Serikali imemshindwa Kakobe?

Mkuu Ng'azagala unaongea mambo ya Msingi sana, na hii inatokana na Ukweli kwamba ubatumia Profession kufanya argument, mimi nimeuilza sana na sijajibiwa narudia tena kuuliza

1: Huo umeme unaoleta Mgogoro ni wa Kv ngapi?
2: Unapita underground au Kuna nguzo?
3: Je Ule umeme unaotoka kidato na Mtera ambao unakuja kuwasha Tv na Redio
zetu dar hauna madhara kwa paa za nyumba unakokatiza?

Mkuu siku zote za sakata hili uko wapi??
  1. ni 132KV
  2. ni kwenye nguzo
  3. unatokea Ubungo tanesco kwenda Victoria kwenye mini-sub station
 
Awali ya yote ningependa kutoa salamu kwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kwa kuweza kukaa kimya na kuangalia nguvu kazi kubwa ikiwa inapotelea barabarani mbele ya kanisa la Kakobe.​


Hivi anawaonea haya au anashindwa kuelewa ya kwamba kuna sheria ya nguvu kazi? Ningelikuwa mimi wote hao wangekuwa keko au segerea kwa uzururaji na uzembe. Wanaacha kufanyakazi jioni wanakuwa ombaomba. Hilo namwachia mkuu wa Mkoa.​

Jambo lingine ni hili la huyu mwenye hilo jumba wanapokaa hao wazururaji na wabomoa uchumi wa taifa letu. Hivi huyu anataka kuiweka serikali mfukoni au vipi?​

Nashindwa kuelewa mtu wa kawaida namna hii anakataa kukutana na waziri kuhusu kaswala kadogo anataka aonane na Mkulu ili azuie umeme unaohitajika kutumiwa na mamilioni ya wananchi kwa ajili ya uchumi wa taifa letu usipite mbele ya kitega uchumi chake. Nauliza huyu ni nani hata awe na confidence la namna hiyo? Sasa kwa mamalaka ninayojipa mwenyewe namwagiza waziri anayehusika atumie mamlaka aliyo nayo kisheria apitishe umeme hapo chini ya ulinzi wa FFU na gari la washa washa.​

Kwanza siamini kama huo mjumba umefuata taratibu zote za mipango miji katika ujenzi kwa sababu naona liko barabarani sana. Pamoja na yote hayo, kwani ni lazima ibada zifanyike barabarani? Kwa nini asiende mbali kama mzee wa upako na hao kondoo zake wakamfuata huko huko? Kama waziri atashindwa kufuata agizo langu nitamwomba mkulu atumie uwezo wake wa kisheria wa kuirudisha ardhi ya eneo hilo mikononi mwa serikali. I think that will be a lesser evel than infringing the right of millions of people to get reliable power.​

Mkulu tumempa dhana ya ardhi yote hivyo tunatanguliza ombi letu kama huyo mdogo wako uliyempa mamlaka atashindwa tumia dhamana tuliyokupa kurudisha hiyo ardhi mikononi mwa serikali.​


MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WALAANI WALE WANAOTEGEA KAZI NA KUSHINDA BARABARANI WAKIZUIA MAENDELEO YA TAIFA. WASAIDIE WAKUMBUKE KUWA MAANDIKO YANASEMA KUWA MAMLAKA ZOTE HUTOKA KWA MUNGU HIVYO WAZIHESHIMU PAMOJA NA MAAMUZI YOA.​

Hapo ndo tunamhitaji waziri kama Magufuli pale Nishati na madini.....huyu kakende wala asinge sumbua
 
Back
Top Bottom