Ofisi ya Rais Utumishi: Baadhi ya Waajiri kuficha Barua za Uhamisho wa Watumishi tatizo ni nini?

Sir John Roberts

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
9,639
15,970
Hili naona kama linataka kuzoeleka kwa baadhi ya waajiri (hasa kwenye serikali za mitaa) unakuta mtumishi amepata uhamisho lakini mwajiri anaficha au anamzungusha kumpa uhamisho wake hii si sawa (kimsingi ni insubordination kwa maelekezo ya Katibu Mkuu mwajiri wa Halmashauri kuyadharau). Hii inatokea huko halmashauri moja mikoa ya kanda ya nyanda za juu kusini sitaitaja kwa sasa ila ikibidi nitaitaja ili kuweka bayana wahusika.

Tukumbuke watu hawa wanapopata transfer hizi wanakuwa na malengo mbalimbali either wao wenyewe au serikali imeona kuna ulazima wa kumuhamisha mtumishi huyo ili kuboresha utendaji kazi wa watumishi hawa.

Naiomba Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma kwa kushirikiana na TAMISEMI wafanye ufuatiliaji kwa Waajiri wanaozuia kutoa barua za uhamisho kwa watumishi wao bila sababu za msingi na wachukuliwe Hatua kali za kinidhamu.

Ahsante.
 
Hii ni kawaida kwa halmshauri nyingi kama sio zote! KM anajikunja kuhamisha watumishi 100 umbe waliohama ni 3 aibu kubwa 🤭🤭🤭! Au hili nalo inahitaji bulldozer?. Yaani watu wako Mawizarani na PhD ishu ya chekechea hii mayo inawashinda? Basi nanyie muitwe local hahahaha!
 
Back
Top Bottom