Nimejaribu kufuatilia kwa karibu mambo yanayotokea kufuatia CDM kuamua kuandamana kupinga mwenendo wa BMK nimejikuta ninapata shida kuamini kuwa nchi yetu ina intelijensia iliyo makini. Sidhani kama kuazimia kuandamana ni kosa. Bila shaka ni vibaya kuandamana bila kufuata utaratibu. Nimeshangaa polisi kupiga marufuku maandamano hata kabla ya taarifa za dhamira ya kuandamana kupelekwa katika ofisi zao.
Nimeshawishika kuamini kwamba huenda serikali kupitia jeshi lake la polisi kama wangeamua kushirikianana na CDM kuandaa na hatimaye kuyasimamia maandaano yao huenda impact ya maandamano hayo isingekuwa kubwa kama dhamira ya CDM ilivyokuwa. Kitendo cha kuyazuia kimeifanya CDM kuwa yenye mafanikio makubwa kwani imewafanya watanzania wajue kuwa kuna ufisadi katika serikali na chama tawala. Ni kweli watu wengi wakiwemo watoto wamejua kuwa serikali yao ni dhalimu kwa kuona mabavu yanayotumika.