SoC03 Serikali iteketeze kichaka hiki cha rushwa barabarani

Stories of Change - 2023 Competition

cilla

JF-Expert Member
Jul 15, 2011
369
296

SERIKALI ITEKETEZE KICHAKA HIKI CHA RUSHWA BARABARANI

UTANGULIZI.
Maana ya rushwa; Rushwa maana yake ni matumizi mabaya ya mamlaka au nafasi fulani iliyo rasmi kwa lengo lakujipatia faida binafsi kinyume na sheria na kanuni ya maadili ya nchi.Pia tunaweza kusema rushwa ni fedha au kitu au nafasi inayotolewa kwa mtu mwenye madaraka fulani ili mtoaji apatiwe upendeleo fulani.Rushwa inaweza ikawa ya ngono, ya fedha, nafasi fulani au ahadi fulani.

Kwa mujibu wa sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa ya mwaka 2007 imeainisha makosa 14 ya rushwa katika taswira tofauti tofauti.Lakini Moja ya makosa ya rushwa yaliyoainishwa katika sheria ni kupokea rushwa,kushawishi au kulazimisha kupewa rushwa, kutoa au kuahidi kutoa rushwa.(sheria ya kupambana na rushwa Na 11/2007).

HALI YA RUSHWA KATIKA JESHI LA POLISI USALAMA BARABARANI(TRAFFIC)
Jeshi la Polisi ni moja kati taasisi za serikali zinazolalamikiwa na wananchi wengi kwamba inahusika sana na upokeaji wa rushwa na hasa Jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani. Pamekuwa na taarifa mbalimbali kwenye vyombo vya habari dhidi ya askari usalama barabarani wasiowaaminifu wanaojihusisha na rushwa.Rushwa barabarani imekuwa ni rushwa inayolalamikiwa sana na madereva na wasio madereva kwasababu ni moja ya rushwa ambazo zimekuwa zikifanyika waziwazi barabarani.

Tafiti mbalimbali zinasadikisha na kuthibitisha ukweli kwamba rushwa imeshamiri kwenye jeshi letu la polisi hasa kwa Askari wa usalama barabarani. Mfano:-

👉Katika utafiti wa mwaka 2009,ambao ulikuwa ukiangazia rushwa katika taasisi mbalimbali, jeshi la polisi lilibainika kuongoza kwa vitendo vya rushwa kwa asilimia 63 kwa ujumla, huku jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani likiongoza kwa asilimia 66,ikifuatiwa na mahakama asilimia 58.1 na ofisi za ardhi ikiwa ni asilimia 41.4.

👉Katika utafiti wa Twaweza uliokuwa na jina Sauti ya wananchi wa mwaka 2017 unaonyesha kuwa jeshi la polisi ni sekta iliyokuwa inaongoza kwa rushwa kwa asilimia 60. Na utafiti wa mwaka 2014 ulionyesha Watanzania 60% (waliokutana na polisi) wameshawahi kuombwa rushwa na polisi, na 43% wamewahi kutoa rushwa.

👉Katika utafiti uliofanywa na kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC) kwa mwaka 2011, ilieleza kuwa jeshi la polisi linaongoza kwa rushwa hasa kitengo cha polisi wa usalama barabarani.

👉Takwimu zilizotolewa na TAKUKURU Mwaka 2023 imeitaja jeshi la polisi kama sekta inayoongoza kwa rushwa zaidi kwa asilimia 45.6 na kufuatiwa na sekta ya afya.

Takwimu hizi zinatushawishi sisi kama wananchi kutafakari na kutafuta njia ya kupunguza au kukomesha kabisa rushwa.

MOJA YA KICHAKA CHA RUSHWA BARABARANI

Kuna utaratibu ambao Jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani wanautumia kama kichaka ambacho ni moja ya maficho yao katika kuomba na kushawishi rushwa .

Kichaka kimoja wapo cha rushwa barabarani ni utaratibu uliotengenezwa na Askari wa usalama barabarani wa kukwepa kuzungumza na madereva wakiwa ndani ya gari mbele ya abiria au wasafiri wengine.Na kwa makusudi madereva nao hupaki gari mbali ili anaposhuka ili kuzungumza na askari aliyemsimamisha watu wengine wasijue,wasione, na wasisikie kile wanachozungumza au kile wanachopeana.

Kitendo hiki cha askari wa usalama barabarani kujadiliana na dereva au kondakta nyuma ya gari mahali ambapo abiria au mtu mwingine kwenye gari hawezi kusikia au kuona kinachoendelea, ni moja ya njia inayotumika kushawishi na kutoa rushwa.

Ikiwa gari limesimamishwa kwa lengo la ukaguzi wa leseni ya udereva kuna haja gani dereva kwenda kupaki mbali ilia pate nafasi ya kuonana na skari wa usalama katika mazingira ya vificho nyuma ya gari?

NJIA YA KUFYEKA KICHAKA HIKI
Na pendekeza serikali itengeneze sheria/kanuni ya usalama barabarani itakayo mtaka askari wa usalama barabarani kutokuwashusha madereva na kwenda kuzungumza nao nyuma ya gari.Zipo sababu za msingi ambazo tunaelewa kwamba hapa dereva analazimika kushuka mfano ukaguzi wa ndani ya gari sehemu ya dereva.Lakini huu utaratibu wa sasa ambao trafiki(traffic) anataka kujua kama una leseni alafu anasimamisha gari alafu anasubiria dereva ashuke amfuate wakutane nyuma gari naona ni njia tu yakutengeneza mazingira mazuri ya rushwa.

Kwanini askari akajadiliane na dereva nyuma ya gari la abiria?kuna siri gani ambayo abiria au msafiri kwenye gari la kawaida asiyotakiwa kujulikana kwa mtu mwingine? Serikali iangalie jambo hili kwasababu kitendo cha dereva na askari kukutana nyuma ya gari ni moja ya njia ya kuomba na kushawishi kutoa rushwa.

FAIDA YA KUWA NA SHERIA JUU KICHAKA HIKI
Faida ya kuwa na sheria/kanuni ya kumtaka askari azungumze na kondakta au dereva katika mazingira ya wazi ambayo abiria na watu wengine wanaweza kuona na kusikia kile kinacho semwa na pande hizo mbili ni kama ifuatavyo:

✔️Kutasaidia abiria au wasafiri wengine katika gari/basi kumjua vizuri dereva wao na kuelewa, makosa aliyonayo dereva na chombo chake cha usafiri kupitia kwa askari usalama barabarani (trafiki).
✔️Itamsaidia dereva na traffic kutokushawishiwa kutoa rushwa kwasababu ya uwazi wa mazungumzo yao mbele ya abiria au wasafiri wengine.
✔️Itawaongezea raia wengine ambao sio madereva uelewa wa ufanyaji kazi wa sheria barabarani.

✔️Itazuia rushwa barabarani kwa pande zote mbili za dereva(watoa rushwa) na askari wa usalama barabarani (waomba rushwa).
✔️Itaondoa hisia za rushwa zinazoweza kujengeka kwa trafiki wengine ambao hawajihusishi na ulaji rushwa.
✔️Itaondoa hisia za kuonewa kwa madereva na askari wetu,kwasababu askari ataeleza makosa ya dereva waziwazi na wengine wakisikia.

MWISHO
Rushwa ni Adui wa haki, vitabu vya dini vinatuambia kuwa Rushwa hupofusha macho hao waonao,rushwa hupotosha hukumu,rushwa hupofusha wenye akili,rushwa huaribu ufahamu,rushwa hupindua nchi nk.Tupinge rushwa tuokoe nchi yetu.🙏
 
Wewe utakuwa mtu wa takukuru, siyo bure.
 
Back
Top Bottom