Serikali itabadilisha lini saini ya Waziri wa Fedha kwenye noti?

wa stendi

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
24,688
26,797
Kama mnavyojua aliekuwa Waziri wa Fedha kipindi hicho ni Dkt. Mpango na kwa sasa ni Makamu wa Rais hivyo noti za fedha zilikuwa na saini yake akiwa kama Waziri, kwa sasa Waziri Ni mwingine je! Kwanini saini ya Waziri husika isiwekwe kwenye noti?

Mpaka sasa akija mgeni asiyejua au mtoto anaenza kujua hela /noti akasoma yale maelezo pale kwa haraka haraka wanaona Waziri bado ni Mpango wakati Waziri kwa sasa mtu mwingine. Je, hili limekaaje?
 
Tunapunguza matumizi yasiyo muhimu mkuu, kuchapisha noti mpya ni gharama kubwa,na nchi yangu haina fedha hizo na hii sahihi haiathiri chochote kwenye uthamani wa fedha ,mkuu tufanye kazi in a smart way ili familia zetu ziwe bora na hii itapelekea taifa bora
 
Sasa iliopo pale ukimwonyesha mtoto si anaona waziri ni mpango?
 
Watz bana,mambo ya msingi ya kusemea yapo kibao huyu analeta jambo lisilo na madhara yeyote

Kwa hiyo wewe unakubali waziri wa fedha ni mpango?mbona waziri fulani alibadiloshwa au kutumbuliwa mnakuwa fasta kisema hapa abadilishe bio?
 
Kama mnavyojua aliekuwa Waziri wa Fedha kipindi hicho ni Dkt. Mpango na kwa sasa ni Makamu wa Rais hivyo noti za fedha zilikuwa na saini yake akiwa kama Waziri, kwa sasa Waziri Ni mwingine je! Kwanini saini ya Waziri husika isiwekwe kwenye noti?

Mpaka sasa akija mgeni asiyejua au mtoto anaenza kujua hela /noti akasoma yale maelezo pale kwa haraka haraka wanaona Waziri bado ni Mpango wakati Waziri kwa sasa mtu mwingine. Je, hili limekaaje?
Yani hilo Jambo madelu analiota kutwa kucha... Yaani nakwambia siku hiyo noti zetu zikisoma jina na saini yake nadhani atafanya sherehe kubwa sana.
 
Sasa iliopo pale ukimwonyesha mtoto si anaona waziri ni mpango?
Huyu mtoto anahitaji mambo muhimu zaidi kimaisha kuliko signature ya finance minister kwenye noti, watoto wetu wanahitaji elimu bora,afya bora na malezi yenye upendo kutoka kwa jamii yote.
 
Yani hilo Jambo madelu analiota kutwa kucha... Yaani nakwambia siku hiyo noti zetu zikisoma jina na saini yake nadhani atafanya sherehe kubwa sana.

Au mjina wake haupendezei kwenye hela ndio maana serikali imeamua kuacha kama lilivo
 
Back
Top Bottom