ni tawi la Dodoma na tawi lingine likijulikana kwa jina la Mazengo.

Tawi la kubwa la Dodoma lina machine za ATM kama sita hivi na tawi la Mazengo likiwa na ATM machine 3 tu.Ukiacha hizo ATM kwenya majengo ya benki,kuna ATM zingine kama 4 au 5 kwenye sheli moja iliyo jirani na stendi ya dala dala hapa mjini.

Kwa upande wa CRDB,wao katika tawi kubwa la Dodoma wana ATM machine kama 4 au 5 tu na tawi dogo la Chamwino wana ATM machine 2 tu.Ukiacha mashine za ATM zilizoko katika matawi haya mawili,sidhani kama kuna mahala pengine popote katikati ya huu mji CRDB wameweka mashine hizi ukiacha ile moja iliyoko St.Johns University kwa ajili ya kuuhudumia wanafunzi ambayo nayo imo ndani ya chuo.

Benki ya NBC hapa town center nayo ndio kabisa bora hata hizo zingine kwani kwa hapa mjini kuna tawi moja tu kubwa la Dodoma lenye mashine za ATM kama 3 au 4 tu.Hawa nao wana ATM mashine moja katika chuo kikuu cha St.John's na nyingine iliyo katika sheli moja iliyoko opposite na stand ya daladala hapa Dodoma mjini.

Benki ya Posta kwa hapa mjini nimewahi ona tawi moja tu lenye mashine moja tu ya ATM na sijui kama wana tawi lingene au ATM mashine nyingine zaidi ya hiyo kwa hapa Dodoma mjini.

Chuo cha UDOM ambacho kiko nje kidogo ya mji nako ndio kuna mashine za ATM za mabenki haya ingawa sina uhakika kama kika benki ina mashine zake ndani ya chuo hiki.

Kama kuna mashine za ATM na matawi mengine zaidi ya haya niliyoyataja yako hapa mjini,basi mwenye kujua yalipo atueleze yako wapi maana mji wenyewe huu ni mdogo sana na ukitoka kidogo nje ya mji sidhani kama kuna matwai mengine zaidi ya yale matawi yaliyoko katika wilaya zingine za mkoa huu na labda maeneo ya mbali na hapa mjini

Ukweli ni kwamba,inapofika mwisho wa mwezi kunakuwa na foleni kiubwa sana katika mashine hizi chache za ATM zilizopo hapa mjini na hata ndani pia huwa kunajaa sana hata kwa siku za kawaida bila kusahau nyakati ambazo vyuo hapa Dodoma hufunguliwa na hivyo wanafunzi wengi kufanya malipo ya ada na mambo mengineyo na hivyo kuongeza foleni ndani ya mabenki haya.

Sasa nachojiuliza kama wizara zote zitamfuta Waziri Mkuu hapa Dodoma ndani ya muda huu mfupi huku wizara moja tu ya Kilimo na uvuvi ikitajwa kuwa na watumish takribani 2000,hali itakuwaje katika mabenki haya siku za mwisho wa mwezi na hata kwa siku za kawaida tu?

Pia tutarajie ongezeko kubwa la watu ndani ya mabenki haya ambao watajitokeza kwa madhumuni ya kutuma au muweka fedha kwenye akaunti za ndugu na jamaa zao waliowaacha Dar-es-salaam,walioko mikoa mingine na hata kutuma na kuchukua pesa kutoka kwa washirika wao wa kibiashara maana hata watumishi nao hujihusisha na biashara ili kuongeza kipato.

Mimi hapa kwa haraharaka naona kuna uwezekano mkubwa sana wa kuongezeka kwa huduma za mobile banking na watu kwenda kwenye ATM nyakati za usiku kukwepa foleni ndefu nyakati za mchana na jioni.

Hata hivyo,kama itafikia hatua watu wakaamua kutumuia huduma ya mobile banking kuhamisha fedha kutoka kwenye account zao za bank na kuzihamishi katika akaunti zao za Mpesa,tigopesa,Airtel money,n.k, ili kuepuka foleni katika mabenki na kwenye mashine za ATM, basi serikali ndio itakayofaidika kwani itaongeza mapato kupitia tozo ya VAT kwenye miamala hii pale tozo hii itakapokuwa imeanza rasimi unless mabenki haya yafanye juhudi za ziada za kuongeza matawi na mashine za kutolea fedha(ATM).

Huu ni mtazamo wangu tu kulingana na hali ninavyoiona hapa mjini Dodoma.
 
Moja ya changamoto ambayo kwa mtazamo wangu naona itageuka kero kubwa kwa watumiaji wa mabenki hapa mjini Dodoma endapo wizara nyingi kama sio zote zitahamia hapa Dodoma kabla ya hiyo September,ni kuzidiwa kwa matawi machache sana ya mabenki yaliyopo katika mjii huu wa Dodoma katika kuhudumia wateja ambao wanaweza kuongezeka kwa wingi ndani ya muda mfupi huku mabenki haya yakiwa hayajajiandaa.

Kwa mfano,benki za NMB na CRDB ambazo ndio hutumiwa na watumishi wengi wa umma kila moja ina matawi mawili tu hapa katikati ya mji huku machine za ATM nazo zikiwa ni za kuhesabu kwa kila benki ukiacha zile chache zilizoko ndani ya viwanja vya Bunge.

NMB hapa Dodoma mjini wana matawi 2 tu moja likiwa ni tawi la Dodoma na tawi lingine likijulikana kwa jina la Mazengo.

Tawi la kubwa la Dodoma lina machine za ATM kama sita hivi na tawi la Mazengo likiwa na ATM machine 3 tu.Ukiacha hizo ATM kwenya majengo ya benki,kuna ATM zingine kama 4 au 5 kwenye sheli moja iliyo jirani na stendi ya dala dala hapa mjini.

Kwa upande wa CRDB,wao katika tawi kubwa la Dodoma wana ATM machine kama 4 au 5 tu na tawi dogo la Chamwino wana ATM machine 2 tu.Ukiacha mashine za ATM zilizoko katika matawi haya mawili,sidhani kama kuna mahala pengine popote katikati ya huu mji CRDB wameweka mashine hizi ukiacha ile moja iliyoko St.Johns University kwa ajili ya kuuhudumia wanafunzi ambayo nayo imo ndani ya chuo.

Benki ya NBC hapa town center nayo ndio kabisa bora hata hizo zingine kwani kwa hapa mjini kuna tawi moja tu kubwa la Dodoma lenye mashine za ATM kama 3 au 4 tu.Hawa nao wana ATM mashine moja katika chuo kikuu cha St.John's na nyingine iliyo katika sheli moja iliyoko opposite na standa ya daladala hapa Dodoma mjini.

Benki ya Posta kwa hapa mjini nimewahi ona tawi moja tu lenye mashine moja tu ya ATM na sijui kama wana tawi lingene au ATM mashine nyingine zaidi ya hiyo kwa hapa Dodoma mjini.

Chuo cha UDOM ambacho kiko nje kidogo ya mji nako ndio kuna mashine za ATM za mabenki haya ingawa sina uhakika kama kika benki ina mashine zake ndani ya chuo hiki.

Kama kuna mashine za ATM na matawi mengine zaidi ya haya niliyoyataja yako hapa mjini,basi mwenye kujua yalipo atueleze yako wapi maana mji wenyewe huu ni mdogo sana na ukitoka kidogo nje ya mji sidhani kama kuna matwai mengine zaidi ya yale matawi yaliyoko katika wilaya zingine za mkoa huu na labda maeneo ya mbali na hapa mjini

Ukweli ni kwamba,inapofika mwisho wa mwezi kunakuwa na foleni kiubwa sana katika mashine hizi chache za ATM zilizopo hapa mjini na hata ndani pia huwa kunajaa sana hata kwa siku za kawaida bila kusahau nyakati ambazo vyuo hapa Dodoma hufunguliwa na hivyo wanafunzi wengi kufanya malipo ya ada na mambo mengineyo na hivyo kuongeza foleni ndani ya mabenki haya.

Sasa nachojiuliza kama wizara zote zitamfuta Waziri Mkuu hapa Dodoma ndani ya muda huu mfupi huku wizara moja tu ya Kilimo na uvuvi ikitajwa kuwa na watumish takribani 2000,hali itakuwaje katika mabenki haya siku za mwisho wa mwezi na hata kwa siku za kawaida tu?

Pia tutarajie ongezeko kubwa la watu ndani ya mabenki haya ambao watajitokeza kwa madhumuni ya kutuma au muweka fedha kwenye akaunti za ndugu na jamaa zao waliowaacha Dar-es-salaam,walioko mikoa mingine na hata kutuma na kuchukua pesa kutoka kwa washirika wao wa kibiashara maana hata watumishi nao hujihusisha na biashara ili kuongeza kipato.

Mimi hapa kwa haraharaka naona kuna uwezekano mkubwa sana wa kuongezeka kwa huduma za mobile banking na watu kwenda kwenye ATM nyakati za usiku kukwepa foleni ndefu nyakati za mchana na jioni.

Hata hivyo,kama itafikia hatua watu wakaamua kutumuia huduma ya mobile banking kuhamisha fedha kutoka kwenye account zao za bank na kuzihamishi katika akaunti zao za Mpesa,tigopesa,Airtel money,n.k, ili kuepuka foleni katika mabenki na kwenye mashine za ATM, basi serikali ndio itakayofaidika kwani itaongeza mapato kupitia tozo ya VAT kwenye miamala hii pale tozo hii itakapokuwa imeanza rasimi unless mabenki haya yafanye juhudi za ziada za kuongeza matawi na mashine za kutolea fedha(ATM).

Huu ni mtazamo wangu tu kulingana na hali ninavyoiona hapa mjini Dodoma.
Mkuu hizo kweli ni mojawapo ya changamoto za kuhamia Dodoma nadhani wamiliki wa bank zote wanaelekea Dodoma , kutakuwa na Bank za Kila Aina mpaka za kimataifa , Wamili wengi wa mabank jicho Lao Lipo Dodoma
 
Dodoma Kwa sasa imejaa wale Ndugu zetu toka Moshi na njombe Kwa maana wakinga na wachaga wapo busy wanakamata maeneo viwanja na kununua nyumba ili baadae wauze
 
Mkuu hizo kweli ni mojawapo ya changamoto za kuhamia Dodoma nadhani wamiliki wa bank zote wanaelekea Dodoma , kutakuwa na Bank za Kila Aina mpaka za kimataifa , BE FORWARD : 2002 SUBARU Legacy B4
Yaani hapa Dodoma itabidi wajiandae kuhamisha watu na kuwalipa fidia ndio wapate sehemu za kujenga maana viwanja kwa sasa vinapatikana nje kabisa ya mji na huwezi kwenda kufungua tawi sehemu ambayo hakuna makazi au kuna wakazi wachache hata kama ujenzi wa nyumba na majumba ndio utakuwa uko katika hatua za awali.
 
Back
Top Bottom