Serikali imeishiwa haina pesa za mishahara

Hasara

Senior Member
Dec 29, 2006
138
9
Serikali imepanga kupandisha mishahara mipya 20007/2008 ya watumishi wa umma kwa kiwango cha shilingi 5,000 mpaka 9,000 tu kwa kila mtumishi, wakati huo huo vyama vya wafanyakazi na watumishi wanajiandaa kwa mgomo mkali nchi nzima kwa muda usiyo julikama kutokana na ukali wa maisha ,mwanye habari nyeti zaidi aziweke hapa.

asanteni
 
Hawa wafanyakazi wa serikali ambao hawajalipwa miezi miwili ni wapi na wa aina gani? Maana kwenda miezi miwili bila kipato si mchezo...
 
Ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya!!!! Maisha bora kwa kila Mtanzania hayo!!! Halafu mnataka tuvute subira kwa miaka mitano kabla hatujaanza kuhoji ahadi mlizotuahidi Watanzania ziko wapi!!? Wadanganyika wanaendelea kuumia pamoja na kuongezeka makusanyo ya kodi hadi kufikia shilingi bilioni 250 kwa mwezi, kupata na kuanza kuchimba gas, kukaribisha "wachukuaji" kwenye sekta ya madini lakini bado hakuna ahueni!!!
 
kwani ile tume iliyoundwa na raisi ilikuwa inafanya kazi gani,au kama kuna mtu anayo ripoti yake atumwagie hapa.
Yasije kuwa yale ya kamati ya spika alipoamua kutumia busara zake
 
Mzee Wangu unajua wafanyakazi wa serikali hawajalipwa leo mwezi wa pili, sasa hiyo nyongeza inaongezewa wapi?

Hii ni kweli au unatania. kwa nini mishahara haijalipwa, kusubiri mishahara mipya au fedha hakuna?
 
Serikali haina hela ilikuwa inasubiri bajeti ipite kwanza, baada ya ku-overspend bajeti iliyopita, yaani jamani hata hizi nazo zinatakiwa kuwa data? Pleasee!
 
ile katuni ya ndege kwa kweli ina ukweli mkubwa sana. HIvi EL na wenzake walio kwenye ndege wana wasiwasi wa watu kukosa mishahara? Hawa watanzania waliomchagua JK kwa asilimia 80 kweli wanaweza kumgomea? Sikumbuki kati ya Mwinyi na Mkapa ni nani kati yao alikabiliwa na mgomo wa wafanyakazi mwaka wa pili wa utawala wake.. je yawezekana lile fungate limefikia kikomo chake?
 
Watumishi wa Umma Bongo hawana ubavu wa kugoma. Kwani wanaamini kuwa serikali haina pesa kama wanavyoambiwa na viongozi wetu wezi wakubwa wakiongozwa na boss wa BOT. Tusubiri na tuone kama kweli watagoma.
 
ile katuni ya ndege kwa kweli ina ukweli mkubwa sana. HIvi EL na wenzake walio kwenye ndege wana wasiwasi wa watu kukosa mishahara? Hawa watanzania waliomchagua JK kwa asilimia 80 kweli wanaweza kumgomea? Sikumbuki kati ya Mwinyi na Mkapa ni nani kati yao alikabiliwa na mgomo wa wafanyakazi mwaka wa pili wa utawala wake.. je yawezekana lile fungate limefikia kikomo chake?

Mi nadhani ujumbe wa katuni ulikuwa mzito kuliko hata makala! Sijui kama mori ungempanda kama inavyosemekana kama katuni isingeambatana na makala. For some reason I just can't get over it...everytime I look at it I burst out laughing.
 
Nifahamisheni SH. 5,000 mpaka 9,000 niongezeko la mishahara mipya kwa kila mtumishi wa umma au ni nauli ya dadala kwenda kazini? kaaaaza kweli kweli....
 
Cha ajabu ni kuwa wafanyakazi waaminifu wengi wao ni akina mama
wafanyakazi wanaoonewa wengi wao ni akina mama
kuchelewa kwa mishahara wanaoumia ni wakina mama
lakini tulipo kuwa tunataka kuwaelimisha kuhusu matumizi ya kura zao hasa tulipokuwa tunawaambia kuwa sura siyo sera wala uwajibikishaji waliyuona wengi wao wajinga. haya sasa
 
Nimepiga simu kwa baadhi ya washikaji bongo ambao wanafanya serikalini hawana habari. Sasa sijui ni wafanyakazi wa serikali ipi??? May be serikali za vijiji!!! MKJJ atakuwa na habari (JOKE)!!
 
Ni majungu tu- watu wanaropoka!
wote/wengi wamepata mshahara ya June- hata mie nimepata-by 28th June. Hata waalimu kule Kibondo na Mbozi wamepata!
Tuache majungu- ambae ana data za Wizara ambayo haijalipwa mishahara ya June- atoe data hapa!
 
Serikali imepanga kupandisha mishahara mipya 20007/2008 ya watumishi wa umma kwa kiwango cha shilingi 5,000 mpaka 9,000 tu kwa kila mtumishi, wakati huo huo vyama vya wafanyakazi na watumishi wanajiandaa kwa mgomo mkali nchi nzima kwa muda usiyo julikama kutokana na ukali wa maisha ,mwanye habari nyeti zaidi aziweke hapa.

asanteni

Hasara,

Hizi habari wewe umezipata wapi? au ni uzushi tu?
 
Back
Top Bottom