Serikali imefilisika? Mishahara January utata mtupu

Status
Not open for further replies.

SG8

JF-Expert Member
Dec 12, 2009
3,955
2,125
Waungwana hii sasa ni too much. Zile tetesi tulizoletewa hapa kwamba huenda mishahara ya miezi ya January na February itakuwa mgogoro sasa ni dhahiri. Mpaka muda huu kuna halmashauri hazijalipa mishahara kwa watumishi wake wengi wao wakiwa ni walimu ambao tumezoea kuona wakiwa kwenye foleni za NMB kuanzia tarehe 23.
Majibu ya kila halmashauri ni kuwa hazina haijatoa pesa kwa kipindi husika. Aidha kuna malalamiko kilakona juu ya kuchakachukliwa kwa waajiriwa wapya wa serikaliwengine toka Julai na walimu wapya wa juzi tu hawajalipwa subsistence allowance zao kwa kuwa hazina ambayo imekuwa ikisisitiza eti haitaki madeni safari hii imezikwamisha halmashauri nyingi.
Baadhi ya halmshauri zimejitahidi kuchakachua posho za walimu wake kwa kuwalipa 35000/= walimu graduate ambao wanatakiwa kupata 45000/=/65000/= per diem. Aidha wengine wamelipwa siku 3 hadi 5 badala ya 14 kama inavyostahili. Je hii ndio serikali inayojinasibu kwamba itamaliza matatizo ya watumishi? Je kwa mtindo huu wiwki ijayo kuna mtumishi atafanya kazi kwa bidii wakti salio halisomi sawaswa? Huu ni usanii mtupu na kwa hakina haya ni "maafa"
 
Mkuu ungetaja angalau halmashauri kadhaa ambazo hazijalipa mishahara hadi sasa
 
Pesa yote waliichukuwa ccm kwenye uchaguzi sasa mnategemea nini? Ufisadi wa Kikwete huo:roll:
 
Wakati wa kampeni wengi waipewa mishahara yao. Sasa wanalalamika nini? Si walikubali kuhongwa? Walifikiri fedha hizo zilitoka wapi? Wao ndo waliofanya nchi yetu isiwe na mabadiliko sasa wakome tu. Acha wapate shida ndo mwanzo tu. Ingefaa wakae hata miezi sita ili wasikie ushauri.
Kwanza hawana kazi, kazi kuzunguka zunguka na vifaili tu maofisini hakuna wanachofanya.
 
Mkuu ungetaja angalau halmashauri kadhaa ambazo hazijalipa mishahara hadi sasa
Mbeya Jiji, Songea wameshindwa kulipa subsistence, Kilolo wamechakachua posho za walimu, Halmshauri almost zote zinalalamikia ukame kwa kiwango ambacho hakijapata kutokea, hata taasisi zenye kawaida ya kulipa mishahara tarehe 18-hadi 23 safari hii wamelipa kuanzia 25
 
Wakati wa kampeni wengi waipewa mishahara yao. Sasa wanalalamika nini? Si walikubali kuhongwa? Walifikiri fedha hizo zilitoka wapi? Wao ndo waliofanya nchi yetu isiwe na mabadiliko sasa wakome tu. Acha wapate shida ndo mwanzo tu. Ingefaa wakae hata miezi sita ili wasikie ushauri.
Kwanza hawana kazi, kazi kuzunguka zunguka na vifaili tu maofisini hakuna wanachofanya.

Mkuu Knock on Effect inatugusa wote... saa hizi TRA wamekuwa wagumu kweli..., kila ukiingiza mzigo nchini bei uliyoweka wanai-uplift na wataka ulipe zaidi mpaka uje kuwapa proof wiki imepita..., Mkuu hizo pesa zitalipwa, the sad thing ni kwamba ni mimi na wewe ndio tutazikohoa.... in one way or another
 
Nimeongea na mdogo wangu ni mwalimu yuko Biharamulo amenambia mishahara ilitoka jana ila c kawaida kwani ilichelewa sana.
 
Wakati wa kampeni wengi waipewa mishahara yao. Sasa wanalalamika nini? Si walikubali kuhongwa? Walifikiri fedha hizo zilitoka wapi? Wao ndo waliofanya nchi yetu isiwe na mabadiliko sasa wakome tu. Acha wapate shida ndo mwanzo tu. Ingefaa wakae hata miezi sita ili wasikie ushauri.
Kwanza hawana kazi, kazi kuzunguka zunguka na vifaili tu maofisini hakuna wanachofanya.

Unaishi wapi ndugu yangu nije nikupe mkono?
 
Hadithi ile ile....Tarehe 1 Oktoba mishahara ya Septemba haijalipwa, tunaelekea wapi? Afadhali utawala wa Hitler kuliko huu wa sasa
 
Gerradi vp kambi ya Adamu Aalima imeangamizwa au imenyanyuka maana nilisikia uchaguzi ulikuwa moto!pili kulikuwa na taarifa kuwa mkurugenzi wenu LIANA SIPORA alikataa kusaini PAY ROLL pamoja na kukabidhi ofisi hahahahaha hebu simulia kidogo.
 
Yule Mama kilaza kabisa. Sasa unakata kukabidhi ofisi utadhani ya kwako! Hawa ndio tulioambiwa wakiwezeshwa wanaweza. Si aondoke tu akawatumikie kina Maharage huko Tabora?
 
Hadithi ile ile....Tarehe 1 Oktoba mishahara ya Septemba haijalipwa, tunaelekea wapi? Afadhali utawala wa Hitler kuliko huu wa sasa

Wewe unazungumzia mshahara wa septemba, 2012. Mie (SIE) wafanyakazi wa Chuo kikuu kipya na kikubwa kuliko vyote Tanzania tunadai serikali SALARY ARREARS baada ya promotion tangu November 2010 hatujawahi lipwa hadi leo hii. Cha ajabu kingine hata annual increment hatupewi kwa mwaka wa pili sasa, hii ni haki ama kitu gani? Tumedai mno lakini hakuna la mafanikio, kweli serikali imefulia ama ina makusudi na maisha ya watu wengine?

Nina imani hakuna afsa wa serikali asiyefahamu madai ya wafanyakazi wa Chuo kikuu hicho kikubwa na kipya kilichoko kanda ya kati
 
Hilo la arrears hata mimi nadai za miaka minne iliyopita lakini swali la msingi liko palepale...Inapofikia tarehe 45 hakuna hata hako kamshahara kadogo maana yake tunaenda wapi? Madhara ya kuongozwa na Uamsho na Boko Haram
 
Kwani wewe upo idara gani kiongozi? Mbona napishana na walimu wakicheka tu hapa mitaani? Kuna majina ya watumishi wengi sana wamefyekwa kwenye payroll ya mwezi huu, usije kuwa mmoja wao
 
hivi mpaka leo serikali haijatoa mishahara kwa sababu gani hata watumishi wa serikali kuu hawana hela nyie mazungumzia wa halmashauri tu kilio ni kile kile
 
Kasi zaidi iyoooooooooooooooooo!
Kanga, kofia, fulana, vitenge, rushwa, alowance za makada wa CCM. Cha moto tutakiona. Ndio maana nimekwenda M4C.

Mmmesahau kuna uchaguzi CCM, hii ni kawaida kwa vipindi kama hivi.
 
Hawa walimu mi nawashangaa sana pale wanapotumika kama dodoki ama dekio particulary during the election, waache wafe kwa nja.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom