Serikali imepata ugonjwa mbaya

Serikali imepata ugonjwa mbaya

Huo mgawanyo wa madaraka ndo umetufikisha hapa tulipo
Nadhani hukunielewa lakini iko hivi unapoendesha gari ya gia na ukapanda mlima huanzi kupanda na gia no moja kwakuwa ikifeli katikati ya mlima umekwisha hivyo unatakiwa kuanza kupanda na gia ndogo ili ikifeli kuna backup
Nyerere alitumia sana mfumo huu. ! maamuzi ya wakuu wa wilaya maamuzi ya wakuu wa mikoa, maamuzi ya bunge maamuzi ya baraza la mawaziri na maamuzi ya mkuu wa nchi
Mambo ya Mchonga yalienda vizuri kukiwa kuna mfumo rasmi wa uwajibikaji na kipi kifanyike vipi lini na nani ahusike (kwenye serikali hii hakuna kitu kama hiki)
Kuna baadhi ya watendaji wa Mchonga waliboronga tena pengine kwa ushauri wake..lakini kiutendaji akawawajibisha kwakuwa maamuzi husika yalikuwa kwenye ngazi yake
Hatari ya maamuzi yanayotoka juu moja kwa moja ni hii akikosea mkuu nani atamwajibisha? Hii ni sawa na kupanda mlima na gia no moja. ..ikifeli ni zahama!

6
 
Mimi na Amini Mheshimiwa Raisi.. PM Majaliwa.. Tizeba.. wote hawakukurupuka... safari hii lile lilokua likionekana haliezekani... mara hii linapata political will... ndugu zangu Wana JF... jitaarisheni kisaikolojia kupokea lile ambalo imani zenu hazitaki kulipokea... lile ambalo masikio yenu Hayataki kulisikia... Safari hii linakwenda kuwa kweli... Na ushauri bure kabisa... instead of kukaa humu ndani kuanzisha thread za kulaumu na kuonyesha rejection ya linalokwenda kutokea.. lets be constructive na kuanza kukimbilia fursa dodoma.. za kwenda nunua viwanja.. kuekeza.. na kucapitalize kwenye hii Move tukufu ya Serikali ya kuendesha serikali kutokea dodoma.. ni hayo machache kwa jioni hii...
 
Hapa ni sehemu ya panapotarajiwa kuwa makao ya nchi , mlima huu ndipo penye kisima kikubwa kilichomaliziwa kujengwa na wachina hivi karibuni, je ujenzi wa kisima hicho umezingatia huu uhamisho mkubwa?
1469648777628.jpg
 
1469649748340.jpg
Dodoma city centre
1469649768521.jpg
university of Dodoma
1469649794916.jpg
 
Kwa hiyo nyie chadema hata hili la kuhamia Dodoma mnalipinga ??

Nakumbuka Mbowe na Lowasa wakati wakiomba kura Dodoma waliahidi serikali ya UKAWA itahamia Dodoma haraka Mara tu baada ya kuapishwa.
Je mlikuwa mnawadanganya watanzania??

Kwa unafiki wenu huu mnafaa kweli kuongoza hata mtaa??
Hatuzungumzii chama hapa hata hao ukawa lait kama wangefanya hivyo kwa haraka mno wangelaumiwa.
 
Magufuli rais wangu,mambo ufanyika kwa mipango na sio matamko,kwani wakati budget inapangwa hichi kitu hakikuwwpo!ebu tufanye kazi kwa mipangilio na si kuamka asubuhi na kutoa matamko.Anyway all the best Magufuli tunakuombea ila ujue hata Mungu akujenga dunia kwa siku moja alipanga na kuji evaluate ndipo alipoendeleo na hatua nyingine.Dodoma serekali itaamia ila kwa mpangilio jamani
 
Ukiambiwa kuna watu wanaweza kuja kupinga hata reply ya namna hii...! Kweli hatufanani
 
Kwa hiyo nyie chadema hata hili la kuhamia Dodoma mnalipinga ??

Nakumbuka Mbowe na Lowasa wakati wakiomba kura Dodoma waliahidi serikali ya UKAWA itahamia Dodoma haraka Mara tu baada ya kuapishwa.
Je mlikuwa mnawadanganya watanzania??

Kwa unafiki wenu huu mnafaa kweli kuongoza hata mtaa??
Mwenye akiri timamu hawezi kupinga kuhamia Dodoma, je ni kwa style gani? Na muda gani? mwenye akiri timamu hawezi kupinga adhabu kwa mtoto aliyeiba hela za jirani na kwenda kula vitumbua lakini je ni adhabu gani unampa huyo mtoto , hivi ni kweli umuunguze mikono na miguu na useme ndio adhabu inayomfaa halafu akitokea mtu akamtetea huyo mtoto na wewe unamuona huyo mtu hana akili.
 
Kwa hiyo nyie chadema hata hili la kuhamia Dodoma mnalipinga ??

Nakumbuka Mbowe na Lowasa wakati wakiomba kura Dodoma waliahidi serikali ya UKAWA itahamia Dodoma haraka Mara tu baada ya kuapishwa.
Je mlikuwa mnawadanganya watanzania??

Kwa unafiki wenu huu mnafaa kweli kuongoza hata mtaa??
Mkuu wewe mwimba kwenye kidonda kibichi.
 
Mijitu mingine bwana yaani kuamia dodoma kuna shida ganj hata kesho
 
Mijitu mingine bwana yaani kuamia dodoma kuna shida ganj hata kesho
Duu chukua muda basi uandike vizuri haraka za nini?
-kuamia-kuhamia
-dodoma- Dodoma
-ganj-gani
Kwa uandishi wa namna hii siwezi hata kukulaumu kwa reply yako hii
 
Mleta mada huna fikra na nnakushauri uanze kutumia kichwa chako kwa kufikiri japo kiduchu kuliko kukiacha kama mzigo tu mabegani mwako.

Wizara zote kila kikao cha bunge huhamia Dodoma, sasa fikiri kwa mwaka kuna vikao vingapi vya bunge?

Hizi wizara na safari za bungeni zisizoisha ni mzigo mkubwa kwa taifa. Alivyofanya Magufuli ni vyema sana.

Sasa ni wakati wa "Black or White and no gray shades".
 
hivi hizi wizara miaka yote zimeshindwa kuwa na visurb wizara mikoani leo ndiyo zinaleta mbwembwe za kuhamia Dodoma?
una manufaa gani kwangu wizara kuhamia huko?
ilhali bado nitasafiri kutoka Nanjilinji kuifuata wizara,
kikubwa muweke na ofisi za kanda tusaidiwe shida zetu huko.
 
Waziri mkuu kuhamia Dodoma hata kesho ni sawa tu. Ofisi ya Waziri mkuu Dodoma ina miundo mbinu mikubwa na bora kuliko ile ya DSM. Hakuna shida juu ya hilo aende tu. Pia hata wizara ya Nishati na madini haiko kiwango cha chini, miundo mbinu imeboreshwa na inaendelea kuboreshwa, hivyo hata mheshimiwa Muhongo anaweza kuhamia hata kesho. Yaliyo baki anaweza kuyaweka sawa akiwa hukohuko.

Zipo taasi nyingi zimeboresha miundo mbinu yake Dodoma. Hivyo kuhamia ni suala la maamuzi tu. Rais hajakurupuka, waziri mkuu hajakurupuka, waende tu. Hakuna sababu za kuwazuia.

Mkumbuke hawa wote sio wageni Dodoma, Ila sisi watanzania hatuijui Dodoma. Dodoma ya Nyerere ni tofauti kabisa na hii Dodoma tunayoizungumza Leo.
 
Kuhamia Dodoma si ugonjwa wala kwenda kichakani hata Kama watahamia Leo hakuna shida kwani wizara zote wana ofisi Dodoma kipindi kirefu na wanaweza kufanya kazi Kwa mtandao Kama bank zinavyofanya kazi, Malawi, Nigeria, India , Brazil nk walihamia miji mipya pasipo kukamilisha Kila kitu wakajiimarisha wakiwa huko huko na baadhi ya wizara na ofisi za balozi zipo miji ya zamani na maisha yameendelea , changamoto lazima ziwepo lakini lazima serikali wahamie Dodoma kulipisha jiji la Dar kujijenga Kwa kasi pia itasaidia kusambaza maendeleo mikoani .

Umesema vyema kabisa!

Pamoja na hayo ningeiomba serikali itumie fursa ya kuhamia Dodoma kurekebisha muundo wake. Ilivyo sasa Wizara zina wafanyakazi wengi kuliko inavyo hitajika. Hakuna sababu ya watendaji kubaki wizarani kwani Wizara kazi yake ni kuratibu utendaji na kusimamia sera.

Tatizo la pili ni kuwa watendaji wa hizo sera wote kwa sasa wapo TAMISEMI chini ya DED. Kinachotokea ni kuwa kuna multiple chain of command kwenye district level inayosababisha conflicts kwenye unit of practice/implementation yaani local communities. Mfano wa mgongano huu unaonekana wazi na dhahiri zaidi kwenye issue za ardhi. Nikipata platform nitalieleza hili viziri. Hakuna connection kati ya watendaji wa sector za wizara kama ardhi, mali asili, maji, mazingira nk kwenye constitutional level yaani wizara na kule wanapo practice yaani local government. Matokeo yake ni tofauti ya de jure na de facto..pia hii imesababisha migogoro kwenye vijiji vingi hasa kupitia miradi ya wafadhili.

Tatizo la tatu ni kuwa japo kuwa watendaji wapo huku local areas yaani kwa wananchi...watendaji wakuu kama Wakurugenzi wa wizara wapo wizarani na spending yao ni mara tatu ya ile ya ngazi ya vijiji. Hii pia inachagizwa na transaction costs ya command/information flow kutoka wizarani kwenda kijijini. Matokeo yake ni spending kubwa ya budget ya serikali inakuwa wizarani kwenye service provision kuliko grassroot kwenye production level. Hii inachangia sana kudidimiza maendeleo kwani kuna inefficiency kubwa mno kwenye matumizi ya budget. Hii ndiyo iliyopelekea wafanyakazi wizarani ku device jinsi ya kitumia pesa kirahisi kwakuweka trainings na workshop zisizo isha.

Ni vizuri basi wizarani kukabaki unit ndogo ya kuratibu sera na watendaji wote wakapelekwa kwenye district level mpaka village ili kusimamia shughuli za uzalishaji kitaalama kuliko ilivyo sasa ambapo locals hawapo coordinated.

Implication ya kupeleka watendaji/wataalamu wote kwenye production level kutasababisha cash/finance kwenda at village level na hii ikitokea itasababisha rural economy ibadilike from batter to cash. Masoko ya mazao yatakuwepo na specialization kwenye production itatokea ki urahisi.

Inahitaji waziri wa mipango na team yake yote pamoja na wachumi kuchanfamkia hii fursa kwani ndiyo njia pekee ya kusababisha BIG PUSH theory kuwa reality...
 
Naomba na lumumba iwe ya kwanza kuhamia dodoma tuone figisu itskayotokea
 
Waziri mkuu kuhamia Dodoma hata kesho ni sawa tu. Ofisi ya Waziri mkuu Dodoma ina miundo mbinu mikubwa na bora kuliko ile ya DSM. Hakuna shida juu ya hilo aende tu. Pia hata wizara ya Nishati na madini haiko kiwango cha chini, miundo mbinu imeboreshwa na inaendelea kuboreshwa, hivyo hata mheshimiwa Muhongo anaweza kuhamia hata kesho. Yaliyo baki anaweza kuyaweka sawa akiwa hukohuko.

Zipo taasi nyingi zimeboresha miundo mbinu yake Dodoma. Hivyo kuhamia ni suala la maamuzi tu. Rais hajakurupuka, waziri mkuu hajakurupuka, waende tu. Hakuna sababu za kuwazuia.

Mkumbuke hawa wote sio wageni Dodoma, Ila sisi watanzania hatuijui Dodoma. Dodoma ya Nyerere ni tofauti kabisa na hii Dodoma tunayoizungumza Leo.
Naomba unielewe tena nilichoandika, sipingani na wazo la kuhamia Dodoma hata maramoja, nazungumzia mkakati na mipango yenye kueleweka na si kukurupuka
Umezungumzia kuhusu wizara tu lakini kumbuka kuna mengi hapo
-majeshi
-Vyombo vya ulinzi na usalama
-miundombinu yote hasa airport
Kikubwa kuliko yote ni gharama ambayo haitajwi popote, kumbuka unahamisha makao ya nchi na si familia
Ili mambo yasiyumbe kuwe na mkakati madhubuti kwenye hili sio kwakuwa Magu kasema basi kila mtu alipuke kusema anahama siku fulani
Iundwe task force ya wataalam wa kila sekta ambao watapanga uhamisho huo
Kwamba 2017 zitahama wizara hizi, 2018 2019 hivyo hivyo
BTW uamuzi huu wa sasa ni wa baraza la mawaziri au umepitishwa na bunge lipi?
 
Hakuna haja ya kuwaleta Dodoma watu....waje tu waziri, Katibu Mkuu na wasaidizi....wengine wote waratibiwe na halmashauri kuwa absorbed katika sector husika.

Huvi huko wizarani kuna kazi gani zaidi ya kuhangaikia mafaili ya wafanyakazi waliojazana huko na accounting issues za transactions zisizo na tija?

Zama hizi za technology iliyo advance unahitaji watu wizarani kufanya kazi gani? Tuangalie wizara za nchi zilizoendelea au taasisi zao zina watu wangapi kwenye coordination level?

Kama tumedhamiria kuvunja statusquo acha Mh. Rais ambaye ameonyesha uthubutu afumue serikali tuumie kwa muda then baadaye dust iki settle kila mtu atakuwa ameshakamata "jembe lake" alime ili asife....HAPA KAZI TU!
 
Back
Top Bottom