Serikali ikajifunze toka St. Francis Sekondari Mbeya kuboresha ufaulu wa kidato cha nne

Kama ni hivyo basi upuuzi kulinganisha matokea ya pande hizi mbili

Sent using Jamii Forums mobile app
Upuuzi kivipi wakati kila mtu anafanya sehemu yake...angalia racing zilivyo, mshindi hupatikana kwa kushinda racing na siyo kushiriki racing! Haijalishi we ni mnene au mwembamba, kama we ni mshindi unapewa ushindi wako, vivyo hivyo kwa aspects zingine!

Shule za kata zinashiriki kusajili wanafunzi ila za private ni kutoa elimu inayomjenga mwanafunzi kwenye nyanja zote!
 
Lazima na Muhimu tuwawekee mbadala wale wenye vichwa "nunda" kama mimi in case wameonekana kufeli sio bora liende

Sent using Jamii Forums mobile app
kwanz naamini wewe haupo hivyo maana naona jinsi unavyoweza kuandika kitu kikaeleweka... Turudi kwenye mada, elimu sio option pekee kwenye maisha sio ni heri mtu akapunguzwa mapema kuliko kumfosia mazingira aje aaibike mbele maana unakuta kichwa yake haipo kwenye elimu kwa hiyo utapiga utaua na mwisho wa siku utapoteza muda for nothing

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Suala la mtoto kutojua kusoma na kuandika mzazi hakwepi lawama iweje mwanao aanze darasa la 1 hadi afike labda darasa la 3 haujawahi kumkagua au kumpa mazoezi ya kuandika ukiwa nae?

 
Hoja yako ya msingi lakini unasahau kwamba mchujo wa Tabora boys na Iliboru ni wa mara moja yaani darasa la saba tu.Huko kwingine ni mchujo endelevu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa mkuu unachotaka useme kwamba st francis wawe na uwezo wa kumuwekea mtu karama ambayo Mungu hajampa?
Yani wasichuje watu hata kama mwanafunzi haelewi chochote kuhusu shule au kama ndo hawa wa kuanza kuruka ukuta kwenda disko bado wamshikilie tu wawe wanaendelea kumfundisha??
Hauko fair mkuu na ndio maana nilisema toka mwanzo kuwa tatizo moja wapo la serikali na hizi shule za kata ni kulazimisha kila mtu asome, hiki ndio chanzo cha ongezeko la zero form 4. Yaani wale walio feli la saba tumeamua tuwaongezee muda wa kukaa shuleni ila tuna uhakika tu watafeli form 4


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Suala la mtoto kutojua kusoma na kuandika mzazi hakwepi lawama iweje mwanao aanze darasa la 1 hadi afike labda darasa la 3 haujawahi kumkagua au kumpa mazoezi ya kuandika ukiwa nae?
Hii ni Hoja kabisa!

Mzazi hana muda wa kukagua maendeleo ya kitaaluma ya mtoto wake...

Mzazi muda wote yuko bize na mipango ya kuzaliana na kutafuta pesa, ila swala elimu hataki kutilia mkazo, anaachia walimu tu...

Inapofikia mtoto anazidisha Ukilaza, anatupia lawama walimu na serikali kumbe yeye kama yeye angetakiwa afanye sehemu yake!
 
Kumbe hapo hata wazazi wa watoto ambao wapi st francis nao wana mchango kwenye ufaulu wa watoto wao,?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mazingira ya ile shule ukifika na wewe utatamani binti yako akasome pale, jiulize je mwanao anauwezo wa kushindana na wenziye? Wazazi wengi wanatamani watoto wao wakasome shule kama ile lakini wanakosea kutowasimamia vizuri wakiwa shule ya msingi, wanategemea walimu ndio wawe wasimamizi wa watoto wao
 

Wazazi wengi waliopo kwenye mini mikubwa kama Dar, Mwanza nk wanajiona wako bize na kutafuta pesa kuliko kufuatilia maendeleo ya watoto wao, Nina mifano kadhaa ya ndugu zangu
 
Upo huo mchango!

Sasa hawa wazazi wa kata kutwa ulabu tuu, atawaza saa ngapi maendeleo ya kitaaluma ya mtoto kama kichwani ni Balimi tu muda wote inaamua mambo!
Naam mkuu
yaani matokeo ya hawa watoto ni team work ndo mana yana meremeta kweli kweli.
Shule zetu hizi hata mtoto akifaulu yani ni effort yale mwenyew anakufa kishujaa

Kuna wazazi hawajui hata watoto wao wapi vidato vya ngapi ila nao wanaomba neema watoto wafaulu tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yani kwa mikakati kama ile hata mimi au wewe tukianzisha shule ndani ya miaka mitano ikisimamiwa vizuri basi lazima tutaambiwa tunafundisha watoto wa vigogo


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yani kwa mikakati kama ile hata mimi au wewe tukianzisha shule ndani ya miaka mitano ikisimamiwa vizuri basi lazima tutaambiwa tunafundisha watoto wa vigogo


Sent using Jamii Forums mobile app

Hahaaa! Watu wamejaribu kauanzisha shule na kuweka mikakati, ila wameshindwa kutengeneza jina kutokana na watoto wanaowapata wanataka kudekezwa, kulishwa chips, kuku, darasani umbembeleze, vitu ambavyo kule St Francis huvikuti
 
We jamaa kupata kwako zero ndo uanataka na wenzio wapate..kubali tu wewe ni kilaza basi..acha wenye shule zao wapige shule..elimu ndo mtaji wa kudumu..ebu niambie wangapi kati ya hao vilaza wenzako mliofeli la saba..mpo kariakoo mna uza hivyo vifaa vya electroniks..bado kwa upompoma wako ukiugu utaend kutibiwa na hao waliopata one...boya kabisa ww..jitahidi utumie akili mara moja moja...kamwe usidharau elimu.

#MaendeleoHayanaChama
Ujinga unapata A 10 unakuja kuwa muhasibu wa halmashauri mshahara laki 5,si bora wanaopata zero wamejiajiri kwenye uuzaji wa electronics kariakoo na magomeni

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Swadakta mkuu


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unapigana na ukuta.Geuza hoja yako iwe hivi; hizo private schools zisichuje ziwe zinasomba vichwa vyovyote tu halafu wapate Div 1 darasa zima tuone!

Sent using Jamii Forums mobile app
Sio guarantee ukipata division one utafaulu ngazi za juu,inahitajika juhudi,kujitoa na uwezaji mkubwa sasa wewe jidanganye kwamba private schools kwasababu zinachagua vichwa basi zinalala tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…