Serikali imenyoosha mikono dhidi ya watoa huduma za tv!

Babu Kijiwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2010
4,762
4,576
MODERATOR USIFUTE HUU UZI WALA KUUNGA NA NYUZI NYINGINE KWA MANUFAA YA UMMA
Nimepitia kwa uangalifu mwongozo wa TCRA juu ya kuonekana kwa local cuannels bure.. TCRA wanasema kwamba makampuni ya Startimes, Ting, Continental na Digitek hayajajisajili kama Pay TV hivyo yanapaswa kuonesha local channels BILA MALIPO. Hata hivyo makampuni ya Zuku, Azam, Multchoice yamesajiliwa kama pay TV hivyo watumiaji wanapaswa kulipia channels zake zote ikiwa ni pamoja na local channels.

Katika hali ya kushangaza ni namna TCRA, Mawaziri wa mawasiliano na viongozi wengine wa serikali wanavyokuwa WANYONGE ikifika suala la kujibia hili. Matamko mbalimbali yametolewa Bungeni kuyaamuru makampuni yasiyo pay tv kuachia local channels lakini hakuna kinchofanyika, mpaka sasa Startimes, Ting, Continental hawaachii local channels bure.

Niliwauliza TCRA wakasema tatizo ni wamiliki wa hizo local channel kushindwa kulipa gharama za uendeshaji kwa makampuni ya Startimes, Ting, Continental na Digitek hivyo kukatiwa huduma.

Hayo ni majibu mepesi sana na yakitoto, kwani wanachotaka watanzania ni kupata habari kama zamani (kabla ya digital) haya mambo ya nani anakwamisha HAYATUHUSU sisi watumiaji na yanapaswa kumalizwa.. halafu nashangaa kama mliweza kukimbizana na bloggers na wakatii ndani ya muda mfupi, mnashindwa nini kuwaadhibu wanaokwamisha?

MODERATOR IKIWEZEKANA U PIN HUU UZI WAHUSIKA WAONE
 
Mfupa mgumu kwa TCRA.

Walivyotulia utafikiri hawajui kinachoendelea, na wasivyojali sijawahi hata kusikia wakitolea ufafanuzi kwa Wanainchi tulioahidiwa "mtaona bure".
 
Mfupa mgumu kwa TCRA.

Walivyotulia utafikiri hawajui kinachoendelea, na wasivyojali sijawahi hata kusikia wakitolea ufafanuzi kwa Wanainchi tulioahidiwa "mtaona bure".
Hata mawaziri wenye kasi wakifika hapo wanakula kona... hawaongei.....
 
TCRA ni chombo cha ovyo kabisa. Sijawahi kuwaelewa, kuwakubali wala kuwaamini katika hili. Niliwahi kuingia ndani sana katika hili, na afisa mmoja akaniambia hili jambo haliwezekani. Kwanini? Kuna mgongano wa kimaslahi.

Watanzania tupambane tu na hali zetu.
 
Kazi ya Tcra ni kuwaonya wapiga picha nusu utupu wa Bongo mavi na Ubongo wa Fleva. Shubaamiti.
 
Maxence Melo nisaidie kupeleka uzi huu jukwaa la habari na hoja mchanganyiko ikibiti naomba uupin mpaka watimize ahadi yao. Tunalipishwa local channels.
 
Channel hizo za local zikionyeshwa bure hakuna tena biashara maana akuna mtu atalipia vifurushi itakua ni mwanzo ya biashara kudoda na wengine kufunga makampuni
 
Back
Top Bottom