Serikali imeshinda kesi 352 mwaka 2024/25

Serikali imeshinda kesi 352 mwaka 2024/25

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,770
Reaction score
1,173
SERIKALI IMESHINDA KESI 352 MWAKA 2024/25

Katika kipindi cha kuanzia mwezi Julai, 2024 hadi Machi, 2025,
Kesi 867 ziliendeshwa mahakamani zikiwemo kesi mpya 461.

Kati ya kesi mpya zilizofunguliwa mahakamani, 10 ni kesi kubwa ambazo zilifunguliwa katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi.

Kesi 451 ziliamuliwa mahakamani ambapo Jamhuri ilishinda kesi 352 kwa watuhumiwa kuhukumiwa kifungo au/na kulipa faini ikiwa ni asilimia 76.4.

Aidha, hadi kufikia Machi, 2025 kesi 416 zilikuwa zinaendelea mahakamani.

Vilevile, kiasi cha shilingi bilioni 9.01 na USD 620,000 zimeokolewa kutokana na operesheni mbalimbali za uchunguzi uliofanyika kote nchini ambapo shilingi bilioni 6.01 ni fedha taslimu zilizorejeshwa serikalini na shilingi bilioni 3.00 na USD 620,000 zilidhibitiwa na kurejeshwa katika miradi mbalimbali ya Serikali na kwa walalamikaji wa Sekta binafsi.

Huu ni utekelezaji wa bajeti ya serikali kwa mwaka 2024/25 kwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).
 

Attachments

  • VID-20250425-WA0017.mp4
    34.8 MB
Back
Top Bottom