DOKEZO Serikali iko wapi masoko yanakuwa machafu kiasi hiki? Kipindupindu kitatuacha?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Yote na yote jamii pia inalo jukumu la kuimalisha usafi
Sio kila kitu selikali iwafanyie, Jamii sasa wao jukumu lao litakua lipi?
ingekuwa wewe ni mlipaji wa kodi usingeongea ujinga hapa,
hapo watu wanalipa ushuru kuna hela ya taka inatolewa kila mwezi ila tatizo ni viongozi wetu wengi wanawaza upigaji tu!
 
Hali ya masoko kwa kweli ni mbaya sana, yaani unaweza kununua bidhaa ukaharibu viatu na ukapata magonjwa mazingira ya masoko yetu. Kila mfanya biashara analipa ushuru wa kuwepo sokoni, hata hivyo inashindwa kubainika hela zinatumikaje? Mbona masoko machafu hadi yanatia kinyaa, na mengine hutoa harufu mbaya kabisa.

Leo nimetembelea soko la Tegeta Nyuki aisee, sijui kama kipindupindu kimetuacha au kinatuvutia kasi tu. Maeneo machafu hata kutembea ni shida. Angalia kama hali ya wauzaji matunda hapa na hayo maji machafu ya pembeni.

Fikiria uchafu huo halafu bado tupo comfortable kununua bidhaa bila kujali afya zetu. Mimi nadhani ni wakati kwa wafanyabiashara kudai matumizi ya fedha za ushuru zinazolipwa kila siku.

Kwa sasa kasi ya magonjwa yasiyoambukiza pia iko juu, kwa uchafu huu magonjwa ya upumuaji yanakosekanaje maana kutakuwa na hewa nzito mfanyabiashara anaivuta kutwa nzima.
Hebu angalia kama hapo, mtu unapitaje, yaani unatoka sokoni kama umetoka shamba miguu imechafuka matope matupu.

Ni kweli tumeshindwa kutumia hela za ushuru kutengeneza mitaro vizuri ili mvua zisilete athari kwa kiasi hiki cha kuhatarisha afya za watu.

Tunasubiri kupindupindu?
Mkuu tupo chini ya ccm na kodi tunalipa.
 
Hii mada ni muhimu sana mamlaka husika zichukue hatua,haya ndiyo mambo yanayoweza kuinua Taifa au kuliangamiza.Ni suala mtambuka yaani pana sana.
 
Hivi tunashindwa wapi waafrika? Akili tunazo,elimu ipoh na rasilimali watu ipo japo rasilimali pesa ni kidogo naamini tukiamus tunaweza na tulishaliweza enzi za mwendazake kipindi cha usafi kila jumamosi
 
Hali ya masoko kwa kweli ni mbaya sana, yaani unaweza kununua bidhaa ukaharibu viatu na ukapata magonjwa mazingira ya masoko yetu. Kila mfanya biashara analipa ushuru wa kuwepo sokoni, hata hivyo inashindwa kubainika hela zinatumikaje? Mbona masoko machafu hadi yanatia kinyaa, na mengine hutoa harufu mbaya kabisa.

Leo nimetembelea soko la Tegeta Nyuki aisee, sijui kama kipindupindu kimetuacha au kinatuvutia kasi tu. Maeneo machafu hata kutembea ni shida. Angalia kama hali ya wauzaji matunda hapa na hayo maji machafu ya pembeni.

Fikiria uchafu huo halafu bado tupo comfortable kununua bidhaa bila kujali afya zetu. Mimi nadhani ni wakati kwa wafanyabiashara kudai matumizi ya fedha za ushuru zinazolipwa kila siku.

Kwa sasa kasi ya magonjwa yasiyoambukiza pia iko juu, kwa uchafu huu magonjwa ya upumuaji yanakosekanaje maana kutakuwa na hewa nzito mfanyabiashara anaivuta kutwa nzima.
Hebu angalia kama hapo, mtu unapitaje, yaani unatoka sokoni kama umetoka shamba miguu imechafuka matope matupu.

Ni kweli tumeshindwa kutumia hela za ushuru kutengeneza mitaro vizuri ili mvua zisilete athari kwa kiasi hiki cha kuhatarisha afya za watu.

Tunasubiri kupindupindu?
Mkuu wa wilaya kashindwa kazi.

Hali inatisha.
 
ingekuwa wewe ni mlipaji wa kodi usingeongea ujinga hapa,
hapo watu wanalipa ushuru kuna hela ya taka inatolewa kila mwezi ila tatizo ni viongozi wetu wengi wanawaza upigaji tu!
Tulia wewe kwa wewe hupendi kulamba asali
 
Masoko si yana watu? Si yana uongozi? Kipindu pindu kikijia haitoharisha serikale ni wao ndio watahrisha maji ya mchele.. mana uchafu wao ndio wanautengeza na uko kwa wao. So hapo ni swala la kutumia akili tu...
 
Back
Top Bottom