kakuruvi
JF-Expert Member
- Sep 2, 2009
- 770
- 256
Habari Wana JF,
Juzi kwenye hotuba ya bajeti ya Serikali iliyosomwa na Waziri wa fedha, Waziri alitamka kufahamu kwamba kufuatia kutokuwepo kwa ajira za moja kwa moja kwa Wahitimu, Wazazi wamekua wakibeba mzigo mkubwa wa familia zao.
Kwa kulitambua hili naomba Serikali kuwezesha upatikanaji rahisi wa mafao ya Wastaafu ili waweze kuendelea kufurahia maisha yao baada ya kulitumikia Taifa, pamoja na kuendelea kuhudumia familia zao japo kwa mitaji midogo kwa Watoto wao Wahitimu ili wasiwategemee moja kwa moja.
Ili hili liwe rahisi kiinua mgongo cha Wabunge pia kicheleweshwe kama wanavyofanyiwa Wastaafu, Wabunge wakipata machungu wanayoyapata Wastaafu kwa sababu wao ndio wanaotunga hizi Sheria, watabadilisha ili mambo yaende sawa.
Nawasilisha!