Serikali iwasaidie wakulima wa mihogo wa Wilaya ya Handeni

Koryo2

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
2,056
2,515
Jioni hii kupitia taarifa ya habari nimeshuhudia taarifa ya kuhuzunisha sana jinsi wakulima wa mihogo kutoka Wilaya ya Handeni walivyopata hasara ya kuharibikiwa kwa tano 200 za mihogo.

Wakulima hawa waliingia mkataba na Kampuni moja ya Dar es Salaam kununua mihogo yao yote watakayolima lakini kinyume na makubaliano hayo kampuni hiyo haikutimiza ahadi yake.

Serikali ipo kuona wananchi wanalindwa na kuwezeshwa. Mhe. Bashe tunakuamini kwa msimamo wako wa kuwatetea wakulima.

Tunakuomba uchukue hatua stahiki ili wakulima hawa wapate haki yao.
 
Wasage udaga wapeleke uganda mbona soko lipo la kutosha.
Shida sidhani kama ni soko, ila gharama za usafirishaji, namna ya kupata masoko hivyo vyote vinahitaji muda na pesa, jambo ambalo wakulima wengi hawawezi fanya.
 
Godwin Gondwe anasemaje? Maana yeye ndiye aliwahamasisha wananchi enzi hizo akiwa DC wa huko.
 
Biashara ya mihogo hivi sasa ni ngumu sana. Siku hizi kuna mihogo-kisasa, inalimwa popote pale, haichagui hali ya hewa. Hivyo kwenye msimu wa mihogo huwa ni mingi mnoo!!

Wengi wanaicha inakomalia shambani! Kilimo cha mihogo wala hakihitaji mbolea!
 
Mbona tulielezwa kuwa kuna soko la uhakika China kulikoni?.
 
Back
Top Bottom