Serikali ilikosea - Mukama

Kidafani

Member
May 30, 2011
28
9
Katibu mkuu wa ccm, Wilson Mkama, amesema serikali ilikosea kutowapeleka katika mazoezi ya vitendo wanafunzi wa vyuo vikuu, kwa kuwa hiyo ni haki yao ya msingi. Mkama aliwaomba radhi wanafunzi hao kwa upungufu huo na kutaka waipe Serikali mwaka mmoja ili ibadili mfumo unatumika sasa.






Source: Mwananchi Jumapili, June 19 2011
 
Waipe serikali mwaka mmoja kwani yeye anafanya kazi ya serikali? Serikali ndio inatakiwa i-respond, sio chama.
 
Mwaka ni mwingi sana maana kuna watakaoendelea kuathirika ndani ya huo mwaka.

Mkama ni msaani anasema kama nani? kuomba mwaka mmoja wakati hayo yanatendeka alikuwa katibu mkuu wa serikali hakufanya lolote ataweza vipi wakati huu alipostaafu kazi serikalini?
 
Katibu mkuu wa ccm, Wilson Mkama, amesema serikali ilikosea kutowapeleka katika mazoezi ya vitendo wanafunzi wa vyuo vikuu, kwa kuwa hiyo ni haki yao ya msingi. Mkama aliwaomba radhi wanafunzi hao kwa upungufu huo na kutaka waipe Serikali mwaka mmoja ili ibadili mfumo unatumika sasa.






Source: Mwananchi Jumapili, June 19 2011

Katika mambo ya kiserikali, kila kosa linaendana na adhabu. Kama Mkama amekiri kuwa serikali ilikosea, ni lazima pia ataje adhabu sahihi iendayo na kosa hilo la serikali.
 
mkama kajibu bila kfikiria yeye adai serikali ipewe mwaka1 na wale wanafunzi nao waongezewe wasome miaka minne nin?ajibu ishu zake zakichama uko,nashinwa kuelewa siasa kwenye taaluma toka lini
 
Wanafunzi sasa hivi wamefukuzwa chuo, Chama cha Magamba kinaomba mwaka mmoja ili serikali yake ifanye marekebisho. Sasa ina maana hao wanafunzi wakae mitaani kwa mwaka mmoja wakisubiri Magamba wafanye marekebisho, hivi kweli anatumia ubongo au kamasi katika kutoa comments kwenye public? Kama kanuni za bunge ziliweza kubadilishwa in days wakati CHADEMA ilipothibitika kuwa ndio chama kinachotakiwa kuunda kambi ya upinzani bungeni, kwa nini suala la elimu kwa hawa vijana wasubiri mwaka mzima?
 
Wanafunzi walitoa kilio chao muda mrefu, yeye mkama, chama chake na serikali waliziba masikio wakadharau wakadai wanatumiwa na wapinzani. Hatimae wanafunzi wakagoma kuishinikiza serkali itambue umuhimu wa suala lao, wakafukuzwa. Siku zote hizo mkama alikuwepo tena kama katibu wa chama tawala. Inakuwaje ajue leo kuwa selrikali ilikosea? Kakumbushwa na nani? Huo mwaka ni wa kurekebisha nini? Kwani katika curriculum ya course yao hakuna kitu hicho?

Mkama aache ubabaishaji, aliyesababisha hayo yote anatakiwa kuwajibishwa na wanafunzi wapewe haki ya mara maoja.
 
Wabunge wa magamba si walikuwa wanasema chadema ndo wamechochea wanafunzi kugoma? Leo iweje huyu gamba jipya akiri serikali imeingia choo cha kike kuwafukuza madent wa udom? tangu lini amekuwa msemaji wa serikali? Tunataka kauli hii isemwe na serikali sio mjinga mmoja toka magamba aje aisemee serikali.
 
Anatakiwa waziri wa Elimu ndio aombe msamaha na siyo CCM. Mukama anaingilia Serikali badala ya kuisimamia. Ilikuwa inatakiwa Chama kimuite mkuu wa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi na kumpa maelekezo ya ama Serikali iombe radhi na hatua za kuchukua dhidi ya mru aliyeifikisha hapo serikali.
 
Back
Top Bottom