Serikali inaangalia uwezekano wa kuongeza malipo ya mafao ya wastaafu

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Profesa Joyce Ndalichako amesema uamuzi wa kuongeza malipo ya kila mwezi utafanyika baada ya tathimini kuona uhimilivu wa mifuko ya Hifadhi ya Jamii.

Ndalichako alikuwa akijibu swali kuhusu kuwalipa warithi 67% ya michango pindi mstaafu anapofariki ambapo amesema mafao yanayolipwa hayazingatii asimilia ya michango isipokuwa wastaafu na wategemezi hulipwa kwa mujibu wa kanuni za mafao ya pensheni.

Profesa Ndalichako amesema Mfuko wa PSSSF hulipa mafao ya mkupuo ambayo ni pensheni ya miezi 36 kwa wategemezi wakati NSSF mstaafu anapofariki Mfuko hulipa mafao ya mkupuo sawa na pensheni ya miezi 24 kwa wategemezi.
 
Wategemezi ni mgane/mjane na watoto wa chini ya miaka 18 bila shaka.

Je kama huyo mstaafu hana watu wenye sifa hizo?

Ikitokea mstaafu akafa kabla ya kupata lumpsum yake hiyo kuwapa wategemezi pension ya miezi 36 pekee ni dhulma ya wazi.
 
Back
Top Bottom