Serikali ilipokosea katika madai ya madaktari | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali ilipokosea katika madai ya madaktari

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by hippocratessocrates, Jul 17, 2012.

 1. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #1
  Jul 17, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Nianze kusema kuwa mimi ni daktari, na ningependa kwa pamoja tusio madaktari na madaktari tujadiliane katika uzi huu, si kwa kuonyesha hisia (hasira,matusi,kejeli n.k), kupoteza muda, kupotosha madai na taarifa na bali kwa kuona mapungufu ya chanzo cha mgomo kabla ya kujadili madhara yake, ili wote kama watanzania(na wasio watanzania pia) kuliweka sawa hili na kulisaidia Taifa.

  MADAI NA UFAFANUZI:
  -Uwajibishwaji wa watendaji wakuu wa W/Afya
  Ufafanuzi: Kutokana na ubadhirifu uliothibitika, hatua za kinidhamu zilipaswa kufuatwa.

  -Uboreshwaji wa Huduma za Afya katika hospitali.
  Ufafanuzi: Upatikanaji wa vifaa kazi, madawa na mazingira ya Hospitali ili kutoa huduma stahiki wa wagonjwa. Yaani
  Upatikananji wa vitendea kazi:(machine za upimaji moyo, kifua, sukari, uzito, urefu n.k), Mashine za Oxygen, vifaa vya kuongezea maji na damu mwilini n.k .
  Upatikanaji wa nyenzo(Machine kama vile CT Scan, MRI, Mashine za mionzi yaani X-ray, mashine za matibabu yaani mionzi ya kutibu saratani)
  Mazingira-Kuongeza vitanda, mashuka, huduma za chakula kwa wagonjwa wasio na ndugu n.k

  -Posho ya kufanya kazi katika mazingira hatarishi (Risk allowance) 30% au Chanjo
  Ufafanuzi: Katika mazingira ya sasa ambapo unaweza kuambukizwa Kifua kikuu(TB), Homa ya Ini (Hepatitis), UKIMWI (HIV/AIDS) tunapaswa kujikinga dhidi ya magonjwa haya tunapokuwa tukitibu wagonjwa na hivyo ni vyema serikali kutoa chanjo au isipowezekana kutoa chanjo na itoe posho tajwa kujikinga, mfano chanjo ya Homa ya ini pekee kwa mwaka ni mara 3 na inagharimu 45,000 (30USD) kwa kila chanjo.

  -Posho ya kuitwa kazini(On call allowance)-5%
  Ufafanuzi: Kisheria(Sina uhakika na kifungu), Muda wa kuitwa kazini au katika kada/sekta nyingine huitwa “Overtime” ni asilimia tano(5%) ya mshahara na hivyo, sheria ifuatwe katika hili.

  -Posho ya kufanya kazi katika mazingira magumu(Hardship allowance)-40%
  Ufafanuzi: Si madaktari wote(yaani madaktari 1500) wafanyao kazi katika hospitali za serikali wanafanya kazi katika mazingira magumu bali, wachache hasa walio vijijini na hivyo, ili kuwapa motisha na kuonyesha njia ya motisha ili madaktari wasibaki mijini tu na hivyo kuwafanya waende vijijini ili kuepuka usumbufu wa wagonjwa kusafiri toka mkoahadi mkoa kwa matibabu, posho ya mazingira magumu itolewe kwa madaktari hawa walio vijijini na si wote.

  -Posho ya Usafiri(10%) au mkopo wa magari.
  Ufafanuzi: Kwa madaktari wale kukaa mbali na hospitali, wapatiwe posho hii au mkopo wa gari(NA PESA HII IKATWE KATIKA MSHAHARA). Hii ikiwa na maana daktari aliye zamu na anayeishi(mfano) bunju na kufanya kazi Muhimbili, au anayeishi Vikindu na kufanya kazi Amana, anayeishi kimara mwisho na kufanya kazi Temeke nk katika mikoa mingine anayetakiwa kufika usiku saa nane na hakuna usafiri anaweza kufika kwa wakati.

  -Posho ya makazi (30%) au kupatiwa nyumba.
  Ufafanuzi: Kisheria (“Doctor is equal to high government officer and is entitled to a house”).Nitapokuwa na vifungu vya sheria nitathibitisha hili. Na kwa kuwa jambo hili lipo kisheria basi na sheria ifuatwe(na ndio Seriakali ilisema inajenga nyumba 700 za madaktari), lakini isipowezekana kwa daktari kupatiwa nyumba(kwa ambao hawana) basi posho ya asilimia 30% itumike kama mbadala.

  -Wafanyakazi wote wa Sekta ya Afya wapewe kadi za kijani za bima ya Afya.
  Ufafanuzi: Kwa wafanyakazi wa sekta ya Afya yaani madaktari, wauguzi, wafamasia, watu wa maabara, nk. Wapewe bima za Afya wakipata huduma sawa na ile wanayotoa.

  -Pendekezo la mshahara kuwa mil. 3.5/=kwa mwezi.
  Ufafanuzi: Kama vile mishahara katika Serikali inavyotegemea
  *Muda wa masomo wa fani.
  *Kiwango cha elimu.
  *Ugumu wa masomo wa fani husika.
  *Ugumu wa kazi.
  *Muda unaotumika kazini.
  Hivyo kwa kuzingatia haya, pendekezo la mshahara tajwa utolewe kwa madaktari lakini kama ikishindikana basi Mwajiri(Seerikali) na itoe pendekezo lake.

  MAKOSA:
  Jumla ya madaktari wote katika hospitali zaSerikali ni 1500, hii ikiwa ni takwimu ya Wizara ya Afya yam waka 2011 na ikijumuisha zaidi ya madaktari 300 waliofukuzwa na 150 waliokwenda nje tayari hadi leo trh 17.07.2012. Hivyo tafsiri iliyotumika ni ;
  -Daktari hayuko entitled kupata nyumba kama high government official kama ilivyoainishwa kisheria
  -Daktari hatakiwi kulipwa overtime (call allowance)mara baada ya muda wa kazi kwa aslimia tano ya mshahara
  -Tafsiri ya kuwa madaktari wote huwa wanakuwa zamu za usiku (overtime) na hivyo kuwekakiasi cha posho tajwa juu kuwa ya madaktari wote na kila siku!
  -Tafsiri ya pesa ya mazingira magumu kwa madaktari wote(KWANI SI MADAKTARI WOTE WAKO MAZINGIRA MAGUMU YA VIJIJINI)
  -Tafsiri ya kutaka posho ya mazingira hatarishi pekee badala nyenzo za kujikinga na chanjo
  -Tafsiri kuwa wafanyakazi wengine wa sekta ya afya hawakujumuishwa katika madai.
  -Tafsiri ya pendekezo la mshahara tajwa kuwa ni SHURUTI ya kurudi kazini.
  -Tafsiri ya kuwa PENDEKEZO la mshahara haliwezi kupungua!
   
 2. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #2
  Jul 17, 2012
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,160
  Likes Received: 1,162
  Trophy Points: 280
  Selikalini hajabakiwa mtu mwenye hekima wala busara, wanasubiri msaada wa watu wa marekani kutatua mgogoro huu.
   
 3. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #3
  Jul 17, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,943
  Likes Received: 1,268
  Trophy Points: 280
  i tried to be a doctor and failed, sasa nawaheshimu tu!
   
 4. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #4
  Jul 17, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Hii mijadala bado inaendelea?

  Vipi hali ya Ulimboka? hajambo?
   
 5. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #5
  Jul 17, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,196
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Mkuu jikite kwenye hoja hiyo hapo juu suala la ulimboka halikuhusu tokea Jana unaulizia mbona sisi hatukuulizi kuhusu kugomea sensa
   
 6. C

  Chibenambebe Senior Member

  #6
  Jul 17, 2012
  Joined: Mar 27, 2012
  Messages: 148
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hali tutegemee kuwa mbaya zaidi kwa kipindi kifupi kijacho kwa sababu waliotangulia kuondoka hakika wamekwenda kuwaandalia wenzao makao hivyo wengi najua watafuata.
   
 7. RGforever

  RGforever JF-Expert Member

  #7
  Jul 17, 2012
  Joined: Apr 3, 2011
  Messages: 6,165
  Likes Received: 1,890
  Trophy Points: 280
  Inauma sana daktari anauwezo wa kumtibu mgonjwa halafu hana kifaa....
   
 8. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #8
  Jul 17, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Sijui na lile sakata la meli za iran kutumia bendera ya Tz likinuka serikali ndo itahamia wapi kuombaomba?
   
 9. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #9
  Jul 17, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,731
  Likes Received: 1,441
  Trophy Points: 280
  Hippo,
  Tuliwaelewa na kuwanunga mkono toka zamani tu. Hoja zenu nyingi zina mantiki na mashiko na serikali badala ya kujibu hoja kwa hoja ikaishia kwenye siasa mbuzi na vitisho.

  Kukosekana kwa daktari kunahatarisha afya na pengine kusababisha kifo, lakini je! kukosekana kwa mwanasiasa kuna madhara gani? Na nini tija yao (wanasiasa) ikiwa nchi imeuzwa, hali ya uchumi ni mbaya, dhuluma na ufisadi vimeongezeka?

  Yet they fetch 10m per month + unlawful allowances to icing their daylight robbery.

  I prefer to have doctors than silly politicians in my team
   
 10. J

  JF2050 JF-Expert Member

  #10
  Jul 17, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 2,086
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Madai yalieleweka na yanaeleweka. Sasa jinsi ulivyoandika hapo serikali haikuelewa nini? siasa uchwara wanazozifanya zitawatokea puani.
   
 11. M

  MWAKIKALI Member

  #11
  Jul 17, 2012
  Joined: Jun 8, 2012
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nchi nyingi zilipata ukombozi wa kweli baada ya uonevu wa kiwango cha juu kwa wananchi uliofanywa na serikali, ukisoma historia ya ufaransa na mfalme louis, baadhi ya nchi za kiarabu africa. Na tanzania uhuru wetu upo jirani zaidi ya ilivyotabiriwa. Thanx god, nimeishi kuuona ukombozi wa kweli wa taifa letu, nakupenda tanganyika.
   
 12. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #12
  Jul 17, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Sidhani kama kulikuwa na dai lisilo na umuhimu, kama pande zote mbili zingejishusha na kwa busara kubwa kutatua mgogoro kwa kusikiliza madai lakini kama tungejifunza "to priotize our priorities"..na katika hili huduma bora na za msingi zifanyiwe kazi kwa uharaka na kisha madai mengine..
   
 13. Makene

  Makene JF-Expert Member

  #13
  Jul 17, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,479
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  imesemwa kila mara kwa madai ya madaktari wao si wafanyakazi pekee.
  Hii ina maana tu iwapo serikari itathibitisha ya kwamba polisi wanalazimika kulinda maandamano kwa fimbo na si silaha za moto, walimu wanaweza kufundisha bila chalk,na kupima matokeo ya kazi yao bila mitihani kwa wanafunzi wao, hata wakulima wa jembe la mkono ndio wenye hali njema kiuchumi na wanaweza kulima bila mbolea na mbegu bora.
  Serikari haina uwezo wa kufilisika, kwa maana ya kuacha ufahari na kuweka matabaka.
  Serikari inatimiza andiko, mwenye hana hata kidogo alichonacho atanyanganywa.
   
 14. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #14
  Jul 18, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Mkuu Makene umenena, ni kweli wengi tunahalalisha ubaya kuendelea kutokea kwa sababu ya ubaya mwingine utaofanyika sehemu nyingine, kwa kusema tu madaktari si wanyakazi pekee na wakati toka uhuru hadi leo TZ yetu ina madaktari 1500 tena wengine wakiwa wamehamia na kuendelea kuhamia sekta binafsi, kuhama nchi na wengine wakifukuzwa..sijui kama hatuoni kama tunaleta chuki na kinyongo kwa wale wachache wanaobaki!
   
 15. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #15
  Jul 18, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Brain drain???
   
 16. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #16
  Jul 18, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  brain drain has peaked up,,,
   
 17. Medical Dictionary

  Medical Dictionary JF-Expert Member

  #17
  Jul 18, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 1,053
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Serekali haijui kwamba inafanya battle na the cream of tanzanian education..!
   
 18. Wanitakiani

  Wanitakiani JF-Expert Member

  #18
  Jul 18, 2012
  Joined: Apr 18, 2008
  Messages: 644
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Natamani Watanzania wote wangesoma huu uzi. Bahati mbaya wanasiasa wamewekeza kwa Watz wengi walio wajinga na wasio na upeo wa kupambanua mambo. Madai ya madaktari ni kwa ajili ya kuwanusuru watz wenzao lkni hoja imepotoshwa. Inasikitisha sana!
   
 19. b

  bdo JF-Expert Member

  #19
  Jul 19, 2012
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,711
  Likes Received: 1,611
  Trophy Points: 280
  unaumia sana maana hadi sasa hujasikia habari mbaya ya afya yake
   
 20. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #20
  Jul 19, 2012
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  dogo.... i am sure kuna wakati you read what you write or listen to your inner self and realize that you are sitting on a glass sofa

  jah bless your intelligence as time goes by....

  brotherly advice
   
Loading...