Serikali imemshindwa Kakobe? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali imemshindwa Kakobe?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mateso, Feb 12, 2010.

 1. Mateso

  Mateso JF-Expert Member

  #1
  Feb 12, 2010
  Joined: Aug 6, 2008
  Messages: 259
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Awali ya yote ningependa kutoa salamu kwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kwa kuweza kukaa kimya na kuangalia nguvu kazi kubwa ikiwa inapotelea barabarani mbele ya kanisa la Kakobe.

  Hivi anawaonea haya au anashindwa kuelewa ya kwamba kuna sheria ya nguvu kazi? Ningelikuwa mimi wote hao wangekuwa keko au segerea kwa uzururaji na uzembe. Wanaacha kufanyakazi jioni wanakuwa ombaomba. Hilo namwachia mkuu wa Mkoa.

  Jambo lingine ni hili la huyu mwenye hilo jumba wanapokaa hao wazururaji na wabomoa uchumi wa taifa letu. Hivi huyu anataka kuiweka serikali mfukoni au vipi?

  Nashindwa kuelewa mtu wa kawaida namna hii anakataa kukutana na waziri kuhusu kaswala kadogo anataka aonane na Mkulu ili azuie umeme unaohitajika kutumiwa na mamilioni ya wananchi kwa ajili ya uchumi wa taifa letu usipite mbele ya kitega uchumi chake. Nauliza huyu ni nani hata awe na confidence la namna hiyo? Sasa kwa mamalaka ninayojipa mwenyewe namwagiza waziri anayehusika atumie mamlaka aliyo nayo kisheria apitishe umeme hapo chini ya ulinzi wa FFU na gari la washa washa.

  Kwanza siamini kama huo mjumba umefuata taratibu zote za mipango miji katika ujenzi kwa sababu naona liko barabarani sana. Pamoja na yote hayo, kwani ni lazima ibada zifanyike barabarani? Kwa nini asiende mbali kama mzee wa upako na hao kondoo zake wakamfuata huko huko? Kama waziri atashindwa kufuata agizo langu nitamwomba mkulu atumie uwezo wake wa kisheria wa kuirudisha ardhi ya eneo hilo mikononi mwa serikali. I think that will be a lesser evel than infringing the right of millions of people to get reliable power.

  Mkulu tumempa dhana ya ardhi yote hivyo tunatanguliza ombi letu kama huyo mdogo wako uliyempa mamlaka atashindwa tumia dhamana tuliyokupa kurudisha hiyo ardhi mikononi mwa serikali.

  MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WALAANI WALE WANAOTEGEA KAZI NA KUSHINDA BARABARANI WAKIZUIA MAENDELEO YA TAIFA. WASAIDIE WAKUMBUKE KUWA MAANDIKO YANASEMA KUWA MAMLAKA ZOTE HUTOKA KWA MUNGU HIVYO WAZIHESHIMU PAMOJA NA MAAMUZI YOA.​
   
 2. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #2
  Feb 12, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,437
  Likes Received: 380
  Trophy Points: 180
  Fikiria watu na si mtu mmoja pekee. watakaoathirika ni wengi na hii miradi ya kulipuka lipuka bila plan endelevu matokeo yake ndo haya. pia ndo muone uchungu wa pesa za misaada. wahisani wnatoa pesa na amri nyuma yake.

  Cha msingi na mbolea ni kutafuta nanmna nyingine ya kupitisha huo msongo. kwa nini wasipitishe kati kati ya tuta la barabara maana wameresevu nafasi kubwa ya kutosha kati kati na ni ardhi ya serikali. mbona wanataka kuwa kama wachaga hii serikali yetu???? hawaridhiki???????????
   
 3. Ng'azagala

  Ng'azagala JF-Expert Member

  #3
  Feb 12, 2010
  Joined: Jun 7, 2008
  Messages: 1,277
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Mkuu msanii - heshima mbele
  mradi si wa kuripukaripuka kama wengi wanavyofikiria, vipimo vyote vilishafanyika chini ya wale wajapani (hata mie nilishiriki mwanzoni kabisa mwa mwaka 2007 katika upimaji ule kutoka tanesco makao makuu mpaka victoria. pale kwa Kakobe hapawezi kuwa na tatizo kwani nyaya zinapita kwenye hifadhi ya barabara na si kwenye eneo lake. yeye (kakobe) hapaswi kutumia eneo la nje ya geti kwani ni eneo la public. eneo lake ni ndani ya geti.
  jamani msitetee tu huyu kakobe ana wataalamu gani? kama si muhuni tu
   
 4. Ng'azagala

  Ng'azagala JF-Expert Member

  #4
  Feb 12, 2010
  Joined: Jun 7, 2008
  Messages: 1,277
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  [​IMG]

  Source: globalpublisherstz.com

  hizi data alizotoa Kakobe hapa ni feki kabisa. mtu hata usiye mtaalamu nenda kasimame kwenye nguzo pale karibu na dispensary ya Edward Michaud (karibu na keepleft /kakobe) na itizame nguzo nyingine pale kwenye junction ya kuingia moli/meeda bar utaona tu kuwa umeme unapita mbali na ukuta wake. hizo nguzo mbili ndiyo zitabeba ule umeme. hapo aliposema unapita overhead kwenye gate 1 ni uongo kabisa.

  anawakaanga wale waumini wake bure ili kupitisha agenda zake feki. tunaomba mkuu wa Mkoa aingilie kati awatimue wale wananchi waende wakafanye kazi.
   
 5. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #5
  Feb 12, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,639
  Likes Received: 23,834
  Trophy Points: 280
  Askofu Mkuu Zakaria Kakobe is powerful, the man has powers from wherever he got them, be devine or devil does not matter what matters he has the powers!

  Jana nimemsikia kwenye media akigomea kushiriki kwenye EIA kwa kusema wameshapanga matokeo!/

  Askofu Mkuu ana lake jambo, anataka kupractice powers ili kuvuna waumini. Anaiprovoke Tanesco, serikali na jeshi la polisi ili hatua zozote zikichukuliwa dhidi yake, atumie powers zake kuonyesha who is mightier, hivyo kuvuna waumini.

  Kuanzia mwaka huu tunahamia kwenye Digital Broadcasting, hivyo hakuna cha interfiarance, TCRA wafuatwe watoe statement, Askofu afunge mdomo, umeme upite!.
   
 6. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #6
  Feb 13, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 12,076
  Likes Received: 4,450
  Trophy Points: 280
  Nilikuwa nakutafuta wewe unayejifanya ulifanya huo mradi.

  Risk assessment mlifanya?
  EIA mlifanya?
  Public engagement ilikuwa ya aina gani?
  je walisaini ??


  Kama hamkufanya hayo hapo juu, basi hiyo hela ya Japan inarudi kwao; International standard za kufanya hiyo miradi ni lazima jamii husika iwe engaged na wasaini. Huu ndio utaratibu wa kisasa. Hii inasaidia

  1, Miradi yote isiyo salama kwa jamii inakuwa evaluated na kama kuna jambo litatokea wahusika wanatakiwa kuwalipa jamii

  2. Kuna miradi -mfano asbestos imeacha makovu na watu wanateseka kwa kansa mpaka leo

  3. Kuepeuka hatari ya wajanja wachache kujineemesha, kwa mfano huo umeme unawezekana ukawana unaenda kwenye kiwanda kimoja tu! raia wengine wakaonekana wananufaika kumbe uongo

  Faida za ku-engage public

  1. Project inarun -smooth, mfano

  leo hii mna schedule, fund, timeline, n.k pengine mmeingia mkataba na wataalamu muwalipe kwa kazi ya mwaka mmoja, je hujaona kitendo kilichotokea sasa kimeleta hasara sana?


  Mifano mingine Tanzania

  Migodi mingi imeanzishwa kwa mtindo kama mnaoutaka kuutumia, leo hii wakazi wa maeneo hayo hawana say, hawana mkataba, tatizo likitokea hakuna wa kumuuliza, watu walifukiwa n.k

  All in all, Kilichofanywa na Tanesco was total unprofessional way ya kuendesha miradi kama hiyo

  Kakobe utamlaumu, sisi wengine tunaangalia nani alitakiwa kufanya nini hapo kwanza. Mlikosea mnaweza kutafuta wataalamu wa risk analysis wakawapiga lecture.

  Na inaonekana kabisa kwa post zako hizi bado huko dunia ya nne! mlichofanya kimepitwa na wakati ningekutolea mifano mingi duniani ujue dunia iko wapi sasa!!

  halafu kesho unageuka na kulaumu wawekezaji migodini, kumbe na wewe unafanya the same kwa jina la umeme!
   
 7. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #7
  Feb 13, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 12,076
  Likes Received: 4,450
  Trophy Points: 280
  sikusoma hii post naona imeingia wakati naandika.

  ebu nijuvye, ina maana EIA kumbe kweli haikufanyika? my God!! nimetoka kumweleza jamaa hapo juu. Kwa hiyo kuna watu walitaka fukia fukia tu??

  Huu mradi unaingia kwenye case studies!

  kuna ndugu hapo juu amesema FFU, FFU haitawezekana, TANESCO kama walishakosea basi gharama zake ni kubwa kuzilipa, yaani kwa hali ilivyo hata Kakowb akikataa anashinda! wenye fedha watachukua fedha yao

  watakachofaya serikali ni kwendanaye hivyo hivyo!!

  My company is doing lots of EIA kwenye migodi na power lines. NI LAZIMA sio ombi!!
   
 8. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #8
  Feb 13, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,639
  Likes Received: 23,834
  Trophy Points: 280
  Waberoya, EIA, ilihafanywa na matokeo yapo, na Kakobe through his powers ameshayajua na kakataa kwenda kuyapokea.

  The rest ni practice of powers!.
   
 9. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #9
  Feb 13, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 12,076
  Likes Received: 4,450
  Trophy Points: 280
  EIA kufanywa sio tatizo swala je ilifanyajwe?

  EIA gani ambayo wahusika hawakuweka sign? na kueleweshwa mradi?

  migodi yote Tz ukienda EIA ipo, huwa wanaacha makudusi component ya risk assessment, na katika hiyo jamii husika lazima waweke sign kama wanakubaliana nao. Sio lazima awe kakobe maana katika jamii husika wanaweza wakawepo representative

  I am telling and I repeat kama EIA haikufanywa ku-meet standard hakuna atakayemgusa Kakobe tena ikiwa fedha ni ya donors.

  Sitting power nuclear plants, industry, dispose harzadous waste, power transmission, telecommunication etc vyote vinahitaji EIA inayo-engage public husika. This how the world operates now! Tanzania not exception
  Ingekuwa fedha zetu, nakuambia jamaa angekuwa ameshavamiwa siku nyingi, lakini hii , I doubt kuna tatizo kubwa utalisikia!

  Pasco this is the case in almost big mines, there was no public engagement na tumezoea ubabe! This fund will surely follow Japan's standard. So when people blame Kakobe in this very issue is another way of endorsing what is going on in our big mines!!!!!!
   
 10. Jituoriginal

  Jituoriginal JF-Expert Member

  #10
  Feb 13, 2010
  Joined: Feb 8, 2010
  Messages: 362
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  wachangiaji wote za mada hii,wamejaa mawazo mgando, na chuki binafsi juu ya walokole,na wakristo ingekuwa msikiti usingeguswa.Tz tunahitaji Crusade erra @wakristo tuungane kupigania haki yetu.waislaam wanafanya kuwa awamu ya nne ni yao.kakobe tuko nyuma yako.Umeme wao wakapitishie kwenye paa la ofisi zao za kufanyia ufisadi Ubungo.Mungu ibariki Tz.Mungu baliki walokole,na wakristo wote wanaotengwa na kunyanyaswa na serikari yao.
   
 11. Ng'azagala

  Ng'azagala JF-Expert Member

  #11
  Feb 15, 2010
  Joined: Jun 7, 2008
  Messages: 1,277
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Mkuu Waberoya heshima mbele. tuliza mzuka, taratibu,
  kitu unachopaswa kujua hapa ni kuwa hiyo project inafanyika kwenye ROW (mali ya serikali), na si katika kiwanja cha Kakobe. na project hii ya Umeme si ya kwanza, kuna nyaya ngapi zimejengwa toka Kidatu/mtela/ nk? zimezagaa kila sehemu na ni nchi zima?

  hivi unafahamu beacon za kiwanja chake(kanisa) zipo wapi na wapi? na je sheria ya ujenzi (building permit) inasemaje? ajenge kiasi gani ndani ya kiwanja chake?
  kama hizi taratibu zingefuatwa hili tatizo halingekuwepo. yeye analipigania eneo la nje ya kiwanja chake ambalo hapaswi kulitumia (pale wanapokaa waumini na penye mabango makubwa ni eneo la barabara).
   
 12. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #12
  Feb 15, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,834
  Likes Received: 249
  Trophy Points: 180
  Mkuu,

  Mbona unaingia jamvini na "comments" za "kishetani"?

   
 13. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #13
  Feb 15, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,561
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  ndugu askofu si mtu mdogo kama unavyotamka ni mtu mkubwa kuliko hata huyo waziri kwenye ulimwengu wa roho waziri anatakiwa amfate askofu ofisini kwake alafu tuache ushabiki wa kisiasa askofu wanachokitetea au kupinga ni haki kabisa na kinamadhara vinginevyo wasingepinga mabona barabara ilipopitishwa awakupinga na umeme walitaka kupitisha eeneo la udsm waligoma na wakaamua kuvusha fasta kwa askofu
   
 14. Mfamaji

  Mfamaji JF-Expert Member

  #14
  Feb 15, 2010
  Joined: Nov 6, 2007
  Messages: 6,572
  Likes Received: 619
  Trophy Points: 280
  Such a statement is too low for a member like you. Anyway , jina lako linamailza yote . MSANII
   
 15. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #15
  Feb 15, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,565
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu Ng'azagala unaongea mambo ya Msingi sana, na hii inatokana na Ukweli kwamba ubatumia Profession kufanya argument, mimi nimeuilza sana na sijajibiwa narudia tena kuuliza

  1: Huo umeme unaoleta Mgogoro ni wa Kv ngapi?
  2: Unapita underground au Kuna nguzo?
  3: Je Ule umeme unaotoka kidato na Mtera ambao unakuja kuwasha Tv na Redio
  zetu dar hauna madhara kwa paa za nyumba unakokatiza?
   
 16. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #16
  Feb 15, 2010
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,565
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Nikikuuliza nipe uthibisho wa Ulichokiandiak utasema Askofu Kasema! Wasomi wetu bana LoL!
   
 17. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #17
  Feb 15, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 36,019
  Likes Received: 6,831
  Trophy Points: 280
  Serikali imeshindwa na mafisadi ije kuwa
  kwa
  mwana wa mungu !!!!moto ule
   
 18. Kaka Sam

  Kaka Sam JF-Expert Member

  #18
  Feb 15, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 543
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mateso,

  ni sheria ipi ya nguvu kazi unayosema??? mi naona ni upuuzi mtupu, ningekuoti ulosema ila sitaki na mimi kuwa mpuuzi.
  je unajua maana ya mzuraraji, au unaropoka tu!!! kama ni mzima usiongee vitu bila ya documents!!
  narudi....
   
 19. M

  Magezi JF-Expert Member

  #19
  Feb 15, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,919
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  kakobe kaisha ona Kikwete hana msimamo ndo maana anavimbisha misuli yake na kuwapotosha walala hoi wanashinda pale juani utafikiri hawana kazi za kufanya. Kwanza wangekamatwa kwa uzururaji kwa sababu hawafanyi kazi.
   
 20. M

  Magezi JF-Expert Member

  #20
  Feb 15, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,919
  Likes Received: 163
  Trophy Points: 160
  kakobe hana tofauti na kibwetere tu....acha kumpa sifa ambazo hana na serikali wakiamua kumtimua pale na kuvunja hilo kanisa lake inawezekana sema wanamstahi tu.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...