baraka bb
JF-Expert Member
- Mar 20, 2016
- 2,691
- 3,878
Habari zenu wakuu!
Mimi ni dereva wa fuso ya kubeba mchanga, huwa tunafata mchanga Kibaha na kupeleka Dar es Salaam. Kipindi cha nyuma tulikuwa tunafanya kazi usiku na mchana na huwa tunanunua mchanga sh 10000/= ushuru wa halmashauri Kibaha 3000/= na Kinondon 1000/=
Halmashauri ya Kibaha ikaleta tamko kwamba tuwe tunafanya kazi kuanzia saa 12 asubuh - 12 jioni. Kumbuka tulikuwa tunalipa kodi kwa kila trip 1 na tulikuwa na uwezo wa kupiga trip zaidi ya 10 ila sasa hivi tunaenda trip 3 hadi 4 kutokana na ufinyu wa muda.
Kilichotokea leo hii tunapita hapa kwenye kulipia kibali cha mchanga (ushuru) mtu wa halmashauri anatuzuia anataka tulipe faini 50,000/=. Anasema ilitakiwa saa12 ndo tuingie shamba sio tuwe tunatoka kama tulivyofanya leo.
Je hii ni sahihi kwa nchi inayoendelea kama hii kupangiwa muda finyu wa kufanya kazi? Je Serikali kuu inatambua hili tunalofanyiwa?
Hadi sasa bado tumekaa hapa Kibaha TAMCO tunasubiri muafaka, hatuwezi kulipa faini ya ajabu hivi kwani huu ni uonevu!