Serikali idhibiti mfumuko wa bei

wazunguwawili

JF-Expert Member
May 29, 2019
3,984
4,131
Hali ya bei za bidhaa inadhidi kuwa tete.

Bei ya petrol, dizel imeongezeka kwa kiasi kikubwa. Zaidi ya sh 40 kwa lita.

Bei ya mafuta ya kula lita 5 kwa 50,000.

Yaa 10,000 kwa lita.

Kama inawezekana hata jeshi la polisi litumike kama ambavyo imewezekana sehemu tofauti.

Nakumbuka msako wa sukari, cement.

Natarajia hata ripot za benki kuu zitaonesha mfumuko huu wa bei.
 
Na bado!

Kumbuka huu ni msimu wa mavuno huko mikoani!

Subiri sasa kuanzia Novemba ujionee kiama
 
Suala la mfumuko wa bei ni jambo LA Demand and Supply, Serikali mwaionea tu.
 
Hii serikali inachoweza kwa ufanisi zaidi pasina shaka yeyeto ni kumkamata Mbowe na sio kupambana na shida za watz.
Hii serikali ipo autopilot,
 
Kuna aina nne za mfumuko wa bei.
1. Tax pushed inflation
2. Cost pushed inflation
3. Currency pushed inflation
4. Demand pull inflation.

Of all the four, Demand pull inflation is the worst ikifuatiwa na currency pushed inflation.

Pale kunapotokea ongezeko la kodi, bei za bidhaa huweza kwenda juu kidogo alafu baadaye zikatulia.

Pia panapotokea mabadiliko ya bei za bidhaa au malighafi kwenye soko la Dunia, bei za bidhaa nyingine huweza kuathirika. Hivi sasa nchi nyingi zimetoka kwenye lock down kwa hiyo bei ya mafuta kwenye soko la Dunia imepanda.

Pia, thamani ya sarafu inaposhuka, bei za bidhaa huweza kuathirika, hasa zile bidhaa zinazoagizwa kutoka nje, ama bidhaa zinazotengenezwa nchini kwa kutegemea sehemu kubwa ya malighafi kutoka ughaibuni.
 
Back
Top Bottom