Serikali ipongezwe kwa kuongeza Mabasi Mwendokasi ruti ya Kimara tena yasiyo na rangi ya kijani maana Ruti hiyo haipendezwi na rangi ya kijani

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
34,059
Reaction score
79,406
Hamjambo wote!

1. Mapema wiki hizi kumekuwa na ongezeko la mabasi ya Mwendokasi Ruti ya Kimara Mbezi.

2. Mabasi ni mapya na mazuri.
3. Kiyoyozi na WiFi kama zote. Password utajua pakuipata.
4. Serikali kwa hilo ipongezwe kwa sababu kama yakiwa hayapo watu wanalalamika na kukosoa. Basi yakiwepo ni uungwana kupongeza na kushangilia.

5. Kingine mabasi yenye Rangi ya Kijani watu wengi wa huu ukanda walikuwa wakilalamika. Hawayapendi na wanapanda Huku wakisononeka.

6. Huku wakihusisha rangi hiyo na rangi ya chama kikuu. Ambapo wakazi wa ukanda huo wa Kimara Mbezi wengi wao sio wapenzi wa chama Kikuyu

7. Ingawaje kijani ni rangi kama rangi zingine. Na katika rangi kuu nzuri Kijani ni miongoni mwa rangi nzuri. Na baadhi ya magombo ya kale huhusisha rangi hiyo kama Rangi ya Peponi.

8. Kwa niaba ya Wapanda Mwendokasi. Naipongeza serikali kwa kusikia kilio cha wananchi wa Kimara Mbezi.

9. Ndio mambo ya serikali hayo. Kuhudumia wananchi wote bila ubaguzi hata kama unajua sio wapenzi wa chama ulichopo.

Barikiweni wote!

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
 
Mwendo wa wakazi wa daslamu kujambiana tu
20260313_200850.jpg
 
Mtu hapongezwi kwa kuhudumia familia yake, sana watoto watasema asante baba, familia umeitaka wewe, umeiunda wewe, kununua viatu tu upongezwe?😅

Kupongezwa kunatokana na kufanya Jambo zuri hata kama ni wajibu au jukumu lako.

Kupongezwa ni sehemu ya Shukrani Sijui kama unaelewa? Kukosolewa ni sehemu ya kulaumiwa sijui kama unaelewa
 
Hamjambo wote!

5. Kingine mabasi yenye Rangi ya Kijani watu wengi wa huu ukanda walikuwa wakilalamika. Hawayapendi na wanapanda Huku wakisononeka.

6. Huku wakihusisha rangi hiyo na rangi ya chama kikuu. Ambapo wakazi wa ukanda huo wa Kimara Mbezi wengi wao sio wapenzi wa chama Kikuyu
CCM bwana kuna watu wa ajabu sana. Wakati ule waligoma kabisa mabasi kuwa na rangi ya bluu eti ina promote Chadema, wakalazimisha yapakwe rangi za CCM! Halafu mnakiita chama kikomavu katika siasa wakati kina mambo ya kitoto namna hii
 
Kila MTU anauhuru wa kuchagua au kupenda rangi atakayo. Pia Kila MTU anauhuru wa kuwa na maoni kuhusu rangi aitakayo.
Rangi ni rangi.

Mtazamo wa CCM kuhusu Rangi ya Blue
Na mtazamo wa chadema kuhusu kijani wote wako katika Jambo lilelile
 
Kwani Chadema ndio walipendekeza mabasi yapakwe rangi ya bluu?
 
Sasa mbona wanalalamika yakiwekwa rangi ya kijani?
Kwa sababu kuyapaka rangi ya blue ilikuwa ni "coincidence", na kuyapaka rangi ya kijani ilikuwa ni maelekezo ya CCM. Kuna tofauti hapo. Ni sawa na wewe uwe shabiki wa Simba na mkeo anunue kanga ya kijani kwa kuwa tu ametokea kuipenda hiyo. Halafu unampa maagizo kwamba kanga inayofuata lazima iwe nyekundu. Sasa kama una watoto mashabiki wa Yanga watakuambia unakosea, kwa sababu wanaelewa mama yao kununua kanga ya kijani halikuwa suala la ushabiki.

Kwa kifupi, uamuzi wa mabasi kuwa blue haukufanyika kwa msukumo wa kisiasa, ila uamuzi wa mabasi kuwa kijani cha CCM ulifanyika kwa msukumo wa kisiasa. Sasa hii tayari imeanza kuleta mtafaruku wa kijinga kabisa, na waliosababisha ni CCM.
 
Hii dhana yako inaushahidi au ni makisio yako?
 
Mkuu, mimi sio wa kuongea kwa makisio. Haikuwa coincidence mabasi kuja ya kijani kipindi cha uchaguzi. Na kama unaamini ilikiuwa coincidence basi wewe ni mtu wa kuamini chochote kile.

Na sasa uchaguzi umepepita, suala la mabasi kuwa ya kijani halina uzito tena.
 
Mimi sina ushabiki. Sioni tofauti ya basi la kijani na blue au jekundu. Au zambarau ndio maana sikufikiria hayo mpaka nilipowasikia vijana wakieleza rangi ya kijani wakiihusha na CCM
 
Hamjambo wote!

1. Mapema wiki hizi kumekuwa na ongezeko la mabasi ya Mwendokasi Ruti ya Kimara Mbezi.

2. Mabasi ni mapya na mazuri.
3. Kiyoyozi na WiFi kama zote. Password utajua pakuipata.
4. Serikali kwa hilo ipongezwe kwa sababu kama yakiwa hayapo watu wanalalamika na kukosoa. Basi yakiwepo ni uungwana kupongeza na kushangilia.

5. Kingine mabasi yenye Rangi ya Kijani watu wengi wa huu ukanda walikuwa wakilalamika. Hawayapendi na wanapanda Huku wakisononeka.

6. Huku wakihusisha rangi hiyo na rangi ya chama kikuu. Ambapo wakazi wa ukanda huo wa Kimara Mbezi wengi wao sio wapenzi wa chama Kikuyu

7. Ingawaje kijani ni rangi kama rangi zingine. Na katika rangi kuu nzuri Kijani ni miongoni mwa rangi nzuri. Na baadhi ya magombo ya kale huhusisha rangi hiyo kama Rangi ya Peponi.

8. Kwa niaba ya Wapanda Mwendokasi. Naipongeza serikali kwa kusikia kilio cha wananchi wa Kimara Mbezi.

9. Ndio mambo ya serikali hayo. Kuhudumia wananchi wote bila ubaguzi hata kama unajua sio wapenzi wa chama ulichopo.

Barikiweni wote!

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
Tutashangilia tu ila kupongeza ni big NO!
 
Back
Top Bottom