Serikali Imejenga Vituo Maalum vya Urekebu na Ufundi Stadi ili Kuwasadia Wanaoathirika kwa Kutumia Dawa za Kulevya

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,899
944

WAZIRI JENISTER MHAGAMA - SERIKALI KUJENGA VITUO VYA MAFUNZO KWA WARAIBU DAWA ZA KULEVYA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge na Uratibu, Jenista Mhagama amesema Serikali imejenga vituo maalum vya urekebu na ufundi stadi ili kuwasadia vijana na wale wote wanaoathirika baada ya kutumia dawa za kulevya.

Ameyasema hayo leo bungeni Dodoma wakati akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu hali ya dawa za kulevya ya mwaka 2022 ambapo amesema kwa mujibu wa utafiti unaonesha uwepo wa kiwango kikubwa cha uzalishwaji na utumiaji wa bangi.

Waziri Mhagama amesema, kwa mwaka ujao wa fedha 2023/2024 Serikali imetenga bajeti ya TZS Bilioni 8.7 zitakazotumika kujenga vituo vya urekebu na ufundi stadi, vitakavyosaidia kubadilisha tabia za vijana wanaotumia dawa za kulevya.

“Vituo hivyo vitakuwa na kazi kubwa ya kuwaondoa kwenye matumizi ya dawa na kuwapa shunguli nyingine watakazotakiwa kuzifanya zitakazotokana na shughuli za ujuzi, ambazo watafundishwa kwenye vitu hivyo,” amefafanua.

xKHu7qmI.jpg
 
View attachment 2645711
Hii itakuwa nzuri sana endapo kama itashirikisha vyema wadau wa maendeleo.
Italeta ukombozi mkubwa kwa vijana wa Taifa letu
 
Back
Top Bottom