Serikali imeamua kukarabati upya reli za zamani

Baada ya kufanya tathimini ya kweli serikali inabadili gia hewani. Huu mradi wa reli mpya SGR unawaumiza vichwa maana uwezo wa kifedha wa serikali kuifikisha reli mpya SGR hata Dodoma ni ngoma nzito.
Mkuu mradi wa SGR unaendelea vizur, mwisho wa mwaka huu awamu ya kwanza ya Dar- Moro itakua imekamilika
 
SGR bado ipo kama kawaida ila lengo la kukarabati reli ya zamani ni kuiongezea ubora hasa wa mataruma na chuma.
Ikumbukwe reli ya kati pekee ndio inatumika kusafirisha mizigo ya WFP
Kwann tunarukia reli za zaman wakati hii haijaanza na kuisha? Au ndio anaandaa mazingira ya kubadili gia angani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tusisahau pia kuyakarabati maisha ya watumishi wetu wa umma na wale wa sekta binafsi kwa kuwapa stahiki zao ikiwemo nyongeza zao za mishahara, kuwapandisha madaraja yao; kuboresha maisha ya wakulima wetu kwa kuhakikisha tunawainua pale walipo kwa kuwapa ruzuku, kuwatafutia masoko, nk; kutengeneza mazingira rafiki kwa wafanyabiashara wetu ili waweze kulipa kodi kwa hiyari kwa kuwaondolea kodi korofi; kuwatafutia fursa za kujiajiri vijana wetu waliomaliza elimu za sekondari na vyuo ili kupunguza wimbi la ukosefu wa ajira kwa vijana, nk.

Nakumbushia tu ya kwamba maendeleo ni watu na vitu. Vinapokwenda vyote kwa pamoja, hakika kila mtu atakua ana furahia na kujivunia utanzania wake.
Kukarabati reli ni zaidi ya kukarabati watumishi wa umma. Bila usafiri mzuri na wa uhakika hata wangelipa kila mmoja sh milion 10 kwa mwezi ni bure.
 
Habari za wakati huu wanajukwaa?
Serikali ya awamu ya tano imeamua kulivalia njuga suala la uchukuzi. Serikali imeamua kufanya marekebisho ya reli za zamani na kuhakikisha zinafanya kazi kwa ufanisi.

  • Reli ya kati
  • Mbali na ujenzi wa standard gauge serikali imeamua kuikarabati reli ya zamani (metre gauge). Ukarabati huu utahusisha uondoaji wa kokoto, kuondoa mataruma ya chuma yote, kuondoa sehemu ya chuma cha reli chenye ubora hafifu au chakavu na kuweka chuma kipya. Pia mataruma yataondolewa kwa kua mengi yalikua yamepanuka na kuongea umbali kati ya chuma hadi chuma na hivyo treni kushindwa kwenda kwa kasi kubwa zaidi. Pia kubadili mataruma na chuma cha reli kutaiwezesha reli kubeba uzito mkubwa kwa ekseli moja.
  • Kazi ya ukarabati inaendelea.

  • Manufaa ya ukarabati
  • Baada ya ukarabati kukamilika treni itakua na uwezo wa kukimbia kwa mwendokasi wa kilometa 70 kwa saa badala ya 35 km/h ya hivi sasa. Moja ya sababu inayozuiua treni kukimbia kwa 70km/h ni kutofautiana kwa ubora wa chuma cha pua na kutofautiana kwa upana wa reli kutoka chuma kimoja na kingine.
  • Reli ya Tanga Arusha.
  • Serikali imeamua kuikarabati na kuifufua reli ya Tanga Arusha. Baada ya ukarabati serikali imepanga kuongeza reli kutoka Arusha hadi Mara ili kuruhusu mizigo kuelekea nchini Uganda kupitia ziwa Victoria.
  • Hatua za ukarabati imefikia pazuri, changamoto kubwa ni watu waliojenga kwenye hifadhi ya reli. Serikali imeshatoa notisi (notice) kwa waliovamia kuondoka kwa hiari. Kazi ya ukarabati bado inaendelea.

Hivi kwanini reli ya kati au sgr isiunganishwe na TAZARA ili kufanya network ya reli
Na connection ingefanyikia Mang'ula Morogoro au kwingine kwenye ukaribu
 
Kwann tunarukia reli za zaman wakati hii haijaanza na kuisha? Au ndio anaandaa mazingira ya kubadili gia angani?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapana mkuu reli ya zamani inakarabatiwa ili isaidie kusafirisha mizigo wakati reli ya SGR inaendelea kujengwa. Kuna shehena kubwa ya mizigo hasa WFP na kampuni nyingine.
Ikumbukwe kuwa reli mpya SGR na ya zamani (metre gauge) zitakua zinafanya kazi pamoja.
Pia shehena ya kujenga reli ya SGR hasa chuma kinabebwa kwa kutumia reli ya zamani
 
Kukarabati reli ni zaidi ya kukarabati watumishi wa umma. Bila usafiri mzuri na wa uhakika hata wangelipa kila mmoja sh milion 10 kwa mwezi ni bure.

Tamaa yangu ni kuona mambo yote yakifanyika kwa wakati mmoja kama ilivyokuwa enzi za JK. Maendeleo ya vitu na watu.

Kinyume na hivyo, tunaweza kuangukia kwenye uchumi kama ule wa Ethiopia siku za usoni! Maana wenzetu wamefanikwa kujenga miradi mikubwa mingi nchini mwao lakini jambo la kushangaza, kila siku wananchi wao wanakamatwa nchini mwetu, kwenye malori na kwenye vichaka kama wahamiaji haramu huku wakijaribu kukimbilia Afrika Kusini kutafuta maisha bora.
 
Hivi kwanini reli ya kati au sgr isiunganishwe na TAZARA ili kufanya network ya reli
Na connection ingefanyikia Mang'ula Morogoro au kwingine kwenye ukaribu
Yote yanawezekana lakini tunaangalia kipaumbele...reli ya zaman inaunganisha moja kwa moja taifa la Rwanda, Burundi na Congo kupitia bandari kavu ya Isaka.
Kwa sasa ni kuhakikisha Rwanda, Congo na Burundi wanatumia bandari ya Dar-es-salaam lakini ili tufanikiwe inabidi tuwe na usafiri wa uhakika na wa gharama nafuu.
Hilo la kuunganisha litafanyika mkuu, tusubiri awamu ya pili
 
Habari za wakati huu wanajukwaa?
Serikali ya awamu ya tano imeamua kulivalia njuga suala la uchukuzi. Serikali imeamua kufanya marekebisho ya reli za zamani na kuhakikisha zinafanya kazi kwa ufanisi.

  • Reli ya kati
  • Mbali na ujenzi wa standard gauge serikali imeamua kuikarabati reli ya zamani (metre gauge). Ukarabati huu utahusisha uondoaji wa kokoto, kuondoa mataruma ya chuma yote, kuondoa sehemu ya chuma cha reli chenye ubora hafifu au chakavu na kuweka chuma kipya. Pia mataruma yataondolewa kwa kua mengi yalikua yamepanuka na kuongea umbali kati ya chuma hadi chuma na hivyo treni kushindwa kwenda kwa kasi kubwa zaidi. Pia kubadili mataruma na chuma cha reli kutaiwezesha reli kubeba uzito mkubwa kwa ekseli moja.
  • Kazi ya ukarabati inaendelea.

  • Manufaa ya ukarabati
  • Baada ya ukarabati kukamilika treni itakua na uwezo wa kukimbia kwa mwendokasi wa kilometa 70 kwa saa badala ya 35 km/h ya hivi sasa. Moja ya sababu inayozuiua treni kukimbia kwa 70km/h ni kutofautiana kwa ubora wa chuma cha pua na kutofautiana kwa upana wa reli kutoka chuma kimoja na kingine.
  • Reli ya Tanga Arusha.
  • Serikali imeamua kuikarabati na kuifufua reli ya Tanga Arusha. Baada ya ukarabati serikali imepanga kuongeza reli kutoka Arusha hadi Mara ili kuruhusu mizigo kuelekea nchini Uganda kupitia ziwa Victoria.
  • Hatua za ukarabati imefikia pazuri, changamoto kubwa ni watu waliojenga kwenye hifadhi ya reli. Serikali imeshatoa notisi (notice) kwa waliovamia kuondoka kwa hiari. Kazi ya ukarabati bado inaendelea.

Mbona huo ni uamuzi wa siku nyingi na kazi zimeshaanza kitambo.
 
Baada ya kufanya tathimini ya kweli serikali inabadili gia hewani. Huu mradi wa reli mpya SGR unawaumiza vichwa maana uwezo wa kifedha wa serikali kuifikisha reli mpya SGR hata Dodoma ni ngoma nzito.
chadema ni watu wa kucharazwa bakora tu ili akili ziwakae sawa, hivi we huoni reli ya sgr inavo tandazwa? maendeleo ni hatua...kwa sasa serikali imeanza kuitandaza toka dar-moro, sasa mmehamisha magori eti haiwezi fika Dodoma, ikifika Dodoma mtahamishia magori mwanza kwamba nako haiwezi fika, chadema ni zero brain kabisa kuanzia mwenyekiti wenu hadi katibu mwenezi wa kijiji/mtaa
 
Mradi huu wa reli SGR, narudia kwa hali mbaya ya kiuchumi na serikali kukosa uwezo wa kifedha reli mpya ya SGR haiwezi kufika Dodoma.
 
Air Tanzania inaenda Mbeya kwa mbinde.
4 flights kwa wiki nzima za bombadier.
4x80 pax~320pax go and return.
(compare Fastjet 2flights EVERY DAY, 2x7x120pax~1680pax every week!)

TAZARA to Mbeya haimo kwenye ukarabati.
Kweli Kamwele anatusomesha namba.
Mkuu umepotea mida. Huko si mna raisi wenu? Poleni sana. Wewe ni mfuasi mzuri wa chama tawala. Umetokea kuwa “collateral damage” or casualty!
 
SGR bado ipo kama kawaida ila lengo la kukarabati reli ya zamani ni kuiongezea ubora hasa wa mataruma na chuma.
Ikumbukwe reli ya kati pekee ndio inatumika kusafirisha mizigo ya WFP

Lakini si World Bank waliotoa fedha za ukarabati wa reli hiyo, na kushawishi hiyo SGR isubiri. Mbona mpango huo hamuuzungumzii kama ndio unaoendesha ukarabati huo unaoendelea sasa?

Habari za Reli Arusha - Musoma naona ni stori tu za kujazia kama ilivyo kawaida. Sioni msukumo wowote juu ya hilo; na ndio maana hata taarifa iliyowekwa hapa ni kama imewekwa kujazia tu!

Vipi, Mpanda hamfiki?
 
Kinyume na hivyo, tunaweza kuangukia kwenye uchumi kama ule wa Ethiopia siku za usoni! Maana wenzetu wamefanikwa kujenga miradi mikubwa mingi nchini mwao lakini jambo la kushangaza, kila siku wananchi wao wanakamatwa nchini mwetu, kwenye malori na kwenye vichaka kama wahamiaji haramu huku wakijaribu kukimbilia Afrika Kusini kutafuta maisha bora.

Mkuu, Ethiopia wapo zaidi ya milioni 100 sasa hivi; na uchumi wao ulikuwa chini sana, tena sana. Kwa wingi wao huo, vijana kukimbia na kutafuta fursa zilipo sio jambo la kushangaza. Wewe angalia Nigeria kama mfano mwingine, na hata China yenyewe na India.

Kwa hiyo usitegemee kwamba Ethiopia wangeendeleza watu wao kwanza ili wasikimbilie nje, ndipo wajenge miundombinu yao.
Sasa hivi uchumi wao unakuwa kwa kasi kubwa, na viwanda vinajengwa kila mahali, kilimo wamekipa kipaumbele kinachostahili. Haya yote yataongeza fursa za ajira, lakini hayawezi kumaliza tatizo la vijana kusaka fursa kila sehemu wanayoweza kuipata duniani.
 
Habari za wakati huu wanajukwaa?
Serikali ya awamu ya tano imeamua kulivalia njuga suala la uchukuzi. Serikali imeamua kufanya marekebisho ya reli za zamani na kuhakikisha zinafanya kazi kwa ufanisi.

  • Reli ya kati
  • Mbali na ujenzi wa standard gauge serikali imeamua kuikarabati reli ya zamani (metre gauge). Ukarabati huu utahusisha uondoaji wa kokoto, kuondoa mataruma ya chuma yote, kuondoa sehemu ya chuma cha reli chenye ubora hafifu au chakavu na kuweka chuma kipya. Pia mataruma yataondolewa kwa kua mengi yalikua yamepanuka na kuongea umbali kati ya chuma hadi chuma na hivyo treni kushindwa kwenda kwa kasi kubwa zaidi. Pia kubadili mataruma na chuma cha reli kutaiwezesha reli kubeba uzito mkubwa kwa ekseli moja.
  • Kazi ya ukarabati inaendelea.

  • Manufaa ya ukarabati
  • Baada ya ukarabati kukamilika treni itakua na uwezo wa kukimbia kwa mwendokasi wa kilometa 70 kwa saa badala ya 35 km/h ya hivi sasa. Moja ya sababu inayozuiua treni kukimbia kwa 70km/h ni kutofautiana kwa ubora wa chuma cha pua na kutofautiana kwa upana wa reli kutoka chuma kimoja na kingine.
  • Reli ya Tanga Arusha.
  • Serikali imeamua kuikarabati na kuifufua reli ya Tanga Arusha. Baada ya ukarabati serikali imepanga kuongeza reli kutoka Arusha hadi Mara ili kuruhusu mizigo kuelekea nchini Uganda kupitia ziwa Victoria.
  • Hatua za ukarabati imefikia pazuri, changamoto kubwa ni watu waliojenga kwenye hifadhi ya reli. Serikali imeshatoa notisi (notice) kwa waliovamia kuondoka kwa hiari. Kazi ya ukarabati bado inaendelea.

Huu nao ni uongo mwingine wa hii serikali. Nabet hapa hadi 2025 hakuna reli itajengwa toka Aruaha kwenda Mara.
 
Ndoto mna
Baada ya kufanya tathimini ya kweli serikali inabadili gia hewani. Huu mradi wa reli mpya SGR unawaumiza vichwa maana uwezo wa kifedha wa serikali kuifikisha reli mpya SGR hata Dodoma ni ngoma nzito.

Ndoto mnazoota kamwe hazitotimia
 
Back
Top Bottom