Serikali imekamilisha uandaaji na uidhinishaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 Toleo la Mwaka 2023

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987
Bunge la 12 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania litaketi kwenye Mkutano wa 13, Kikao cha 4, leo Novemba 3, 2023 ambapo mambo kadhaa yatajadiliwa. Karibu kufuatilia kikao hiki.


Serikali imekamilisha uandaaji na uidhinishaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 Toleo la Mwaka 2023 na Mitaala katika ngazi ya Elimu ya Awali, Msingi, Sekondari na Mafunzo ya Ualimu kwa lengo la kufanya Elimu yetu iendane na wakati.

Mitaala iliyoboreshwa imezingatia mahitaji ya sasa ikiwa ni pamoja na kuweka msisitizo katika stadi za karne ya 21 ili kumjengea mhitimu stadi za Kuwasiliana, Kushirikiana, Ubunifu na Fikra tunduizi. Aidha, ratiba ya utekelezaji wake inatarajiwa kuanza rasmi mwezi Januari, 2024 na kukamilika mwaka 2027.

Haya yamebainishwa na Waziri wa Elimu wakati akijibu swali la Rose Cyprian Tweve, Mbunge wa viti maalumu aliyetaka kufahamu ni lini Serikali itabadili Mitaala ya Elimu ili Kwenda na na wakati.

Pia, kwa upande wa Elimu ya Kati na Elimu ya Juu, mapitio ya programu mbalimbali pia yanaendelea kwa lengo la kuifanya iendane na wakati, vipaumbele vya nchi na mahitaji ya soko la ajira. Kwa mfano, kwa upande wa Elimu ya Juu kupitia Mradi wa High Eduction for Economic Transformation (HEET) programu zaidi ya 300 zitahuishwa au kuanzishwa
 
Back
Top Bottom