Serikali imepata ugonjwa mbaya

Serikali imepata ugonjwa mbaya

Magari yote ya maofisa yapelekwe vijijini kwenye production....
 
usishangae kumsikia Makonda naye akitoa tamko la kuhamia Dodoma!
1469685442038.jpg
 
Umesema vyema kabisa!

Pamoja na hayo ningeiomba serikali itumie fursa ya kuhamia Dodoma kurekebisha muundo wake. Ilivyo sasa Wizara zina wafanyakazi wengi kuliko inavyo hitajika. Hakuna sababu ya watendaji kubaki wizarani kwani Wizara kazi yake ni kuratibu utendaji na kusimamia sera.

Tatizo la pili ni kuwa watendaji wa hizo sera wote kwa sasa wapo TAMISEMI chini ya DED. Kinachotokea ni kuwa kuna multiple chain of command kwenye district level inayosababisha conflicts kwenye unit of practice/implementation yaani local communities. Mfano wa mgongano huu unaonekana wazi na dhahiri zaidi kwenye issue za ardhi. Nikipata platform nitalieleza hili viziri. Hakuna connection kati ya watendaji wa sector za wizara kama ardhi, mali asili, maji, mazingira nk kwenye constitutional level yaani wizara na kule wanapo practice yaani local government. Matokeo yake ni tofauti ya de jure na de facto..pia hii imesababisha migogoro kwenye vijiji vingi hasa kupitia miradi ya wafadhili.

Tatizo la tatu ni kuwa japo kuwa watendaji wapo huku local areas yaani kwa wananchi...watendaji wakuu kama Wakurugenzi wa wizara wapo wizarani na spending yao ni mara tatu ya ile ya ngazi ya vijiji. Hii pia inachagizwa na transaction costs ya command/information flow kutoka wizarani kwenda kijijini. Matokeo yake ni spending kubwa ya budget ya serikali inakuwa wizarani kwenye service provision kuliko grassroot kwenye production level. Hii inachangia sana kudidimiza maendeleo kwani kuna inefficiency kubwa mno kwenye matumizi ya budget. Hii ndiyo iliyopelekea wafanyakazi wizarani ku device jinsi ya kitumia pesa kirahisi kwakuweka trainings na workshop zisizo isha.

Ni vizuri basi wizarani kukabaki unit ndogo ya kuratibu sera na watendaji wote wakapelekwa kwenye district level mpaka village ili kusimamia shughuli za uzalishaji kitaalama kuliko ilivyo sasa ambapo locals hawapo coordinated.

Implication ya kupeleka watendaji/wataalamu wote kwenye production level kutasababisha cash/finance kwenda at village level na hii ikitokea itasababisha rural economy ibadilike from batter to cash. Masoko ya mazao yatakuwepo na specialization kwenye production itatokea ki urahisi.

Inahitaji waziri wa mipango na team yake yote pamoja na wachumi kuchanfamkia hii fursa kwani ndiyo njia pekee ya kusababisha BIG PUSH theory kuwa reality...

Nimeipenda analysis yako, at least umekuja na solutions, siyo mijandaheka mengine inakuja na utumbo usioeleweka wala kuelezeka.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Hatuna dira wala mipango ya maendeleo, maana hatuelewi tunafanya nini,
Kila siku linakuja jambo jipya, wote wanahama, ilikuwa ziara za kushtukiza wote wakaingia, ikaja kutumbua wote, watumishi hewa wote, vyeti wote, sasa dodoma wote, wameshasahu tena habari za msako wa sukari itakwisha miaka 5 hakuna kilichofanyika,
Huyu kweli hakuwa amejiandaa kuwa rais huo Ndio ukweli

Dira na mpango wa maendeleo upo lakini hautiliwi maanani, Kuna Dira ya maendeleo ya Taifa 2025, Mpango wa taifa wa miaka mitano 2016-2021. Na kipaumbele cha mpango wa maendeleo ni viwanda na elimu itakayowezwsha kukua kwa viwanda.
 
Mleta mada huna fikra na nnakushauri uanze kutumia kichwa chako kwa kufikiri japo kiduchu kuliko kukiacha kama mzigo tu mabegani mwako.

Wizara zote kila kikao cha bunge huhamia Dodoma, sasa fikiri kwa mwaka kuna vikao vingapi vya bunge?

Hizi wizara na safari za bungeni zisizoisha ni mzigo mkubwa kwa taifa. Alivyofanya Magufuli ni vyema sana.

Sasa ni wakati wa "Black or White and no gray shades".

Nimeipenda analysis yako, at least umekuja na solutions, siyo mijandaheka mengine inakuja na utumbo usioeleweka wala kuelezeka.
Wewe ukiwa mmojawapo, soma upuuzi ulioandika hapo juu
 
Watanzania nani ameturoga? Yaani ni mtu anaweka umbea tayari watu tunaotegemea wangeonesha walivyoelimika nao wanaanza kutiririka kwa "speculations" na maoni binafsi "opinions"! Au mfumo wetu wa elimu una kasoro? Au ndio ya vyeti bandia? Kwanini hatuoni constructive criticism? Zitusaidie kuona umuhimu au mapungufu ya viongozi wetu? Halafu mnadai kupewa ajira, kwa lipi? Napita tu.
 
Sijadili kutangulia Najadili dhana ya kukurupuka
Hawajakurupuka Mkuu maana ni kitu ambacho alitoa ahadi siku nyingi tu. Kwahiyo naona anatimiza ahadi yake. Naona neno kukurupuka umelikosea mkuu. Hapo ulitakiwa kusema wanatekeleza haraka amri ya mkuu wao.

Pia, Unamaanisha nini kusema serikali inahamia vichakani Mkuu?? Ulitaka serikali siku zote iwe Dar es salaam tu??

Ningeona posti yako ya maana sana kama ungezungumzia kuhusu kuhamishwa kwa serikali kwenda dodoma badala kutatua kero za wananchi wake mfano kuhakikisha Maji safi, kuboresha miundo mbinu mzuri katika suala la ajira kwa vijana kwa kubadilisha changamoto mbali mbali kuwa fursa kwa vijana.

Haki maoni( Fair comment).
 
Naomba unielewe tena nilichoandika, sipingani na wazo la kuhamia Dodoma hata maramoja, nazungumzia mkakati na mipango yenye kueleweka na si kukurupuka
Umezungumzia kuhusu wizara tu lakini kumbuka kuna mengi hapo
-majeshi
-Vyombo vya ulinzi na usalama
-miundombinu yote hasa airport
Kikubwa kuliko yote ni gharama ambayo haitajwi popote, kumbuka unahamisha makao ya nchi na si familia
Ili mambo yasiyumbe kuwe na mkakati madhubuti kwenye hili sio kwakuwa Magu kasema basi kila mtu alipuke kusema anahama siku fulani
Iundwe task force ya wataalam wa kila sekta ambao watapanga uhamisho huo
Kwamba 2017 zitahama wizara hizi, 2018 2019 hivyo hivyo
BTW uamuzi huu wa sasa ni wa baraza la mawaziri au umepitishwa na bunge lipi?
Mkuu mshana Jr: kuhusu suala la jeshi nafikiri hata Dodoma lipo.

Vyombo vya usalama vipo kama kawaida.

Uwanja wa ndege upo unahitaji kurekebishwa tu. Pia najisikia mwenye furaha sana kuhusu huo uwanja wa ndege ambao upo mbioni kujengwa mkoani Dodoma ili tuweze kuwa na viwanja vikubwa vingi na sio viwe Dar es salaam tu. Hii itapelekea kidogo kuwa na uwianao ya maendeleo.

Je ni jeshi la aina gani unataka liende Dodoma? Au chombo gani cha usalama unataka kiwepo Dodoma ambacho hakipo?

Ngoja serikali ihamie Mkoani Dodoma na watu wa bara wapate unafuu kidogo mkuu na sio kila kitu Dar es salaam.
 
Serikali ikihamia Dodoma Tanzania itakuwa moja hatutakuwa na mambo ya Bara na Visiwani
 
Mkuu mshana Jr: kuhusu suala la jeshi nafikiri hata Dodoma lipo.

Vyombo vya usalama vipo kama kawaida.

Uwanja wa ndege upo unahitaji kurekebishwa tu. Pia najisikia mwenye furaha sana kuhusu huo uwanja wa ndege ambao upo mbioni kujengwa mkoani Dodoma ili tuweze kuwa na viwanja vikubwa vingi na sio viwe Dar es salaam tu. Hii itapelekea kidogo kuwa na uwianao ya maendeleo.

Je ni jeshi la aina gani unataka liende Dodoma? Au chombo gani cha usalama unataka kiwepo Dodoma ambacho hakipo?

Ngoja serikali ihamie Mkoani Dodoma na watu wa bara wapate unafuu kidogo mkuu na sio kila kitu Dar es salaam.
Hebu nisome kwa kutulia upate maana halisi ya kile nilichoandika
 
Kijana,epuka kumquote mtu kama hutambui na wala huelewi falsafa yake..

Words should first be given their literal meaning, ya falsafa yanakuja baada ya literal meaning kuwa absurd
 
Nimeipenda analysis yako, at least umekuja na solutions, siyo mijandaheka mengine inakuja na utumbo usioeleweka wala kuelezeka.
Hili ni janvi ukaliwa na kila mtu na sikila anayelikalia ana akili kama ya uliyemsifia, na dunia ndivyo ilivo
 
Back
Top Bottom