YEHODAYA
JF-Expert Member
- Aug 9, 2015
- 36,900
- 52,053
Nchi za wenzetu zinakuwa na digrii zinazofundisha utengenezaji wa mashine mbali mbali.Watu hawa huweza unda kila aina za mashine ziwe za kilimo,viwandani, injini,meli .ndege nk ni watu ambao kama ambavyo watu husomea ujenzi wakawa wajenzi wa majumba na hawa wakitoka wakimaliza masomo huwa waundaji wa mashine za kila namna hata za kutengeneza vipuri mbali mbali.
Tunataka Tanzania ya viwanda ni wakati muafaka serikali kupeleka watu kusoma hizo digrii na pia wakirudi waweza saidia kuanzisha vitivo vya vyuo vikuu vya Machine Building au kuanzisha syllabus VETA ya mafunzo ya utengenezaji mashine.
Watu hao ni muhimu mno katika nchi inayotaka kuingia kwenye viwanda.Kwa sasa wataalamu wengi tunaowatoa kwenye elimu yetu ni mafundi makenika wa kutengeneza vililivyoharibika vilivyotengenezwa sio wataalamu wa kuunda mashine!!! Tupate wataalamu wetu wa kuunda mashine sio mafundi makenika tu wa mashine!! Tuwe na wataalamu wetu wa kuunda magari sio mafundi makenika wa kutengeneza gari lililoharibika tu la mjapan.Digrii hizo pia zaweza zalisha watu wanaoweza jiajiri na kuanzisha viwanda vyao vya kuunda mashine na mitambo mbalimbali.
Ni wakati wa kuondokana na kuzalisha makenika na kuanza kuzalisha waunda mashine
yehodaya123@gmail.com