Serikali kila wanamtaa/kijiji kuchanga Tsh. 150,000 kununua kibao cha jina la mtaa/kijiji chao

Kama kweli kuna shida
Halmashauri pesa zote za Mapato ya ndani na hela wanapewa na Serikali kuu kazi yake nini?

Pili Mabilioni ya Pesa yalitolewa na mama Samia kwa ajili ya huo mradi Tanzania bara na Zanzibar hilo la vibao halimo?
 
Dodoma. Rais Samia Suluhu Hassan amewaonya wakuu wa mikoa kutotumia fedha za kugharamia mradi wa anwani za posta na makazi kwa ajili ya matumizi ya mengineyo (OC).
Pia, Mkuu huyo wa nchi amesema kuwa awali mradi huo ulipangwa kutumia Sh720 bilioni lakini gharama hizo zimepunguzwa hadi kufikia Sh28 bilioni.
Rais Samia amesema hayo leo Jumanne Februari 8, 2022 wakati akizungumza katika kikao kazi cha wakuu wa mikoa jijini hapa.
“Fedha tutaleta kwa ukubwa wa mikoa yenu pande zote (Tanzania Bara na Zanzibar), fedha hizi sio OC (matumizi mengineyo) ni ya mradi. Mtaendelea kutumia OC zenu, fedha iende katika miradi,”amesema.
Amesema halmashauri zinatakiwa kuchangia fedha katika utekelezaji wa mradi huo.
Ameshauri utekelezaji wa mradi huo kutumia nyenzo zilizopo katika kuukamilisha ili kufanikisha shughuli ya sensa ya watu na makazi ambayo itafanyika Agosti mwaka huu.
Rais Samia pia awaagiza viongozi kuwashirikisha watanzania kwa kuwafundisha kuhusu umuhimu wa mradi huo wa anwani za posta na makazi ili waweze kuwa na uelewa na kushiriki ipasavyo.
Amesema mradi huo utafanyika kwa utaratibu wa operesheni maalum kama ilivyofanyika katika ujenzi wa madarasa yaliyotokana na fedha za Uviko-19.
Amesema mradi huo unatakiwa kukamilika itakapofika Mei mwaka huu.
“Kama hamkumaliza zoezi au halikwenda vizuri tutakaa ana kwa ana, ukiwa na changamoto zake tuzungumze ukikaa nazo hadi muda ukamalizika itabidi tukae ana kwa ana tuelezane,”amesema.

Source: Mwanamchi

Mytake:Hivyo vibao haiko.kwenye hizo bilioni 692? Ina maana gani kuwa na mradi ambao vibao haviko kwenye bajeti huo utapeli
 
Kwa hiyo BAO LA MKONO anataka gharama ya mafuta ya kuzunguka Tanzania nzima na Chopa zilipwe na kila mtaa?

Kale ka-kibao ka chuma kakujulisha kwamba huu ni mtaa wa Kikolobinywo ndio 150,000/-?

Tumepigwa na tunaendelea kupigwa.
 
Back
Top Bottom