Pensheni kwa Wastaafu na Wazee Zanzibar Zapandishwa

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,888
939

RAIS DKT. MWINYI APANDISHA PENSHENI KWA WASTAAFU NA WAZEE ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itapandisha pensheni kwa wastaafu kwa asilimia mia moja akitolea mfano wa mstaafu wa kima cha chini anayepokea shilingi elfu 90,000/= atapanda mpaka shilingi 180,000/=. Ametekeleza ombi la wastaafu hao walilolitoa mwaka jana .

Ameyasema hayo tarehe 01 Mei 2023 katika kilele cha Maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika Viwanja vya Skuli ya Nungwi, Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Rais Dk. Mwinyi amesema Serikali itapandisha pensheni jamii kwa asilimia mia moja na hamsini kwa Wazee kuanzia miaka 70 ambapo kwa sasa wanaopata elfu ishirini watapanda hadi shilingi elfu hamsini.
Utekelezaji wa mabadiliko hayo utaanza Mwezi Julai mwaka mpya wa bajeti utakapoanza.

Serikali inashukuru kwa namna Wafanyakazi walivyopokea kwa furaha mabadiliko ya mishahara yaliyofanyika.

Vilevile Dk.Mwinyi amesema mipango na mikakati ya Serikali ni kuimarisha uwajibikaji kwa kuzingatia namna ya kuboresha mazingira ya kufanyia kazi yakiwemo mishahara bora na stahiki nyengine za watumishi.

Dk Mwinyi amesema serikali ipo hatua za mwisho za kuanzisha mfumo wa Bima ya afya kwa wafanyakazi wote umma Zanzibar.

Amesema Serikali imepokea ombi la Wafanyakazi kupatiwa fedha za nauli kuwawezesha kwenda kazini na kurudi nyumbani nje ya mishahara yao.

📅 01 Mei 2023

📍Viwanja vya Skuli ya Nungwi, Mkoa wa Kaskazini Unguja.
 
Attachments

  • WhatsApp Video 2023-05-02 at 11.02.20.mp4
    16.3 MB
  • WhatsApp Image 2023-05-02 at 11.02.15.jpeg
    WhatsApp Image 2023-05-02 at 11.02.15.jpeg
    167.9 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-05-02 at 11.02.18.jpeg
    WhatsApp Image 2023-05-02 at 11.02.18.jpeg
    214.1 KB · Views: 2

RAIS DKT. MWINYI APANDISHA PENSHENI KWA WASTAAFU NA WAZEE ZANZIBAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itapandisha pensheni kwa wastaafu kwa asilimia mia moja akitolea mfano wa mstaafu wa kima cha chini anayepokea shilingi elfu 90,000/= atapanda mpaka shilingi 180,000/=. Ametekeleza ombi la wastaafu hao walilolitoa mwaka jana .

Ameyasema hayo tarehe 01 Mei 2023 katika kilele cha Maadhimisho ya siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika Viwanja vya Skuli ya Nungwi, Mkoa wa Kaskazini Unguja.

Rais Dk. Mwinyi amesema Serikali itapandisha pensheni jamii kwa asilimia mia moja na hamsini kwa Wazee kuanzia miaka 70 ambapo kwa sasa wanaopata elfu ishirini watapanda hadi shilingi elfu hamsini.
Utekelezaji wa mabadiliko hayo utaanza Mwezi Julai mwaka mpya wa bajeti utakapoanza.

Serikali inashukuru kwa namna Wafanyakazi walivyopokea kwa furaha mabadiliko ya mishahara yaliyofanyika.

Vilevile Dk.Mwinyi amesema mipango na mikakati ya Serikali ni kuimarisha uwajibikaji kwa kuzingatia namna ya kuboresha mazingira ya kufanyia kazi yakiwemo mishahara bora na stahiki nyengine za watumishi.

Dk Mwinyi amesema serikali ipo hatua za mwisho za kuanzisha mfumo wa Bima ya afya kwa wafanyakazi wote umma Zanzibar.

Amesema Serikali imepokea ombi la Wafanyakazi kupatiwa fedha za nauli kuwawezesha kwenda kazini na kurudi nyumbani nje ya mishahara yao.

📅 01 Mei 2023

📍Viwanja vya Skuli ya Nungwi, Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Huyu mwamba anapata boost sana kutoka jmt aendelee kula Bata tu
 
Back
Top Bottom