DOKEZO Serikali itusaidie kumaliza tatizo la vibaka Ipuli, Tabora imekuwa too much sasa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

BigTall

JF-Expert Member
Mar 9, 2022
422
1,049
Kumekuwa na sintofahamu ya matukio ya wizi uliokithiri maeneo ya Ipuli hapa mtaani Mrenda Mkoani Tabora, matukio ambayo yanayofanywa na watu ambao bila shaka ni vibaka kulingana na aina ya wizi wanaofanya.

Tabia hiyo ilianza mdogomdogo lakini sasa inazidi kukomaa, vibaka wanakata madirisha ya vioo na kutindua nondo kisha huingia ndani na kuiba.

Wakati mwingine huvunja milango na kuingia ndani na kufanya uhalifu, ajabu zaidi mara nyingi wizi huu hufanyika mchana.

Mfano hapa jirani kuna mama mmoja mstaafu ni kama amesaini mkataba na vibaka wa kuwa wawe wanamuibia kila mara, kwani ni zaidi ya mara 10 ameibiwa na vibaka ndani ya kipindi cha miezi mitatu iliyopita.
photo_2023-06-29_12-11-00.jpg

Uharibifu uliofanywa na vibaka
photo_2023-06-28_21-34-24.jpg
Mara nyingi vibaka wanavizia wenyeji wakiwa wametokea, ni wazi wanajua ratiba nzima ya watu wanaoenda kuwaibia.

Bi mkuwa mkubwa huyo jirani niliyemtolea mfano hapo juu ameshatoa taarifa katika Kituo cha Polisi kuhusu uhalifu anaotendewa yeye na watu wengine kadhaa wa mtaani lakini mara zote wamekuwa wakiambiwa Polisi wanafanya uchunguzi bila matokeo chanya yoyote na uhalifu unaendelea.

Baadhi ya vitu ambavyo vibaka hao wamekuwa waki-target ni simu za smart ambazo Polisi mara kadhaa wamekuwa wakiomba IMEI namba za simu zilizoibiwa ili wazifuatilie lakini nako ni bilabila.

Kuna wakati Polisi walikusanya vibaka wanaodhaniwa kuwa ni wezi wa mtaa huo ila baada ya siku mbili wakaanza kuwaachia bila maelezo, kisha uhalifu ukaendelea kama kawaida.

Kifupi mama huyu anayeishi peke yake yupo katika wakati mgumu kwa kuwa hata akienda sokoni huku nyuma wanamuibia.

Tunalalamika sana lakini mamlaka za Ulinzi ni kama zinaona fresha tu, sasa naanza kuwaelewa wale wanaoamua kujichukulia hatua mkononi dhidi ya wahalifu.
photo_2023-06-29_12-11-08.jpg
 
Isevya ,ng'ambo,kiloleni,tambuka reli,na kiyungi hatari sana haya maeneo
 
Katika sehemu zenye vibaka Duniani nadhani Tabora inakimbizana na Kolombia,ni mkoa hatari kwa kuishi
 
Kumekuwa na sintofahamu ya matukio ya wizi uliokithiri maeneo ya Ipuli hapa mtaani Mrenda Mkoani Tabora, matukio ambayo yanayofanywa na watu ambao bila shaka ni vibaka kulingana na aina ya wizi wanaofanya.

Tabia hiyo ilianza mdogomdogo lakini sasa inazidi kukomaa, vibaka wanakata madirisha ya vioo na kutindua nondo kisha huingia ndani na kuiba.

Wakati mwingine huvunja milango na kuingia ndani na kufanya uhalifu, ajabu zaidi mara nyingi wizi huu hufanyika mchana.

Mfano hapa jirani kuna mama mmoja mstaafu ni kama amesaini mkataba na vibaka wa kuwa wawe wanamuibia kila mara, kwani ni zaidi ya mara 10 ameibiwa na vibaka ndani ya kipindi cha miezi mitatu iliyopita.
View attachment 2672830
Uharibifu uliofanywa na vibaka
View attachment 2672831
Mara nyingi vibaka wanavizia wenyeji wakiwa wametokea, ni wazi wanajua ratiba nzima ya watu wanaoenda kuwaibia.

Bi mkuwa mkubwa huyo jirani niliyemtolea mfano hapo juu ameshatoa taarifa katika Kituo cha Polisi kuhusu uhalifu anaotendewa yeye na watu wengine kadhaa wa mtaani lakini mara zote wamekuwa wakiambiwa Polisi wanafanya uchunguzi bila matokeo chanya yoyote na uhalifu unaendelea.

Baadhi ya vitu ambavyo vibaka hao wamekuwa waki-target ni simu za smart ambazo Polisi mara kadhaa wamekuwa wakiomba IMEI namba za simu zilizoibiwa ili wazifuatilie lakini nako ni bilabila.

Kuna wakati Polisi walikusanya vibaka wanaodhaniwa kuwa ni wezi wa mtaa huo ila baada ya siku mbili wakaanza kuwaachia bila maelezo, kisha uhalifu ukaendelea kama kawaida.

Kifupi mama huyu anayeishi peke yake yupo katika wakati mgumu kwa kuwa hata akienda sokoni huku nyuma wanamuibia.

Tunalalamika sana lakini mamlaka za Ulinzi ni kama zinaona fresha tu, sasa naanza kuwaelewa wale wanaoamua kujichukulia hatua mkononi dhidi ya wahalifu.
Oyaa mzee baba Poker malizia ile stor yako basi

Inawezekana hao vibaka wa tabora unawajua
 
Toa mfano,tegesha umeme katika hayo madirisha kila uingiapo usiku,afrajiri unaondoa, wakinasa vibaka 2 uoga utawaingia.
 
Back
Top Bottom