Serikali imefilisika? Mishahara January utata mtupu

Status
Not open for further replies.
Hawa walimu mi nawashangaa sana pale wanapotumika kama dodoki ama dekio particulary during the election, waache wafe kwa nja.

Chitemo, jifunze kuelewa. Hakuna mahali katika kile kinachotokea Mwezi Oktoba pametajwa waalimu. Hilo ni lako. Hata huyo aliyeko UDOM hajasema yeye ni mwalimu, vinginevyo umekariri wafanyakazi wote wa Chuo Kikuu ni waalimu (nina wasiwasi siku moja utatuambia wanaofanya kazi Hospitali ni madaktari na manesi).

Kama utaanzia mada mwanzoni kabisa ni kuwa mishahara ya January ilichelewa. Waalimu waliotajwa ni miongöni mwa waajiriwa wapya, hiyo ikimaanisha wakati wa uchaguzi 2010 hawakuwa wafanyakazi waserikali hata wahusishwe katika shughuli za Uchaguzi Mkuu.

Kinachojadiliwa ni uzembe wa Serikali kushindwa kuwalipa mishahara wafanyakazi wake katika muda muafaka. Ama yamkini kuchelewa huko kunaweza kuwa ni dalili mbaya ya tatizo lilipo ndani ya Serikali yaani Kufilisika

Jadili hoja acha malumbano, ufafanuzi huo unatosha.
 
Jamani mbona mwaongea kwa hasira? Ni kweli hamjalipwa hadi leo? Mbona wenzenu tunawaona wanafanya fujo tu kwenye mabaa?
 
hivi mpaka leo serikali haijatoa mishahara kwa sababu gani hata watumishi wa serikali kuu hawana hela nyie mazungumzia wa halmashauri tu kilio ni kile kile

Makubwa!!! Ninavyokumbuka kuna mwongozo wa serikali unaosema mishahara yote ya serikali italipwa ifikapo tarehe 25 ya kila mwezi. Hivyo, kama ni kweli watumishi hawajalipwa, kuna ucheleweshaji wa siku sita. Je viongozi wa idara za utawala wametoa maelezo yoyote kuhusu huu ucheleweshaji wa mshahara huko kwenye halmashauri au kwenye wizara???
 
Hilo la arrears hata mimi nadai za miaka minne iliyopita lakini swali la msingi liko palepale...Inapofikia tarehe 45 hakuna hata hako kamshahara kadogo maana yake tunaenda wapi? Madhara ya kuongozwa na Uamsho na Boko Haram

ulitaka tuongozwe na LRA au jeshi la wokovu?
Hapo ndo kilicho jificha ktk mioyo yenu kinapo dhihiri.
Kumbe tatizo ni imani ya anaetuongoza wala sio mfumo mzima wa nchi yetu.

Hata siku moja Mwenyezi Mungu hamfichi mnafik, atamdhihirisha tu. Mnayofanya yatawarudi hapahapa duniani, subirini muone.
 
Wewe dogo una matatizo gani? Mbona hautaki kuelewa? Wenzio wanalalamika hawajalipwa mishahara hadi leo, wewe unaleta mambo ya udini, SHAME ON YOU
 
MISHAHARA YA SERIKALI MPAKA LEO WATUMISHI WOTE HAWAJALIPWA NA HAKUNA MAELEZO YOYOTE..MWEZI WA SEPTEMBA......!! na mzee yuko majuuuu...!!
 
Inasikitisha sana Walimu walio chini ya katibu mkuu yaani Wakufunzi wa Vyuo vya Ualimu mpaka leo 01/10/2012, hawajapata mishahara ya mwezi wa Tisa (09).
 
Nimekatwa almost 2000 kwenye simbanking kucheki salio kama jamaa wameingiza, tar 1 mshahara haujatoka? ingekuwa july tungeelewa, hakuna jibu july ningeelewa. wamefuliaaaaa!
 
Mimi milidhani mimi tu niliye maternity leave sijaingiziwa kumbe ni wengi hawajapata.Wanatutesa kwa kweli
 
Wewe dogo una matatizo gani? Mbona hautaki kuelewa? Wenzio wanalalamika hawajalipwa mishahara hadi leo, wewe unaleta mambo ya udini, SHAME ON YOU

Huyu yeye alileta nini, ukabila au utaifa?
Tafakari, kisha chukua hatua.

quote_icon.png
By Gerrard

Hilo la arrears hata mimi nadai za miaka minne iliyopita lakini swali la msingi liko palepale...Inapofikia tarehe 45 hakuna hata hako kamshahara kadogo maana yake tunaenda wapi? Madhara ya kuongozwa na Uamsho na Boko Haram
 
tatizo ni hiyo system mpya inayoitwa epica 9 kutoa hela hazina imekua utata kwa hawa maakauntant wa wizara ila vumilia wakitoka training mshahara utaanza kuingia
 
Msiwe na wasiwasi, JK anapitisha bakuri hapa New York, then Canada. Unajua huu ndio muda wa "Thanx giving na X-Mas" unakaribia hivyo atapata tuu mishahara
 
Huyu yeye alileta nini, ukabila au utaifa?
Tafakari, kisha chukua hatua.

quote_icon.png
By Gerrard

Hilo la arrears hata mimi nadai za miaka minne iliyopita lakini swali la msingi liko palepale...Inapofikia tarehe 45 hakuna hata hako kamshahara kadogo maana yake tunaenda wapi? Madhara ya kuongozwa na Uamsho na Boko Haram
Okay, lakini si vizuri kuingiza malumbano ya udini wakati huu jamani, mnataka tuwe kama Nigeria, ama nchi nyingine zenye hali hiyo? TUSIFIKE HUKO WAKUU
 
Kuishi kwa kutegemea mshahara wa mwezi ni hatari sana ndugu zanguni. Hebu fikiria wakikukatia huo mshahara ghafla, maisha na familia yako yatakuaje?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom