Huko tuendako ni kubaya....
Walioweka mfumo wa utawala wa sheria na mgawanyo wa madaraka na majukumu walifanya hivyo kutokana na uzoefu na shida zilizopata kutokea
Nasikitika kusema kuwa tunachanja mbuga kuelekea vichakani na hatari ni kubwa kwakuwa vichaka vina mengi
Sasa hivi hakuna mipango thabiti ya tulipo na tunakoelekea, akiongea tu Mkuu wa nchi serikali nzima inalipukia huko...tushukuru Mungu mpaka sasa hakuna matamko mabaya sana....lakini hatujui ya kesho...huwezi jua ataamka kesho aseme nini....!
Kwenye mkutano wa kukabidhiwa uenyekiti wa chama pale Dodoma mkuu aliweka nadhiri ya kuhamia Dodoma kabla ya kipindi chake cha kuongoza kwisha...bado ana miaka minne na miezi miwili
Kilichofuatia ni matamko ya mlipuko toka kwa watendaji wake...waziri mkuu akasema atahamia Dodoma mwezi wa tisa, lakini jana waziri Chizeba (kilimo?)akasema yeye atahamia wiki jayo na magazeti yakalipuka na Chizeba ampiga bao waziri mkuu (sort of comedians)
Tusubiri matamko zaidi toka kwa wengine usishangae hata wakuu wa mikoa na wilaya nao wakatoa matamko ya kuhamia Dodoma

Mkuu wenu kasema akishahamia Dodoma wengine watafuata..! Sasa haraka ya nini? Sifa au nidhamu ya woga? Kumbukeni kuhamisha wizara ni tofauti kabisa na kuhamisha familia..!
Kuna mengi ya muhimu ya kufanya kwa sasa acheni hizo