mkiluvya
JF-Expert Member
- May 23, 2019
- 802
- 725
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene amesema Serikali ipo katika mchakato wa kuhakikisha Mahabusu waliopo katika Magereza mbalimbali nchini wanaanza kufanya kazi kama ilivyokuwa kwa wafungwa.
Amesema mchakato huo ambao tayari umeanza, utakapo kamilika utaleta mapendekezo madhubuti ya jinsi gani ya kuwatumia mahabusu hao pamoja na wafungwa katika kufanya kazi za uzalishaji mali na kuhakikisha Jeshi hilo linajitegemea kikamilifu.
Akizungumza na Maafisa na Askari Magereza katika Magereza ya Segerea, Ukonga na Keko jijini Dar es Salaam, leo, kwa nyakati tofauti alipofanya ziara ya siku moja ya kusisitiza magereza yanajitegemea nchini, alisema ili binadamu ale lazima afanye kazi, na pia vitabu vitakatifu vinasisitiza hilo, hivyo mahabusu wanapaswa kufanya kazi kwa kuwa nao wanakula vyakula magerezani.
“Kuna mjadala mkubwa tunaendelea kuchakata kuhusu mahabusu waweze kufanya kazi, lakini lengo letu sio kuwafanyisha kazi za sulubu, au kazi zinazotweza utu wao, hapana, wao pamoja na wafungwa wana adhabu wanayoitumikia, tunataka kuwatumia katika kuzalisha, kwahiyo watafanya kazi kama watu wengine wanavyofanya kazi, hili naomba lieleweke,” alisema Simbachawene.