Serikali itueleze ukweli inapata wapi pesa za kununua ndege

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,502
51,098
Katika vitu ambavyo serikali yetu imeonyesha determination, ni suala la kununua ndege. Katika suala hili, serikali imeweka pamba masikioni na kuignore kila sauti inayohoji suala hili la kununua ndege. Mimi binafsi ninajiuliza na kujihoji maswali yafuatayo kuhusiana na suala la ndege. JE SERIKALI HII INAPATA WAPI FEDHA ZA KUNUNUA NDEGE?

Katika nchi ambayo hata ujenzi wa stendi za mabasi tunafikiria kuomba mkopo, Nchi ambayo hata madawati yamekuwa shida kiasi kwamba katika shule nyingine mwanafunzi akianza kidato cha kwanza anaambiwa aende na dawati lake mwenyewe, hivi inaingia akilini kuwa Serikali ina Mihela mingi lakini haiwezi kufanya vitu hivyo?

Mimi nina wasiwasi kuwa lazima kuna kitu serikali hii imefanya ili kuraise fund kwa ajili ya kununua hizi ndege

1. Nina wasiwawasi na madini yetu huenda yameshakabidhiwa kwa mabeberu in exchange ya ndege

Tusidanganyane bwana, serikali hii haina pesa za kutoa cash kununua ndege kila kukicha, Je haiwezekani madini yetu yanabadirishana juu kwa juu na hizi ndege?

Haiwezekani kwamba kuna watu kwenye black market wanauza madini yetu na fedha kutakatishwa kwa hizi ndege?

Ninahofu na hilo kwa sababu mabeberu ni rahisi kukusaidia kwenye dili kama hizi kwa sababu wanapata fursa ya kupata madini lskini at the same time wanapata fursa ya kuuza ndege zao. Laiti kama ukitaka kutumia fedha hizo kujenga shule, maji, vyuo n. k, mabeberu hawakupi ushirikiano!

2. Je, miti milioni 2.6 tuliyouza baada ya kukata mapori kule Selous ili kujenga bwawa la Stieglers ndiyo inayotupa hizi hela za kununua ndege?

Thamani ya ile miti ni matrilion ya fedha, hatujawahi kuelezwa hizo pesa ziko wapi na zinafanya nini, Je ndiyo hizo tunazonunulia hizi ndege?

3. Je, kuna mikopo tusiyoifahamu?
Katika vitu ambavyo viligubikwa na usiri mkubwa ni. mikopo katika mabenki ya kibiashara tuliyochukua enzi za mwendazake. Je kuna mikopo mingine tumechukua ili kununua hizi ndege?

Haya ni maswali ya msingi inabidi tujue, maana kwa kawaida ni ajabu sana kuona serikali imekomaa kwa nguvu zote na mradi huu wa ndege licha ya vikwazo vingi ikiwemo hasara zinazoripotiwa kila mara na CAG kuhusu shirika la ATCL.

Je, serikali ina dili za siri na mikataba ya siri na mabeberu juu ya mradi huu wa ndege kupitia funds za gizani?

Wananchi tunahitaji kujua ili tusije kustukia tumeshauzwa!

Tusidanganyane serikali hii haina hela ya kununua ndege hizi kwa pesa za kawaidakawaida, Je inapata wapi matrilion ya kununua hizi ndege?
 
Umetaja jambo moja linaloshangaza..... ujenzi wa stand za mabasi ambazo nyingi ni white elephant, nenda Tanga Kange, Iringa, Stendi Kuu ya Dodoma zote hizi ni underutilised kwa asilimia kubwa.

Pia kuna wimbi la ujenzi wa masoko ya ghorofa ambayo nayo ni underutilised kwa asilimia kubwa, nenda soko La ndugai Dodoma, Magomeni, uone jinsi fedha zilivyoteketezwa bila huruma
 
Katika vitu ambavyo serikali yetu imeonyesha determination, ni suala la kununua ndege. Katika suala hili, serikali imeweka pamba masikioni na kuignore kila sauti inayohoji suala hili la kununua ndege...
Tunatumia mikopo tusiyoifahamu, wewe tazama deni la taifa linavyopaa ndio utajua pesa za kununua ndege zinazokuja kupaki viwanjani zinatoka wapi.
 
Hii nchi niya ajabu sana vipaumbele muhimu sio muhimu visivyo muhimu ni muhimu huduma za msingi Kama maji,elimu,afya,umeme nk viongozi wakiambiwa changamoto zake hukimbilia kusema hakuna pesa wakati huo huo Kuna matumizi makubwa ya pesa ya mtanzania mvuja jasho kwenye misafara ya viongozi wa nchi
 
Matumizi ya neno “Mabeberu” huwa linaketa ukakasi kwa kiasi fulani..
 
Au ndiyo yale madini tunayoambiwa Jiwe alikuwa anapiga dili na Mr Slim(PK), tunalipwa kwa njia ya kupewa ndege?

Tuambiwe ukweli!
 
Umetaja jambo moja linaloshangaza..... ujenzi wa stand za mabasi ambazo nyingi ni white elephant, nenda Tanga Kange, Iringa, Stendi Kuu ya Dodoma zote hizi ni underutilised kwa asilimia kubwa...
Hii ya ujenzi wa majengo yasiyotumika ni changamoto kubwa sana. Nashindwa kuelewa nani anayefanya marketing research ya baadhi ya hizi investment.
 
Back
Top Bottom