Serikali Kufungua Shamba la Miwa na Kiwanda Kikubwa cha Sukari Wilaya ya Songea Kijiji cha Muhukuru

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
944

WAZIRI MHAGAMA - SERIKALI KUFUNGUA SHAMBA LA MIWA, MUHUKURU

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika na Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama (MB) wa Peramiho amesema Serikali kupitia Halmashauri ya wilaya ya Songea imedhamiria kufungua shamba kubwa la miwa na kiwanda cha kuzalisha sukari katika kijiji cha Muhukuru.

Kauli hiyo imetolewa Mkoani Ruvuma katika Kijiji cha Lupokela leo tarehe 30/09/2023 katika Maadhimisho ya siku ya Kahawa yaliyoandaliwa na Kampuni ya Aviv Wawekezaji wa mashamba ya Kahawa katika Halmashauri ya wilaya ya Songea.

“tunaamini tukifungua shamba jingine Muhukuru tunaweza kuzalisha ajira nyingine nyingi na kuongeza mapato ya Halmashauri na pato kwa wananchi.” Alisisitiza

Wawekezaji kampuni ya Aviv wanazalisha 4.5% ya kahawa yote inayozalishwa nchini ambayo inauzwa nje ya nchini, na wanasaidia Nchi kupata fedha za kigeni, ambazo zinawezesha serikali kujenga miradi ya maendeleo kwa wananchi.

Aidha Serikali ya Awamu ya Sita inayongozwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan, imeendelea kuweka Mkazo katika kufungua kilimo ili kusaidia kuchochea uchumi na kutoa ajira ili kuhakikisha kilimo kinakuwa na faida katika kufungua uchumi wa mwananchi mmoja mmoja.

“Wananchi ni mashuhuda wa uwekezaji Uliofanywa na kampuni ya Aviv katika kilimo cha kahawa; ulivyowezesha kufanya mabadiliko ya kijamii, uchumi na mabadiliko ya mwenendo wa maisha ya wananchi katika vijiji vinavyozunguka mradi,” alifafanua.

Ameongeza kusema Muwekezaj kampuni ya Aviv anashiriki katika ujenzi wa miradi mingi katika vijiji vinavyozunguka mradi kama utaratibu wa serikali unavyoelekeza kwa Wawekezaji, kwamba washirikiane na Wananchi katika kurudisha mchango wa kile walichokivuna kama faida. Amewaomba wananchi kutobweteka na badala yake kuendelea kujitoa katika ujenzi wa miradi ya maendeleo.

Kwa upande wake Meneja wa Shamba la kampuni ya Aviv Tanzania Bw, Hamza Kassim amesema siku ya leo tunadhimisha siku ya kahawa duniani, maadhimisho ambayo yanayofanyika kila tarehe 01 ya mwezi wa 10, kila mwaka.

Ameongeza kusema, kampuni ya Aviv wamefanikiwa kuwa na uzalishaji endelevu kwa sababu ya kujenga miundombinu ya Umwagiliaji.
WhatsApp Image 2023-10-01 at 14.55.37.jpeg
WhatsApp Image 2023-10-01 at 14.55.35.jpeg
WhatsApp Image 2023-10-01 at 14.55.37(2).jpeg
 
Wametenga eka ngapi za kulima miwa hapo kijijini??
 
Back
Top Bottom